TPDC Oral vipi?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
31,187
Reaction score
88,941
Wakuu, kuna watu waliitwa interview TPDC baada ya kupita katika ile mitihani. Vipi mbona hakuna feedback? Mbona hatuambiani Oral ipoje ili na sisi tujiandae?

Kama tulivyowekeana matangazo, tukawekeana majina ya walioitwa written, kisha waliopita kwenda kwenye Oral, basi tufahamishane imekuaje huko? Pannel watu wangapi? Maswali yapoje yapoje?

Shukrani.
 
kaka hapo umesema maana watu ni wengi wanaendelea kusubiri hiyo interview na ikitokea utafahamu mazingira ya interview na panel ilivyokuwa inakuongezea confidence,TUAMBIZANE WADAU
 
Kuhusu pannel kuna mtu zaid ya 16 na zaid ya 10 wanapata chance ya kuuliza maswali. Maswali yanabadilika kulingana na position, mfano maswali ya watu wa research officer (chemical & process engineer) yalikua tofauti kabisa na watu wa research officer (mechanical engineer). Kitu kingine ni kwamba muda wa interview kwa kila candidate ni mfupi mno yaan ni chin ya dk 10, so ina bidi kubuild confo toka unapoanza interview. Pia hakuna yale maswali ya general tuliyoyazoea, km why the company should hire you, maswali yote ni technical kulingana position uliyoomba. All in all confo ni muhimu sana maana jamaa wapo na maswali waliyoyaandaa, so almost all questions are technical ones. Tea, lunch na maji wanatoa, so guys worry not about those stuffs. God bless ya people.
 

umesaidia sana mkuu. shukrani za pekee kwako.
 
Kitu kingine iwapo unataka ufanye intervirw na kuondoka mapema basi inabid kuwahi na uwe wa mwanzo kujiandikisha, maana majina wanaita kulingana na muda uliyofika sehemu ya intervw.
 
tunashukuru sana wadau wetu na hii ndo maana halisi ya Forum kwa kweli,stay blessed waungwana!
 
kaka boro hujapata fununu za mshahara kwa scale ya TPDC PS1 ni shilingi ngapi maana wanaweza kuwataka watu watu wanegotiate katika hilo
 
Broda Gambayi, kuhusu salary kwa scale TPDC PS 1 kwa kweli sijui, ila kama TPDC PS1 itakuwa sawa na TPDC RS1 salary itaanzia na 1.6M. Hii nina uhakika maana nipo jamaa yangu pale yeye ni engineer ndo aliniambia hivyo. Mie nishapiga intervw tayar na kama nilivyosema hapo mwanzo labda kama watabadili mode ya kuuliza maswali yaan wale jamaa hawana muda kabisa wa kunegotiate salary ni maswali tu. Kwa kuwa muda wa intervw ni kidogo confo toka mwanzo ni muhimu pia CNN iwe imetulia hope ukifanya hivyo ndani ya hizo dk kumi or so utakua umejibu kitu fulan cha kukupa matumain.
 
means kwa muda huo mchache hawataki chenga ni kuwaambia vitu straight tu kwa kweli maana ukileta mbwembwe ndo bhasi tena kaka,shukrani sana kaka ngoja nasi twende mkuu tukapige hiyo kitu
 
ni team wazee,vijana au mixer kwenye panel maana wazee nao ni noma sana kwa kweli kaka Borro
 
Pannel ni watu 12 wanajigawa upande mmoja sita mwingine sita we unawekwa mtu kati kama unapigwa lecture hivi.

Muhimu jiandae sana na maswali ya proffesional yako pia jiandae sana na maswali general ya kijamii ambayo ni too technical hakikisha inakuwa updated na mambo ya kidunia.
 
Hivi mkuu kama ule mtihani wao umefaulu ila bado hawajakupigia simu si unaweza ukkaibuka hiyo siku ya interview?
 
Hivi mkuu kama ule mtihani wao umefaulu ila bado hawajakupigia simu si unaweza ukkaibuka hiyo siku ya interview?

As long as jina lako lime appear kwenye rangi ya kijani kwenye yale matokeo ya written nenda tu, may be walikupigia network ikasumbua ukawa not reachable or muda bado utapigiwa simu.
 
Kuhusu kupigiwa cm, hawajapiga cm hata kama itakua kwa watu wachache sana. Kama ulifaulu written yakupasa uende ukapige oral. Venue ipo ndani ya tpdc kota mikocheni mbele ya rose garden
 
Intaview za tpdc huwa hawaulizi maswali ya mishahara au general questions. Wejipange maswali huwa yanabase kwenye ur professional in deep. Mungu atutangulie.

Tpdc ni akili yako tu hakuna kingine zaidi ya hapo wakuu
 
Mashirika yote ya umma inabidi yaige mfumo wa Tpdc katika ajira
 
kwa kuwasaidia wale mara ya kwanza interview..

-vipi, mbali na vyeti original, unaenda na CV au wanayo ile ile ulio tumia ku-apply.?

-wanazisoma zile CV/veti pale pale, au wanapiga copy watavisoma baadae?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…