TPI yakana kutengeneza ARV bandia

KIGENE

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,552
813
KIWANDA cha Tanzania Pharmaceutical Indusrties Ltd (TPI), kimekanusha kuhusika na usambazaji, uzalishaji wa dawa bandia za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV's).

Kiwanda hicho kinachomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali asilimia 40 na wamiliki wazawa asilimia 60, kimesema kuwa kinazalisha dawa ya TT-VIR 30 na si TT-VR30 ambayo ni bandia huku utaalamu wao wakiupata kutoka nchini Thailand.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TPI, Zarina Madabida, alisema kuwa kiwanda hicho hakijawahi kutengeneza dawa hiyo.

Madabida ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum (CCM), alisema kuwa kiwanda hicho hakiwezi kutengeneza dawa bandia ikizingatiwa kuwa ni teknolojia yao inachanganya dawa na kuwa katika muonekano mmoja na si rangi tofauti kama dawa hizo bandia.

Badala yake, mbunge huyo alihusisha tuhuma hizo na harakati za kuchafuana ili kiwanda hicho kifungwe. Alisisitiza kuwa kutokana na hali hiyo wanaunda timu yao ya uchunguzi kuhusiana na jambo hilo ili wajue nani aliyefanya mchezo huo wa kiuaji na wakishetani na kwamba hawatakubali mpaka wezi hao wakamatwe.

Madabida aliongeza kuwa anashangazwa na dawa hizo kukamatwa Agosti wakati wao dawa zao zilipelekwa kwa msambazaji (MSD) Machi 2011.

"Mimi nashangaa sana sisi dawa zetu zilitoka Machi na muda wote huo hatujatengeneza, sasa iweje zionekane feki Agosti?
Alihoji na kuongeza kuwa "hatuwezi kuua ndugu zetu wala kuharibu biashara yetu hapa nimechezewa faulo."

Kuhusu kiwanda hicho kufungiwa na serikali ili kupisha uchunguzi, alisema bado hajapata taarifa bali amepewa barua na TFDA kujieleza ndani ya siku 14 kwanini asifungiwe.

Akizungumzia wagonjwa wanaotumia dawa hizo kuandamana alisema kuwa wana haki ya kufanya hivyo kwani wanatetea uhai wao.

Kiwanda cha TPI, ni kiwanda kikubwa cha dawa kwa ukanda wa Afrika Mashariki kilichokuwa kizinduliwe Novemba mwaka huu kikiwa kimewezeshwa euro milioni 5 na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Source: Tanzania Daima
 
Hiyo tume inayoundwa inatokana na akina nani? wanatumia njia gani kugundua uhalifu huo kama ulifanywa? napendekeza utaalamu wa forensic technology utumike kwa vile huo unga dawa fake umepita kwenye mitambo hiyo siku nyingi. Kwanza kabisa hicho kiwanda kifungwe mara moja na uchunguzi huo ufanywe na chombo huru kutoka nje ya nchi.
 
Inakuwa kama issue ya Mwangosi kila mtu anaunda tume yake. Ina maana taasisi zilizowekwa kisheria zimeshindwa kazi au haziaminiki?
 
TPI pekee ndiye sole supplier wa dawa hizo MSD,pia hizo dawa feki na halisi makopo 12000 yote ni batch moja.Hana la kutudanganya watanzania huyu kada wa ccm,ilitakiwa maelezo haya atoe mahakamani
 
TPI pekee ndiye sole supplier wa dawa hizo MSD,pia hizo dawa feki na halisi makopo 12000 yote ni batch moja.Hana la kutudanganya watanzania huyu kada wa ccm,ilitakiwa maelezo haya atoe mahakamani
Huyo kada wa CCM hawezi kukamatwa kwasababu yeye anatumiwa tuu na mwenyekiti wa chama chake
 
Tuhuma ni kwamba hizo ARV fake zinaletwa kutoka India na kufanyiwa packaging hapo. Hilo wafanyakazi wa TPI na watu wengine wanaweza kuthibitisha iwapo uchunguzi utafanywa kwa makini. Tatizo linakuja ni kwamba:

1. Serikali ina share asilimia 40 katika TPI

2. Akina Madabida ni wachangiaji wakubwa sana wa CCM

Hili suala nalifananisha na kiwanda kingine kinachotengeneza vyandarua vyenye dawa za mbu, vyandarua ambavyo siku hizi ni fake kabisa havijamaliza kabisa malaria. kiwanda hicho cha Wahindi huchangia mabilioni kwa CCM.

Tatizo wavunja sheria nchii hii ndio wafadhili wa CCM,hivyo ni muda wao sasa kurudisha hasara walizotumia.
 
Tuhuma ni kwamba hizo ARV fake zinaletwa kutoka India na kufanyiwa packaging hapo. Hilo wafanyakazi wa TPI na watu wengine wanaweza kuthibitisha iwapo uchunguzi utafanywa kwa makini. Tatizo linakuja ni kwamba:

1. Serikali ina share asilimia 40 katika TPI

2. Akina Madabida ni wachangiaji wakubwa sana wa CCM

Hili suala nalifananisha na kiwanda kingine kinachotengeneza vyandarua vyenye dawa za mbu, vyandarua ambavyo siku hizi ni fake kabisa havijamaliza kabisa malaria. kiwanda hicho cha Wahindi huchangia mabilioni kwa CCM.

A to Z au TMTL mkuu? Hebu funguka banaa!
 
Back
Top Bottom