TPDC yaeleza ukweli wa gesi ya Ruvu

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema kiwango cha gesi kilichogunduliwa katika Kitalu cha Ruvu ni cha uhakika na kuwataka wananchi wasiwe na mashaka.

TPDC imesema kampuni ya Dodsal ya Uarabuni imegundua kiwango cha futi za ujazo trilioni 2.17 katika Mambambakofi-1 kimethibitishwa na kwamba hata TPDC wenyewe wamejiridhisha.

============================

SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA

TPDC_logo.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kutoa maelezo kuhusu taarifa iliyotolewa na gazeti la Matanzania, Toleo namba 8129 la Jumapili tarehe 20 Machi 2016 lenye kichwa cha habari “Gesi ya Ruvu shakani”.

Taarifa hiyo ilikuwa na lengo la kupinga kile kilichoelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kuwa ujazo wa gesi iliyogunduliwa na Kampuni ya Dodsal ya Uarabuni wenye kukadiriwa kufikia trilioni 2.17 una mashaka.

TPDC inapenda ieleweke kwamba, Kampuni ya Dodsal iligundua gesi katika kisima cha Mambambakofi-1 kwenye kitalu cha Ruvu mwezi Aprili 2015. Taarifa za ugunduzi ziliwasilishwa baada ya kufanya yafuatayo:

1. Vipimo vya kuangalia uwezekano wa gesi au mafuta kwenye mashapo ambapo kisima kilichorongwa kitaalamu iitwayo “wireline logging”. Vipimo hivyo vilionyesha uwapo wa gesi na kwa kitaalamu inaitwa “cross over”

2. Kuchukuliwa kwa vipimo vya mgandamizo kulingana na urefu wa kisima “pressure vs depth” kwenye eneo lenye mashapo lililoonyesha uwepo wa gesi

3. Aidha zilichukuliwa sampuli za gesi katika mashapo hayo ili kubaini aina ya gesi iliyopo pamoja na tafiti zingine.

Baada ya kupitia vipimo hivyo vitatu, vikaonyesha uwapo wa gesi. Kampuni ya Dodsal ikaiarifu TPDC ambayo nayo ilipitia vipimo vya logging na pressure na kujiridhisha uwepo wa gesi asilia. Sheria inaitaka TPDC kama mwenye leseni kuiarifu Serikali kuhusu kufanyika kwa ugunduzi huo. Taarifa hiyo lazima iambatane na kiasi cha awali kinachobashiri ujazo wa gesi ambao ulikuwa ni futi za ujazo bilioni 160 (0.16TCF).

Sheria hiyo pia inamruhusu mkandarasi kuendelea kufanya uchambuzi zaidi wa kina kutumia taarifa za kisima kilichochimbwa. Kwa kufanya hivyo, Dodsal wameleta taarifa ya ongezeko la ujazo wa gesi katika eneo tajwa kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.01. Hivyo basi, kwa ujumla wake Dodsal wameleta makadiria ya ujazo wa gesi wenye ukubwa wa trilioni 2.17.

Mkandarasi atahitajika kufanya Drill Stem Test wakati atakapoleta mpango kazi wa kuhakiki ujazo wa gesi na uwezo wa mashapo kuzalisha “appraisal program”.

Mnamo Machi 2016, Serikali imetimiza matakwa ya kisheria ya kitalu cha Ruvu kuwa na “Location” na Kampuni ya Dodsal inajiandaa kuleta mpango kazi kama inavyoelekeza sheria mpya Petroleum Act 2015 kifungu namba 64 na 65.

Imetolewa na;
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Benjamin W. Mkapa Pensions Towers, Tower “A”,
Azikiwe/Jamhuri Street
P.O. Box 2774,
Tel. +255 22 2200103/4
Dar Es Salaam, Tanzania
Website: www.tpdc-tz.com
 
View attachment 331406

Haya aliyeanzisha ligi hiyo aingie uwanjani awajibu wasomi hao
 
Hizi gesi zinatakiwa zitumike na kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi, kusema imegunduliwa ipo haimsaidii kitu mwananchi kama mimi, maana hata madini yaligunduliwa na yapo lakini mwananchi wa kawaida hayamsaidii kitu, kutumia dhahabu ni jambo la ajabu kwa mwananchi wa kawaida kama haipatikani nchi hii.
 
Hoja sio ipo, kumbuka hapo hiyo taarifa imekuja baada ya watu kuanza kusema hata uwepo wake ni wa mashaka. Me nafikiri tujadili kwanza weledi wa waandiishi wetu wa habari hapa nchini manake tangu wasifiwe wanaandika chochote kinachopita mbele yao. wataalamu wamesema ipo, anaibuka mtu hana hata data anasema ana wasiwasi na uwepo. Tutafika mahali tutashindwa kuamini vyombo vya habari kabisa.
 
Hizi gesi zinatakiwa zitumike na kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi, kusema imegunduliwa ipo haimsaidii kitu mwananchi kama mimi, maana hata madini yaligunduliwa na yapo lakini mwananchi wa kawaida hayamsaidii kitu, kutumia dhahabu ni jambo la ajabu kwa mwananchi wa kawaida kama haipatikani nchi hii.
Unasema haunufaiki wakati hamna chochote unachofanya ili unufaike, wananufaik wengi tuu, au unataka uletewe dhahabu mpaka mlangoni kwako?
 
