TPN - Hafla ya Kujumuika Pamoja Jumamosi 28 Februari 2009 Saa 11 Jioni Mwanzo Lodges | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TPN - Hafla ya Kujumuika Pamoja Jumamosi 28 Februari 2009 Saa 11 Jioni Mwanzo Lodges

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Sanctus Mtsimbe, Feb 25, 2009.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wana JF na Wazalendo;

  Karibuni Tujumuike Pamoja:

  [​IMG]

  Kwa niaba ya TPN napenda kuwakaribisha wote katika Hafla ya Kujumuika Pamoja itakayofanyika siku ya Jumamosi Tarehe 28 Februari 2009 kuanzia Saa 11 Jioni katika Hoteli Mpya ya Kitalii ya Mzalendo Mwenzetu inayoitwa Mwanzo Park Lodges | Mkuranga - Tanzania Kongowe njia ya kwenda Mkuranga kupitia Mbagala.

  Kutakuwa na Chakula cha Jioni na Muziki na mambo mengi ya kuvutia, Na pia ni nafasi ya pekee ya kuonana na Wazalendo mbalimbali na Wanataaluma tofauti na kufahamiana. Pia Tutajulishana juu ya Maendeleo ya Mkakati wa kufanya “TZ DIASPORA SUMMIT” Mwezi wa December 2009. Utakuwa ni usiku wa pekee ambao si vema ukakosa.

  Gharama za ushiriki ni TZS 25,000 kwa mmoja au TZS 40,000 kwa “Couple”.

  Kwa confirmation - Wasiliana na:
  Laila Mohammed
  Tel: 255 754 277 335
  255 713 201 204
  Email: laymohd_tpn@yahoo.com
   

  Attached Files:

 2. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,754
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kaka Sanctus nashukuru kwa mwaliko ... Nimepata bahati ya kipekee kabisa kutembelea Lodge hii baada ya kuona katika Blog ya Sankofa... na kusema ukweli `its a home away from home...` Hafla njema...
   
 3. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mzalendo Tusker Bariiidi;

  Hakika mwenzetu huyu amekuwa mbunifu sana na ni busara tukamuunga mkono. Mbali na mandhari nzuri, pia ni mahali mwafaka kwetu kukakaa pamoja, kuongea na kujifunza . . . . Tunajivunia hatimaye kuwa na sisi Watanzania tunaweza kufanya vitu vya uhakika . . . .

  Kutakuwa na mengi ya kuvutia na kubadilishana mawazo . . . . Karibuni sana. Kwa watakaopenda kuona site yao, wanaweza kutembelea kubofya hapa: Mwanzo Park Lodges | Mkuranga - Tanzania
   
 4. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wazalendo;

  Nimekuwa nikiulizwa juu ya namna ya kufika Hotel. Naambatanisha site map:

  [​IMG]


  [​IMG]
   

  Attached Files:

 5. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Asanteni sana . . .

  Namba ya Waliothibitisha ni nzuri sana . . .

  Nashukuru wote kwa kuitikia mwito. Kwa wale wa dakika za mwisho bado mnakaribishwa pia.

  Wasalaam.
   
 6. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Sanctus,

  Kwanza nipo Nchini,Nipo eneo la Chuo kikuu sehemu ya mlimani kukutana na baadhi ya ma-Comredi wa muda mrefu na rafiki zangu.Na wamenihakishia aJamiiforums inapatikana hapa tofauti na maneno ya ya mzee mwanakijiji.

  Hapa nipo kwenye chumba cha Prof. mmoja ambaye pia ni mwanachama wa JF,tunajadili ishu mbali mbali kuhusu mstakabali wa nchi hii na maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2010.

  Kuhusu TPN
  1.Ningependa kujua mpaka sasa mmefanya kitu gani kusaidia Taifa katika suala la ICT?

  2.Ningependa kujua mtazungumzia nini huku katika hiyo hoteli,.

