TRA Arusha Wamegoma!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA Arusha Wamegoma!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mwana Kwetu, Jul 24, 2012.

 1. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Tangu juzi hapa TRA Arusha huduma ya kuprocess Driving licence kitengo cha kupiga picha na finger print hakitoi huduma yoyote licha ya wateja kuwa kwenye msururu bila kupata huduma yoyote. Leo ni siku ya tatu na kisingizio kinachotolewa ni kwamba eti MTANDAO HAMNA.

  Watanzania wenye akili hawawezi kuamini wala haingii akilini kusitisha huduma kwa siku 3 kwa kisingizio cha kutokuwepo kwa mtandao. Habari za kuaminika zinasema kuna ka mgomo baridi na suala la mtandao ni kisingizio tu. Na ikithibitika kuwa si mgomo ni mtandao kweli basi hii itamhusu sana huyu mama aliyepo kwenye hiki kitengo kwani kila mtu huwa anamlalamikia kwa jinsi alivyo na nyodo na kufanya kazi kama vile yuko nyumbani kwake.

  Kuna wakati anawaona wateja kama omba omba wanaohitaji msaada kwake na hivyo huonyesha dharau bila kujua hao walipiga foleni ndo wanampa justification ya kupata kipato.

  Kwa ufupi shughuli zote za upigaji picha na finger print kwa ajili ya Driving Licence hapa Arusha TRA zimekwama tangu juzi.
   
 2. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kweli kwani jana jioni nimefika pale kupata hiyo huduma nikakuta watu kwenye que na hakuna kinachoendelea na kuelezwa kuwa No network. Leo asubuhi nikawahi mapema lakini nikaelezwa tena hakuna network na hilo jibu halielezi mtandao utarudi saa ngapi au lini. Haiwezekani Meneja akaendelea kujikalia huku huduma nyeti kama za Leseni zikikwama na kusababisha watu kupoteza muda wao kuja kukaa foleni bila kujua hatima ya mtandao.
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ni bora wangeweka tangazo kuwahabarisha watu pale nje kuliko kuwaweka watu kwenye foleni muda mrefu wakijua hakutakuwepo huduma siku nzima
   
 4. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Leo asubuhi wazungu waliokuwa kwenye foleni ndio waliodokezwa tu wakaondoka na wengine wanafuatilia kupigwa picha tangu wiki iliyopita bila mafanikio
   
 5. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Labda wanatengeneza mazingira ili wapate kitu kidogo kwa sababu teknolojia ya kutumia mandao inawanyima ulaji. Baadhi ya wafanyakazi wa hiki kitengo ni TATIZO kwani hata utendaji siyo mzuri kiuduma kwa hiyo kama mtandao umekatika kwao wanafurahia bila kujua wanahatarisha kazi zao
   
 6. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Ina maana huo mtandao wao ambao unaharibika siku tatu bila kutengenezeka una tofauti gani na mitandao mingine kama ya CRDB ambayo haiwezi katika siku nzima? Lazima kuna uzembe mkubwa kwa upande wa hiyo idara na ikiwezekana stahili ya hao watu warudishwe tu reception au kutoa fomu la sivyo hako ka ugonjwa katageuka kansa
   
 7. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sidhani kama ni mgomo yawezekana kweli mtandao hakuna na hilo ni suala la kawaida tu...cha msingi wangewka tangazo la tatizo hilo ili kuepuka foleni...
   
 8. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Kwa siku 3 kuna zaidi ya watu 200 wameshindwa kuhudumiwa na kwa hivyo serikali imepoteza kiasi kikubwa cha mapato. Kwa bahati mbaya wanaotoa huduma na hata meneja wa TRA anaona hilo ni jambo dogo wakati mshahara usipopandishwa kutokana na kukosekana mapato waliyokwamisha wao wanaanza kulalama bila kujua sababu ni wao wenyewe.
   
 9. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,964
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Mtandao wa ttcl upo chini, baada ya mkonga wa mawasiliano kwenda mikoani kukatwa na mkandarasi anayejenga barabara ya Morogoro tangu wiki iliyopita.
   
 10. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Inawezekana ni kweli ila inasikitisha kwani hiki kitengo cha kupiga picha na kuchukua finger print ndicho kinachotegemewa mkoa mzima wa Arusha ni kwa jinsi gani kwa siku tatu mfululizo na inawezekana kikaenda hata wiki nzima mtandao unakosekana? Licha ya tangazo kuwekwa lakini bado uwajibikaji wa idara mzima umekuwa wa kizembe sana ktk kutatua jambo hili
   
 11. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tatizi la mtandao siku tatu hiyo itakuwa ofisi au kijiuchochoro , maana nijuavyo technologia lazima kuwepo na alternative network kama moja wapo inakuwa iko down na hao wanaotoa support wako hapa hapa bongo au ndio wamekata ticket kutoka marekani waje kutatua tatizo ,hii nchi ina vijimambo kweli hatuko hapa kwa bahati mbaya bali ni makusudi ya watawala tuwe masikini.
   
 12. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wakuu tusilaumu bure ni kweli kabisa TRA kuna tatizo kubwa sana la network na sio Arusha tu karibia mikoa yote yaani mpaka hata Tin huwa zinachelewa lazima wabadilishe system yao ya network
   
 13. Lord K

  Lord K JF-Expert Member

  #13
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwaiyo ukitaka info uende na mzungu.......ukoloni bado sana kuondoka.
   
 14. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Tatizo nchi imekuwa kama familia ambayo haina baba na hivyo kila mtu anaamua kufanya anavyotaka akijua hakuna wa kumkemea. Siku tatu hakuna mtandao huu ni uchuro ambao hautaeleweka ukimweleza mtu halafu kesho serikali inalalama mapato yameshuka
   
 15. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Visingizio vingine vimekaa ki-uswahili mno kwa sababu mbona tunatumia TTCL broadband, tigo.voda, zantel na air tel internet zinafanya kazi tena kwa speed tu kubwa? Kwani huu mtandao wao ni special?
   
 16. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #16
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaka, huo mgomo usije ukawa na uhusiano na kutekwa nyara kwa pesa za NSSF/PPF, si unajua hili linamhusu kila aliye ajiriwa?
   
 17. s

  sambu JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Kwa hiyo ni kawaida TRA kuwa na mtandao siku tatu mfululizo????? Watanzania ebu tuache utani tusichekwe kila siku. haikubaliki kuwa majibu mepesi kiasi hiki. Ebu hesabu manhours ngapi zinapotea kwa kisingizion hiki?
   
 18. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #18
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yaa!!!biometrics ndicho kinachotegemewa kwa suala zima la TIN vuta subira nina imani wahusika wanasikitika pia kwa kupoteza mapato lazima watakuwa wanashughulikia kuwa na subira...
   
 19. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kaka mtandao umerudi...nenda
   
 20. A

  Anold JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  TRA huwajui? hiyo ni mali yao binafsi! wanafanya bidii kwa kazi zenye tija, hapo ukienda kilokole utaopewa leseni hata ya daraja F japo umeshamiliki leseni ya Daraja c kwa miaka 10, ila ukipenyeza rupia utaweza kuona jino la pembeni la huyo mama unayedai ananyodo. Mbona kuna vishoka hapo ukiwapa chochote kitu utashangaa mtandao unafanya kazi. Hao hawaguswiiiiii. Ndiyo maana chi hii inahitaji sana mabadiliko ili kujenga mfumo kwanza, maana hapo ndio kwenye tatizo!!!
   
Loading...