Kama Watanzania hawatamiliki asilimia kubwa katika uvunaji wa rasilimali hizi za Tanzania,basi uwepo wake hautaleta manufaa makubwa kwa Watanzania wenyewe.Dubai,Qatar,Saudia hazikujengwa na Total,Shell wala kampuni yoyote nje ya Dubai,Qatar au Saudi.Tusipigane vita kwenye umiliki wa Raslimali hizi.Big up Tanzania kwa kuendelea kuwa na hazina kubwa ya nishati ya gesi...kazi kwetu kuitumia kwa manufaa yetu zaidi.
 
Mabomba ya hii gesi yaelekezwe wapi? Au itachakatwa Arusha? Utasikia kituko katika hayo.
 
hii gas muhongo alisema itaiingizia serikali sh.12trillions,.....kitu cha uongo kabisa muongo kadanganya taifa,.....
kwa wataalamu wa calculations zake ilibidi iingizie nchi 35trillions,.....
naona kuna upigaji deal wa muhongo.....watoe elimu ya calculations za hiyo gas ili wananchi tujue nchi itaingizaq kias gan kwa tr 12.7 of gas,......
kuna calculations zipo serikali itoe elimu kwa raia waelewe tunafaidika nayo vipi na fedha zitazopatikana ktoka hii gas zionekane zitavyotumika
kuepuka upigaji wa wahuni waliozoea kupiga...........
+MBUGA+MADINI+GAS YA MTWARA+MLIMA klm wa1 afrika+OLDUVAI GOERGE+BAHARI(BANDARI) YA DAR+BANDARI YA TANGA+BANDARI YA MTWARA+MBUGA NK,......lakini raia wanaotumia umeme nchi nzima ni 11% kati ya watu 40millions............deni la taifa trillion 48,...hii nchi ya ajabu sana,...
tunaweza kuendesha nchi tukitegemea bandari2 bila kutegemea bajeti ya mikopo toka kwa wahisani,......na tungeizidi hata afrika ya kusini kwa maendeleo
ila viongoz wetu wameweka siasa mbele kuliko nchi,.....
tubadilike
 
Wanagundua gesi tu, gundueni na mafuta ndiyo tutajua nyie ni wajanja mbona wenzenu Kenya, Uganda na msumbiji wanagundua mafuta
nchi hata haina vifaha ya kugundulia kaka......
wakati gas iliyopo inatosha kununua vifaa tukagundua wenyewe tukazalisha wenyewe watu wakaja kununa2 kwetu na kupata faida maradufu......
 
hii gas muhongo alisema itaiingizia serikali sh.12trillions,.....kitu cha uongo kabisa muongo kadanganya taifa,.....
kwa wataalamu wa calculations zake ilibidi iingizie nchi 35trillions,.....
naona kuna upigaji deal wa muhongo.....watoe elimu ya calculations za hiyo gas ili wananchi tujue nchi itaingizaq kias gan kwa tr 12.7 of gas,......
kuna calculations zipo serikali itoe elimu kwa raia waelewe tunafaidika nayo vipi na fedha zitazopatikana ktoka hii gas zionekane zitavyotumika
kuepuka upigaji wa wahuni waliozoea kupiga...........
+MBUGA+MADINI+GAS YA MTWARA+MLIMA klm wa1 afrika+OLDUVAI GOERGE+BAHARI(BANDARI) YA DAR+BANDARI YA TANGA+BANDARI YA MTWARA+MBUGA NK,......lakini raia wanaotumia umeme nchi nzima ni 11% kati ya watu 40millions............deni la taifa trillion 48,...hii nchi ya ajabu sana,...
tunaweza kuendesha nchi tukitegemea bandari2 bila kutegemea bajeti ya mikopo toka kwa wahisani,......na tungeizidi hata afrika ya kusini kwa maendeleo
ila viongoz wetu wameweka siasa mbele kuliko nchi,.....
tubadilike
Ngoja aje
 
Hizi gesi zinatakiwa zitumike na kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi, kusema imegunduliwa ipo haimsaidii kitu mwananchi kama mimi, maana hata madini yaligunduliwa na yapo lakini mwananchi wa kawaida hayamsaidii kitu, kutumia dhahabu ni jambo la ajabu kwa mwananchi wa kawaida kama haipatikani nchi hii.
Tatizo ni kwamba mwenye gas ni yule aliyeichimba na sisi tunaambulia kodi kiduchu maana jamaa huwa wanadanganya kuhusu mapato halisi! Udanganyifu unaanzia kwenye utafiti. Watafiti wanadanganya gharama walizotumia kwenye utafiti. Wanataja gharama maradufu na kuwa inabidi warudishe kwanza gharama zao kabla ya kuanza kulipa kodi!
 
Mkuu ndio sababu nimesema imsaidie mtu wa kawaida, hata kama imepatikana nyingi kiasi gani bila kusaidia mtu mmoja, haina faida kwetu.
 
kulikuwa na sababu gani ya kujenga bomba kutoka mtwara hadi dar kumbe nyingine iko ruvu tu hapa!
Hapo ndipo utakapogundua kwamba tulikurupuka na tukafanya kasi ya ajabu ya ujenzi wa Bomba la Gesi ili itakapogundulika hapo Ruvu mradi wa ujenzi utakuwa umekamilika. Ukichunguza hayo matukio yamepangwa kisanii sana.
 
Back
Top Bottom