  3.Nani atatoa maada na siyo suala la kusema kutakuwa na Mziki na get together(lengo lenu na imekuwa tabia ya watanzania wengi)...Suala la msingi mnalotakiwa kufanya ni kujadili mambo muhimu yahusuyo Taifa letu na hata ikiwezekana mjadili kwa siku nzima bila kuwapo matukio mengine yasiyo ya muhimu.

  My Take
  Inavyoonessa hiyo ni deal vtu na vielelezo vya kuwa kuna vyumba ya double na single inaonesha mnataka watu wakapumzike tu huko na nyie mfaidike.

  Sanctus nakufahamu sana kwa muda mrefu hata kabla haujaja nchini,kwa kusoma baadhi ya vitu ulivyoandika na hata kwa kusikia na kukuona ukiongea.Binafsi kukuona kwako na wewe kuwa na shahada yako ya kwanza ambayo siyo ya mambo ya IT wala ICT,Nakuona kama optunist mwwenye lengo binafsi(kama Wahindi).

  Nachoana ni kuwa ,Kungekuwa na chombo muhimu chenye wataalam wa ICT hapa Tanzania,Hata vitu kama Vitambulisho vya kitaifa vingeanzia hapa.Ila TNP imejaa watu wale wale ambao wamekuwa wakiipeleke serikali yetu katika gharama kubwa zisizo na msingi(nyingi za kifisadi).

  Kuna watu kama kina sawe ambao wamekuwapo pale UTUMISHI kwa muda mrefu ial hakuna chochote ambacho wanweza kujisifia.

  TNP ni kama kijiwe cha kisiasa ambacho kimekosa mwelekeo.

  Wapi tunatakiwa tuelekee

  Tunahitaji umoja wa kaifa katika kumaliza matatizo yanayotukabili katika njanja zote.Kuanzia siasa hadi huku kwewnye ICT.
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hizo pesa za kujenga hiyo lodge zilitokana na nini??? Nitashiriki kama nitahakikishiwa kuwa hakuna aliyepoteza uhai kwa kusingiziwa kesi au kupigwa risasi au kudhulumiwa mali zake au kama si kutokana na fedha za madawa ya kulevya.

  Who are the shareholders of this lodge???? Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh patamu hapo.
   
 8. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sanctus, this is rather a short notice. If this occasion wasn't announced earlier than it currently appears, I think i won't be far fetched to call it "an unprofessional invite" since it concerns TPN. Convince me otherwise please....!! :(
   
 9. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #9
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Du! Duuuu!

  I love JF always there are issue and issues.

  Asante sana Gembe kama unadai ujanifahamu kweli. Binafsi sina cha kuficha.

  Kama umewahi kusoma mabandiko yote ya TPN hapa JF au kuona kile ambacho TPN imefanya mpaka sasa na bado ukaona post yako imetulia basi, kweli kutakuwa kuna haja ya kupata mchango zaidi.

  So, let me start by saying, kuna post nyingi sana za TPN na hata reports ambazo maswali yako yote uliyouliza na issues ulizozitaja zimejibiwa vizuri. Can you be kind enough uzipitie post hizo kwanza na kama kuna hujaridhika basi I will be happy to take your challenges.

  I wish if you really know me or TPN and what we do . . . maana uliyoyaandika ni the opposite. I challenge you to come on the event or any other TPN events and see for yourself what is being done.
   
 10. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu,

  Mwekezaji huyu ni Mzalendo kama mimi na wewe na nijuavyo mimi kapata mkopo. Unaweza kumpata na kumwuliza maswali mengine yote. Contacts tembelea tovuti yao.

  Si vibaya wakati mwingine tukiyaangalia mambo kwa mtazamo chanya. Only if you choose to understand.
   
 11. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #11
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Steve;

  Mialiko hii imewafikia members wote wa TPN kuanzia mwezi moja uliopita. Pia kumekuwa na Invitation kupitia Media na Websites mbalimbali.

