TRA imetoa wapi mamlaka ya kugawa Sukari bure?

Nimesikia taarifa ya habari kuwa,Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi

Sakata la hii sukari lilianza Febuary mwaka huu,unaweza ukajiuliza
Tangu Februari hadi leo nini kilikuwa kinasubiriwa?

Je lini TRA imeanza kugawa BURE vitu vinavyodaiwa kodi?kwa hiyo kesho wakikamata gari ambazo hazijalipiwa ushuru watazigawa bure?

Je, wakikamata mafuta yatagaiwa bure?Haya yanayotokea ni madhara ya nchi kutokuwa na DIRA.

Tunakumbuka miezi miwili nyuma wimbo wa viongozi wote wa serikali kuanzia Dc,RCs,na wakuu wa idara zote za umma ulikuwa ni watumishi HEWA!

Suala la watumishi Hewa halijaisha limekuja suala la sukari sasa hadi TRA ambao sheria inawataka wakusanye kodi,ni mamlaka ya kukusanya kodi,wala sio kutoa vitu ambavyo havijalipiwa ushuru!

Kimsingi hii ni ishara na kielelezo cha Ombwe la uongozi,pamoja na ukosefu wa DIRA

Bila MAONO Taifa huangamia

Sasa ikiwa kila mamlaka ikikamata sukari inagawa humo humo mikoani ilipopata bure je itakuwaje mikoa ile ambayo sukari haikamatwi si watakoma kwa uhaba wa sukari?? Pili je kuna uhakika gani kuwa hiyo sukari imegaiwa yote ...je hao Maafisa wa TRA hawajachukua ya nyumbani kwao kama Gunia kila mtu??

Huu mchezo sasa
 
Siku nyingine kabla ya kutoa Uzi jf fuatilia kwanza habari husika na siyo kama hivi ulivyokurupuka Leo
 
Sasa ikiwa kila mamlaka ikikamata sukari inagawa humo humo mikoani ilipopata bure je itakuwaje mikoa ile ambayo sukari haikamatwi si watakoma kwa uhaba wa sukari?? Pili je kuna uhakika gani kuwa hiyo sukari imegaiwa yote ...je hao Maafisa wa TRA hawajachukua ya nyumbani kwao kama Gunia kila mtu??

Huu mchezo sasa
Hapo ndio penye chezo lote .
 
Achana na huu upumbavu unajiaibisha.Kaa kimya!
Jadili bila matusi!
TRA walikuwa wanadai kodi ya 200mil,kugawa bure ndio wamepata hiyo kodi?nipe mfano wa bidhaa iliyotaifishwa na kugawanywa bure.Wangeweza kutaifisha na kuiuza ili kupata hiyo kodi inayodaiwa!
Panua ubongo kabla kabla ya kupanua mdomo
 
Hoja yako inahamahama, tatizo lako Ni bora TRA wangepiga mnada hiyo Sukari kuliko kuigawa bure kwa taasisi? Najaribu kukuulewa mkuu!

Taasisi zilizopewa ujue huwa zinapewa pesa zinunue sukari.Ingeuza mzunguko ungekuwa ule ule ingepata pesa ambazo ingebidi wazitoe kwenye hizo taasisi zikanunue sukari!!! Mzunguko wote wa nini.TRA imekusanya sukari basi peleka moja kwa moja kwenye hizo taasisi kupunguza urasimu na mizunguko isiyokuwa na maana.
 
Kama ni Ya Magendo Na Haikulipiwa Ushuru Kuigawa na Jambo Jema Japo Imefanywa Kisiasa!
 
Nchi hii ina longo longo za kiwango cha chini sana ! Haya mambo ya kugawa ni lazima yahojiwe , unayakumbuka mabilioni ya jk ? Hatari mkuu ! Au kwa mfano unafahamu mtu yeyote aliyenufaika na mifuko ya WAMA au labda EOTF ?
 
Jadili bila matusi!
TRA walikuwa wanadai kodi ya 200mil,kugawa bure ndio wamepata hiyo kodi?nipe mfano wa bidhaa iliyotaifishwa na kugawanywa bure.Wangeweza kutaifisha na kuiuza ili kupata hiyo kodi inayodaiwa!
Panua ubongo kabla kabla ya kupanua mdomo
Wewe ndiye unatakiwa kupanua ubongo wako.

Hoja siyo kama hawajawahi kugawa bidhaa wanazozitaifisha, hoja ya msingi ni mamlaka ya serikali kugawa huduma au bidhaa bure kwa wananchi.

Wewe unadhani serikali inapotoa bidhaa bure kwa waathirika kama wa mafuriko huwa inapata wapi uwezo huo?

Unashangaza kweli.
 
Nimesikia taarifa ya habari kuwa,Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi

Sakata la hii sukari lilianza Febuary mwaka huu,unaweza ukajiuliza
Tangu Februari hadi leo nini kilikuwa kinasubiriwa?

Je lini TRA imeanza kugawa BURE vitu vinavyodaiwa kodi?kwa hiyo kesho wakikamata gari ambazo hazijalipiwa ushuru watazigawa bure?

Je, wakikamata mafuta yatagaiwa bure?Haya yanayotokea ni madhara ya nchi kutokuwa na DIRA.

Tunakumbuka miezi miwili nyuma wimbo wa viongozi wote wa serikali kuanzia Dc,RCs,na wakuu wa idara zote za umma ulikuwa ni watumishi HEWA!

Suala la watumishi Hewa halijaisha limekuja suala la sukari sasa hadi TRA ambao sheria inawataka wakusanye kodi,ni mamlaka ya kukusanya kodi,wala sio kutoa vitu ambavyo havijalipiwa ushuru!

Kimsingi hii ni ishara na kielelezo cha Ombwe la uongozi,pamoja na ukosefu wa DIRA

Bila MAONO Taifa huangamia
Hivi kweli na wewe unajiita mwanasiasa halafu hujui kitu kidogo kama hiki? Hivi chadema ni chuo cha ujinga? Tunajua mnafurahishwa sukari kukosekana lakini mtajuta!

Leo ndio nime amini Chadema mna mkono kwenye ufichwaji sukari! Kasome Mamlaka ya TRA! Wewe ni mjinga mjinga!
 
Jadili bila matusi!
TRA walikuwa wanadai kodi ya 200mil,kugawa bure ndio wamepata hiyo kodi?nipe mfano wa bidhaa iliyotaifishwa na kugawanywa bure.Wangeweza kutaifisha na kuiuza ili kupata hiyo kodi inayodaiwa!
Panua ubongo kabla kabla ya kupanua mdomo
Sio lazima waiuze wanaweza wakaigawa bure kama service tuu....jambo dogo kama hili linawasumbuaje Bawacha!
 
Mfanyabiashara mwenye kiwanda cha juisi lazima atakuwa na stock kubwa ya sukari kama mojawapo ya bidhaa za kiwanda chake.Je ni wakati gani unatambua aliyehifadhi sukari na aliyeficha?
QUOTE="Mdau Mkuu, post: 16142235, member: 20323"]1. Wafanyabishara nao wamepata wapi mamlaka ya kuficha sukari?
2. Je ni kifungu gani cha sheria kinamruhusu mfanya biashara kuficha sukari?

Yaani mie ndo hapa najishangaaga sijielewi au nalazimisha kutokuelewa.

Kable sijajibu swali lako nakwama katika maswali yangu hayo[/QUOTE]
 
Kama hujui Sheria kaa kimya....

Ina maana hujui kuwa TRA ina mamlaka kisheria

1: Kupiga fine bidhaa iliyoingizwa kimagendo AU

2: Kuitaifisha na kuigawa

3: Kuiuza?
kaka kila mtu sasa naleta mada kila mtu kishakuwa mwandishi wa JF jukwaa la Great Thinkers, hawa jamaa wa Jamii Forum wanatakiwa waondoe hilo neno jukwaa la great thinkers, sasa hivi kuna jukwaa la viabaka waandishi uchwara wasiofanya utafiti kabla ya kupost thread. Umuulize na yale magari wanayokua wanayapiga mnada mamlaka wamepewa na nani???
 
Sasa ikiwa kila mamlaka ikikamata sukari inagawa humo humo mikoani ilipopata bure je itakuwaje mikoa ile ambayo sukari haikamatwi si watakoma kwa uhaba wa sukari?? Pili je kuna uhakika gani kuwa hiyo sukari imegaiwa yote ...je hao Maafisa wa TRA hawajachukua ya nyumbani kwao kama Gunia kila mtu??

Huu mchezo sasa
jamaa wanajua kila mkoa kuna watu wameficha sukari ama watu watatupa kama wakati wa Sokoine ila mkuu kama upo mkoa ambapo hakuna sukari jitahidi kuamka mapema asubuhi ama zunguka usiku waweza kukuta dhahabu kikuangukia
 
Mfanyabiashara mwenye kiwanda cha juisi lazima atakuwa na stock kubwa ya sukari kama mojawapo ya bidhaa za kiwanda chake.Je ni wakati gani unatambua aliyehifadhi sukari na aliyeficha?
QUOTE="Mdau Mkuu, post: 16142235, member: 20323"]1. Wafanyabishara nao wamepata wapi mamlaka ya kuficha sukari?
2. Je ni kifungu gani cha sheria kinamruhusu mfanya biashara kuficha sukari?

Yaani mie ndo hapa najishangaaga sijielewi au nalazimisha kutokuelewa.

Kable sijajibu swali lako nakwama katika maswali yangu hayo
[/QUOTE]
Aisee unajiaibisha ndugu yangu. Kumbe wewe ni mjinga kiasi hicho!!!?
 
Hiyo meli iliyobeba shehena ilikamatwa tangu Januari na kulikuwepo pia bidhaa nyingine licha ya sukari. What a coincidence, bidhaa nyingine zimekutwa ziko expired kasoro sukari inayotafutwa kwa tochi
 
Back
Top Bottom