TRA imelala sana

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
314
Kama tunavyojua kodi nchi mwetu inakusanywa na TRA(Tanzania revenue authority) naona kama wamelala kimawazo au wanashindwa ubinifu wa kuongeza mapato yao ya kila siku kila mwezi kulifanya taifa lisiwe tegemezi kwa mataifa ya nje,world bank,IMF na mashirika mengine ya kimataifa.

Tanzania ni nchi yenye watu wanaokadiriwa milioni 50 bado tunasubiri report kamili ya sensa mwaka huu itatupa majibu tupo wangapi lakini cha kusangaza tunakusanya kidogo sana kuliko idadi ya wananchi na mali zetu nchini.

Kodi zetu kwa haraka zinatoka na mishahara ya waajiriwa,viwanda,makampuni,migodi(hapa tunadanganywa sana) na bidhaa kama chakula viwanji vya viminika.

Hivi nataka niwaulize TRA wanajua tanzania tuna watu wangapi wanapangisha nyumba zao na je wanawakata kodi hao watu.tuchukulie mfano ni wangapi wa nyumba osterbay,masaki,mbezi beach,njiro na maeneo mengine ambayo nyumba ni bei ghali.unakuta nyumba masaki ni dola 3000 kwa mwezi mtu anaingia pale analipia kwa mwaka mzima zaidi ya dola 36000 hivi sasa mtu ana nyumba hata 3 ambazo bei zake ni hizo je serikali imechukua kodi asilimia ngapi hapo.

Turudi huku mtaani sasa chumba 50000 unakuta mwenye nyumba ana vyumba hata 8 ina maana kwa mwezi ana 400000 je serikali inapata kodi kweli hapa maana naona nyumba nyingi unamlipa mwenye nyumba yenye anaenda lilipia kodi ya ardhi na nyumba ambayo ni 10000 tu.

Ni wakati sasa tuzijue nyumba zote za biashara serikali ukusanye kodi kwa kutokana na kile mwenye nyumba anachoingiza kwa mwezi na kwa mwaka ni wakati wa TRA kuanza kupita kwenye nyumba za watu na kuzisajili na kutoa vitabu mpangaji yoyote atakayelipa kodi awe anapewa risiti hii itaongeza kujua mwenye nyumba anaingiza kiasi gani.

Sijui kama kuna mfumo wa kuwabana wenye nyumba ambao wanaingiza pesa nyingi sana na hazilipiwi kodi kabisa ni uhakika kabisa hapa serikali inapoteza matapo na kungangania kuwabana wananchi kwenye vyakula na vinywaji.

Kingine kuna wakina mama wana migahawa barabarani sehemu za vitu kwa kuwa wanauza chakula hawakwati kodi jiulize kuna vijana wana vibanda vya chipsi kwa siku wanaingiza faida ya 20000-50000 je serikali inapataje kodi zao.

Ni wakati wa TRA kuandaa mfumo kwa wafanya biashara wote wenye vibanda barabarani kukatia TIN no na kufungiliwa account kwenye mabenk yaweke huduma nafuu ili hizi pesa zinazoenda kuwekwa nyumbani ziwekwe kwenye mabenk.

Mimi nadhani kama hawa kina mama,vijana wote watakatia TIN no hata TRA wakipata 2000 kwa mwezi kwa biashara na hizi hela wanazokusanywa wakaelezwa umuhimu wake wawe wanaziwekwa benk nchi yetu itapiga hatua kubwa sana tuseme mimi kijana nauza chips ninapata faida ya 30000 kwa siku labda kwa wiki naenda kuhifadhi bank 100000 kwa mwezi nina laki 4.sijaimalisha maisha yangu kuliko kukaa na ile hela nyumbani tu.

Hii itasaidia vipi hawa kina mama na vijana
1.Hela zinakua safe
2.Unaweza chukua mkopo upanue biashara yako
3.Ukipatwa na shida ni rahisi kuzichukua hela kuliko kukaa nazo unaweza kuwa na matumizi ya ajabu.

Shime kwa TRA kufanyia tafiti hizi nyumba za wapangaji,biashara ndogo ndogo na kukusanya mapato.

Tanzania bora italetwa pale tutakapolipa kodi

Fred kavishe
 

blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,217
422
Mkuu, usiombe mama ntilie na wenye nyumba wapigwe kodi!

Wewe Mfanyakazi ndie utakae umia kwa sababu wewe ndie uneyehitaji hicho chakula na wewe ndie unayepanga hizo nyumba.

Sana sana hawa watu watatafidia kwa kukupandishia chakula na kodi ya nyumba.

Sijui kama unajua kwamba Tanzania watu wasiolipa kodi ni wafanyabiashara wakubwa kama wa mahoteli makubwa, viwanda, migodi nk

lakini wewe unataja mtu masikini aongezewe kodi!
 

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
314
Mkuu, usiombe mama ntilie na wenye nyumba wapigwe kodi!

Wewe Mfanyakazi ndie utakae umia kwa sababu wewe ndie uneyehitaji hicho chakula na wewe ndie unayepanga hizo nyumba.

Sana sana hawa watu watatafidia kwa kukupandishia chakula na kodi ya nyumba.

Sijui kama unajua kwamba Tanzania watu wasiolipa kodi ni wafanyabiashara wakubwa kama wa mahoteli makubwa, viwanda, migodi nk

lakini wewe unataja mtu masikini aongezewe kodi!