  Hata hivyo Mwanataaluma na mtu yeyote anakaribishwa kushiriki. TPN is not a closed organization.
   
 12. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu Sanctus Mtsimbe, aliyosema Gembe hujajibu yote, usikimbilie kwamba kila kitu kipo hapa JF. Huo ni udhifu, kama kipo basi ungeweka link, swali hili utaliapata kwa link hii, na swali lile utalipatakwa link ile.

  Unaulizwa nani atatoa mada?, ina maana hata hili jibu la hili swali TPN kupitia kwako mlishalituma JF?. Jibu maswali, usilete majibu rahisi rahisi katika maswali magumu.

  Mawazo ya Gembe yana maana kubwa, kukutana tu sio tatizo, watu wanakutana hata mitandaoni, lakini jee baada ya kukutana mnalisadia vipi Taifa. Mnaweza hata kukutana mara 100, ikawa ni kupoteza muda tu, bora mngekutana pale Metropol, Musoma ama Ukumbi wa Uhazili, Tabora mkacheza dansi mkaenda zenu. Kuliko mnapoamua kukutana wanataaluma, halafu lengo liwe tu kujuana na muziki. Mkusanyiko kama huo kama kun mada zinatolewa, na kuchangia halafu mnakuja na malengo utakuwa na faida kubwa.

  Sasa hata hiyo fedha TZS 25,000 kwa mmoja au TZS 40,000 kwa wawili, hii nayo inapunguza wahudhuriaji. Watu TZ wanamaliza shule na hawana kazi, na hata kama tunapata kazi kipato ni kidogo, sidhani kama nitatoa hiyo fedha wakati mwanangu anataka nauli ya daladala. Mngekuwa kwa mambo muhimu ili kupata washiriki wengi mnafanyia katika kumbi kama Nkuruma pale UDSM ama ukumbi wowote ulio karibu na jiji.

  Ila jibu maswali ya Gembe, kama umewekatangazo hapa, tunataraji pia utakuwa na majibu. Usikwepe maswali.
   
 13. M

  Mama JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Watanzania bana, eti hafla ya kujumuika.

  TNP wanajumuika, wamekosa kazi ya kufanya na hawana mambo ya kudiscuss bali kujumuika ili kumuunga mkono mzalendo mwenzao!

  Ama kweli tuna safari ndefu sana.
   
  Last edited: Feb 27, 2009
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Mama:

  Networking ni kitu muhimu sana.
   
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  .... pale kinapofanyika (preferably si kwa gharama kubwa sana) na kuleta matunda
   
 16. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Unayoongea ni muhimu sana. Gharama za information ni ndogo na ndizo ziletazo matunda.

  Hila kitu kinachoni-bore kuhusu watanzania, ni kutopeana information za kuendelea. Hapa ninapokaa nakutana na naongea sana na watanzania lakini sioni mtu kastua kuwa kuna kitu kinachoweza kufanyika zaidi ya ubishi wa mambo ya siasa za kimataifa.
   
 17. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu zakumi,

  Mambo haya ya networking kwa nchi yetu ndiyo yamezaaa ufisadi ambao haujawahi kutokea.Mtandao wa kina RA nao ulianza hivi hivi kama TPN.
  Kuna sehemu nyingi sana za kufanya mihadhara bila ya kuwa na gharama kubwa na mie nitakuwatayari kuwaombea.

  sehemu kama nkurumah pale chuo kikuu cha dar esa salaam mnaweza kupata.tyatizo mind za watanzania zimejaa upuuzi mmoja kwamba kila hafla au semina lazima pesa nyingi zitumike na hakuna mtu anayefanya review baada ya hiyo mihadhara.

  we need a change.

  Mkuu Mfumwa tupo Mstari Mmmoja.Sanctus amevwatuka tu na hana hoja zaidi kaleta vioja.aweke CV yake hapa
   
 18. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #18
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Viongozi na Wazalendo;

  Nimewasoma. Mafikirio yalikuuwa huenda huko nyuma mmekuwa mkipitia mabandiko yote ya TPN. Nadhani nimekosea si wote wanafanya hivyo ingawa kwa hakika najua kuwa maswali haya yameulizwa mara nyingi sana na yamejibiwa kwa kiwango cha kuridhisha.

  Tuanze upya:

  Links ambazo maswali yanayofanana na hayo yaliulizwa na pia tazama report iliyoambatanishwa:

  https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/15629-jamii-forums-karibuni-tanzania-professionals-network.html

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/22659-idea-hold-tanzanians-diaspora-summit-december-2009-a.html

  https://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/16002-tuzo-kwa-mtanzania-aliyefanya-vyema.html

  Katika ICT: Hatujafanya mengi sana kwani TPN imeanza Mwishoni mwa Mwaka 2007. Hata hivyo kuna machache yaliyofanywa:

  - Kupitia baadhi ya members wake, tumeshiriki katika kuandaa mkakati wa Mkonga "Optic Fiber" ya ndani ya nchi ambayo muda si mrefu.

  - Maandalizi ya report ya mkakati wa utekelezaji wa Bill Gate/JK MoU ya kusaidia ICT katika area ya Elimu, Tourism na E-Government.

  - Na sasa tunashirikiana kwa karibu na COSTECH kuandaa mkakati ni vipi Science na Technology vitasaidia kuondoa umasikini. Katika hili DG wa COSTECH atakuwepo katika hafla pia kuongelea ni wapi tumefikia na nini tutafanya pamoja.

  - Maandalizi ya Diaspora Summit December 2009. Angalia Link hapo juu.
  - Maandalizi ya Tuzo ya Mtanzania aliyefanya vema. Angalia Link hapo juu.
  - Wazo la mkakati wa kutunisha mfuko kupitia Carnival Festivals za Tamaduni za kitanzania ili kuanzisha VIJIJI VYA KIJASILIAMALI na INCUBATORS CENTRES.
  - Networking kwa ajili ya Ujuzi, Mitaji na Masoko.

  TPN katika mwaka huwa tuna Networking Events zenye watoa maada walau mara moja kwa miezi miwili. Pia tunashirikiana na British Council ambapo kila mwezi kuna maada mbalimbali.

  Katika event ya sasa nia ni kujumuika na kutumia muda mwingi watu wafahamiane zaidi na kunetwork. Hata hivyo kutakuwa na waongeaji (Very Briefly)wafuatao:
  - DG wa COSTECH
  - Director wa UDEC ambao mwaka huu TPN imeshirikiana nao kufanikisha mashindano ya BUSINESS PLAN iliyoshirikisha wajasiliamali zaidi ya 350 na ambao tunaweka mikakati ya kuinuana.
  -MATRON wa TPN
  -Mwakilishi wa TPN
  - Kutakuwa pia na Interraction

  Hakuna mtu anayekuzuia kufikiria utakavyo. Wewe ni kiumbe huru.


  Nashukuru kama unanifahamu. Kama nilivyosema siwezi kukuzuia kufikiri utakacho. Ni kweli kuwa sina shaada ya kwanza ya ICT na kama unanijua utagundua kuwa mpaka namalizi shahada yangu hakukuwa na course za ICT zaidi ya Options katika Faculties mbalimbali. Kwa kuwa unanifahamu, bila shaka unajua shahada yangu ya kwanza na ya pili nilisoma nini na wapi.

  Opportunisti mwenye Malengo Binafsi - hilo nakuachia wewe ufikiri utakavyo. Hata hivyo records zangu na wale ambao nimefanya nao mambo mbalimbali, zinapingana kabisa na wazo lako.

  TPN na wala si TNP kama unavyoiita na Mtandao wenye madhumuni makubwa wa kuwafanya wanataaluma washirikiane na kubuni mikakati ya kuwezeshana kiuchumi. Unaweza ukapitia hapa:TPN - Homepage

  Nijuavyo kuna vyama mbalimbali vya kitaaluma na hata cha ICT kipo na kina viongozi wake. Kwa maoni yangu vyama visivyo vya kiserikali NGO vinaweza tu kuishauri serikali au kuweka pressure.

  Kama una ushahidi kuwa TPN imekuwa ikiipelekea serikali katika gharama kubwa, si vibaya ukitoa ufafanuzi ili tuamini unachoandika. Nijuavyo mimi, mengi unayoongea kuhusu TPN ni kinyume cha tunayoyafanya na kupanga kuyafanya.

  Siwezi kumjibia Sawe. Ila najua kuna mazuri mengi aliyoyafanya pia. Just for interest Mzalendo Gembe: Ni nini ambacho umeifanyia Nchi ambacho wewe binafsi unaweza kujisifia na TPN ijifunze kutoka kwako?

  TPN kama inayojitambulisha, haina mlengo wa Kisiasa, Kidini, Kijinsia, rangi wala mwegemeo wa namna yoyote. TPN si Kijiwe ni mtandao unaohusisha watanzania walioko ndani na nje ya nchi. Na ndiyo maana pia tunaandaa Diaspora Summit.

  Nashukuru kama umeliona hilo. Hicho na mengine ndiyo TPN inajaribu kufanya. Tuungane mkono itapendeza zaidi. Kama kunamapungufu, tusaidiane na kusahihishana. Nadhani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuendelea mbele. Kama kuna tofauti na unachofikiri, bado unaweza kutoa mawazo mbadala na yakafanyiwa kazi.

  Karibu sana Mzalendo Gembe.
   
 19. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #19
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mzalendo Mfumwa;

  Kwa heshima na taadhima, nimemjibu Mz. Gembe. Sikujua kuwa kuna kazi sana kupata links nilizoomba mzirejee maana ukibofya tu jina langu hapo juu, unaona Thread zote nilizozianzisha. Hata hivyo usijali sana.

  Kama umesoma majibu yangu kwa Gembe bila shaka nitakuwa pia nimejibu swali lako. Hakika TPN tunapokutana huwa inakuwa ni mikakati ya kutenda tu, na tunashukuru kuwa hilo linatokea. Hata hivyo kama una mawzo zaidi ya kuboresha unakaribishwa sana.

  Ndugu yangu, hapo tunapokutanika ni moja ya sehemu ya mafanikio ya mikakati ya TPN hata wakaweza Ku-Invest kupitia networking yetu ya kuwezeshana KIJASILIAMALI, KIMITAJI na KIMASOKO. Je, si vema kumuunga mkono na wengine kujifunza toka kwake. Si vema kujua amefanikiwa vipi?

  Jambo lolote uaweza kuliangalia katika namna mbili. NEGATIVE au POSITIVE. Eventi hii ni kwa ajili ya Networking zaidi na tunafanya hivyo mara moja kwa mwaka. Au ni dhambi TPN kuonana katika Social event? Je, 40,000 kwa couple au 25,000 kwa mtu kwa gharama za chakula na maandalizi yote na yote yatokanayo na Event hii haifai? Bado unaweza kutoa mawazo mbadala.

  Nashukuru kwa ushauri. Done. QED.
   
 20. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #20
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mama;

  Nini kimetokea kwako? Una Posts: 2,576 lakini bado ni Senior Member? I thought > 250 makes you Senior Member. Au kuna namna?

  Hafla ya Kujumuika ni GET-TOGETHER EVENT. Nimeeleza pia ni nini kitafanyika. Naomba usome majibu kwa Gembe. Pia umuhimu wa sisi wenyewe kutiana moyo pale moja wetu anpofanya jambo jema.

  Kama una mawzo mbadala. karibu sana. Tutakusikiliza.
   
Loading...