Wote hata wafanyakazi wakubwa watoe kodi huo ni ushauri tu najua wafanyabiashara wakubwa hawatoi kodi ni wakati TRA kuwabana
kama umenielewa vizuri ni kuboresha maisha ya mama lishe na kuiongezea serikali mapato.kwahiyo wewe unaona sahihi kabisa watu waendelee kuingiza pesa za kupangisha nyumba bila serikali kukata kodi.
 

silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
903
853
mkuu badala ya kuhimiza rasilimali zitumike kwa maslahi ya taifa wewe unataka masikini waengezewe kodi. mabilioni mangapi yanaibiwa na mafisadi kila kukicha?
kwanza gangamala hela za Richmond, Epa, Rada, mabilioni ya uswisi yarudi halafu ndo useme masikini watozwe kodi. kwani kwa mfumo uliopo hata wakitozwa zitaishia mifukoni mwa mafisadi.
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,096
14,444
Tatizo la mapato kwa watanzania ni Tatizo la kisiasa zaidi na itikadi ya chama kilichopo madarakani (CCM) ndiyo mwamuzi.

- TRA inapoteza mapato mengi sana kwa kuhujumiwa na wanasiasa uchwara kwa mikataba feki.

-TRA inahujumiwa kwa msingi wa wafanyabiashara kukwepa kutoa kodi kulingana na thamani ya biashara zao (chama kinawalinda) sababu wanakichangia tena wengi ni wanachama kwa jina la heshima ya kifisadi -Kada

- TRA wenyewe hawaeleweki, kutokana na siasa mbuvu wanakula rushwa sana kufanya makadrio fyongo/kidogo (wanapunguza mapato)

- TRA wamekamatwa na wafanyabiashara hasa wanasiasa na kuwaacha kufanya biashara bure! kwa kupeana kitukidogo

Upuuzi wa TRA umepinda mgongo kutolea macho kodi za wafanyakazi (Akili yao imeishia hapo ikiacha matajiri kujifanyia watakavyo)

Sio sahihi kwa mtazamo wangu, kuwabana watu wachini kutoa kodi tukiwaacha matajiri kupeta bila aibu na migodi kujibebea

dhahabu na madini mengine bure. Ni kukosa fikra pevu kuwafata maskini. Ieleweke wazi mlaji yaani maskini ndiyo mtu anayebeba

mzigo wote na wafanyabiashara hayawahusu maana kila hasara wanayoihisi wanafidia kwa kupandisha bei ya bidhaa na mwisho

wa siku mlalahoi/mlaji ndiye huchukuwa mzigo wote.
 

silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
903
853
kuna jamaa alikodishwa jengo la umoja wa vijana CCM maarufu youth league (sie tunaliita yuslik) liliopo eneo la darajani Zanziba. ni jengo ambalo lilikuwa linahitaji marekebisho.

Basi jamaa kwa vile ni jengo la CCM akaliombea msamaha kontena 500 za saruji. wakati matengenezo halisi ata kontena moja tu ambalo lina pakiti 540 basi lingetosha.

sasa jamaa baada ya kupata msamaha huo akawa anakula dili na wafanyabiashara wa saruji , na kwa kutumia msamaha huu akafanikiwa kutoa kontena zaidi ya 100 BUuUurReee. baadae mawakala wa forodha wakashtukia mchezo jamaa ndo akastop. na mpaka leo hii jengo hilo bado halijamaliza ukarabati. kwa iyo hii nchi we acha tu
 

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,285
7,307
Sijui wala mabilionia 10 kwanini hawapo katika walipa kodi 10 wakubwa,jamani hata gazeti la Raia Mwema linawshinda kwa kulipa kodi,lenyewe ni kati ya walipa kodi wakubwa katika kituo cha TRA cha Manzese,tunataka pia hao Masharo Bilionia wafanye kama walivyofanya gazeti la Raia Mwema.Nikiangalia hao Masharobilionia 10 hata sura zao zinatosha kuonyesha kuwa hawalipi kodi ,wamekaa kiujanjaujanja,wanakampuni kibao zinazoanzishwa na kufa bila kufanya shughuli zozote na sifa ingine kubwa waliyoayo hao matajiri ni kila kukicha wana migogoro ya kesi kwenye taasisi za fedha,na pia huwalipa wafanyakazi wao mishahara mbuzi na mwisho wanapenda kujionyesha makanisani,misikitini na kwenye runinga,huko CCM na kujifanya ni watu wakarimu sana na wanatii mamalaka ya nchi
 

blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,217
422
Wote hata wafanyakazi wakubwa watoe kodi huo ni ushauri tu najua wafanyabiashara wakubwa hawatoi kodi ni wakati TRA kuwabana
kama umenielewa vizuri ni kuboresha maisha ya mama lishe na kuiongezea serikali mapato.kwahiyo wewe unaona sahihi kabisa watu waendelee kuingiza pesa za kupangisha nyumba bila serikali kukata kodi.

Mkuu nachotaka hapa uelewa ni kwamba kwenye kodi za aina hii atakayelipa na kuumia zaidi ni mpangaji au mtu anayenunua chakula.

Mfano kama nyumba yangu napangisha kwa laki moja basi kama kuna kodi ya serikali labda asilimia 15 basi nitapangisha nyumba hii kwa laki moja na kumi na tano elfu. Atakayelipa hiyo kodi si mwenye nyumba, ni wewe mpangaji.

Na hivyo hivyo kwenye chakula. Sijui Mkuu umenielewa. Hata kwenye mfano VAT, anayelipa ni wewe unayenunua na kutumia kile kitu mfano nguo. Mfanyabiashara halipii kodi. Kodi anayelipa ni wewe mtumiaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom