TAKUKURU yakumbwa na kashfa ya rushwa katika utoaji ajira

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
TAKUKURU walitangaza ajira nafasi mbalimbali ikiwemo nafasi za "WACHUNGUZI WASAIDIZI" .Hatua ya kwanza watu waliomba wakajaza taarifa kwenye mfumo na kuambatanisha nyaraka zote zilizohitajika.

Hatua ya pili kuna walioitwa kwenda kwenye usahili wa maandishi (Written Interview), Orodha ya majina ilitoka wakaitwa huko Dodoma chuo cha Mipango na Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) tar 08/Januari 2022.

Hatua ya tatu ,waliopita hatua ya pili ya Usahili wa maandishi (Written Interview) waliitwa kwenye hatua ya tatu ya Usahili wa kuongea (Oral Interview) ambao ulifanyika Kuanzia tar 1 Machi hadi tar 18 Machi 2022 huko Dodoma (Nane nane ). Na Orodha ya walioitwa kwenye Oral Interview iliwekwa wazi .

Sasa kuna changamoto mbili ambazo zinaleta ukakasi sana katika huu mchakato wa ajira ,ambapo TAKUKURU wanapaswa kutoa ufafanuzi wa kutosha sababu kuna viashiria vya Rushwa hasa Upendeleo (Nepotism) , mjuano au hongo ili kuwapa watu nafasi ya ajira jambo ambalo linatengeneza taswira mbaya kwa TAKUKURU.

1. Kuna documents mbili zenye orodha ya majina ya watu walioitwa kwenye Usahili wa maandishi (Written Interview) na Usahili wa kuongea (Oral Interview) , Usahili wa maandishi ndio ulianza baadaye ukafuata usahili wa kuongea (Oral Interview) . Jambo la kushangaza kuna majina ambayo katika orodha ya usahili wa maandishi ulioanza hayakuwepo ila usahili uliofuata wa Oral Interview yapo. Yametokea wapi majina hayo?.

Mfano ,Jina la "Sadick Msabaha Komba " hili jina ni miongoni mwa majina ambayo katika hatua ya awali ya Written Interview halikuwepo katika orodha ya walioitwa ila katika hatua iliyofuata ya walioitwa Oral Interview ambayo ni hatua ya pili baada ya hatua ya Written Interview lilikuwepo.

2. Changamoto nyingine, baada ya Oral Interview , hakuna orodha ya majina ya watu waliopita katika Oral Interview zaidi kuna hiyo taarifa ya TAKUKURU waliyoitoa "Tangazo la kuitwa kwenye Mafunzo ya awali ya Uchunguzi". Wakisema waliopita Oral Interview watatumiwa taarifa kwa njia ya Emails.

Kwanini orodha isiwe wazi ? .Zinatolewa sababu eti ni siri hawapaswi kujulikana kwa sababu wanaenda kuwa ma afisa wa TAKUKURU sio kweli ni njia ya kupachika watu wao.

Kwanini mtu aliingizwa hatua ya Oral Interview ikiwa hakuwepo hatua ya Written Interview,? .

kwa logical Argument ya Syllogism , kupitia Proposition, inferences na conclusion ni wazi mchakato uliharibiwa ,kwani kuna viashiria vyote watu wengi waliotumiwa emails sio waliopita hatua ya Oral Interview .

Ndio maana hata majina ya waliopita katika Oral Interview hayajawekwa wazi. Hoja ya kusema hao watu ni siri hawapaswi kujulikana sababu ya majukumu yao ya kichunguzi ni hoja nyepesi inayotumiwa kuchomeka watu wao.

Uwazi ni jambo muhimu sana katika kupambana na Rushwa na TAKUKURU ilipaswa kuonesha uwazi katika mchakato wote wa utolewaji ajira .Watu wengi wanalalamika kwamba kulikuwa na mambo yasio fuata taratibu (Irregularities) katika mchakato wa usahili wa kazi .

Wengi waliokwenda kwenye hatua ya Oral Interview hawajapata hizo emails na hata marafiki zao walioshiriki pia hawajapata hizo emails, Swali hizo emails za kuitwa kwenye Mafunzo ya awali ya Uchunguzi ametumiwa nani ?.

Kuna haja suala hili mamlaka wakaliangalia kwani linaacha dosari kwa taasisi nyeti ya kupinga rushwa na yenyewe kuhusishwa na Rushwa .

Abdul Nondo .
IMG_20220411_164432_468.jpg
IMG_20220411_164432_487.jpg
IMG_20220411_164432_420.jpg
 
Hilo ni moja, kuna interview flani tulifanya pale Dodoma, ni hayo hayo tuu yalitokea, yaan tumetoka kwenye oral tukaambiwa majibu baada ya siku mbili,

Tulikaa mwezi mzima ndio wanatoa majibu,

Ambao hawakuwepo kwenye list ya oral wakaitwa kazini, ni kawaida tushazoea ila yana mwisho, sisi ambao wazazi wetu ni wakulima au Fundi mchundo hizi ajira rasmi tutasikia tuu,

Nipo mtaani na maisha yanasonga
 
hili nilitegemea kusikia toka kwa wadau hasa baada ya tangazo lao la mwisho lenye maswali mengi... wekeni majina watu waone kama kuna janja janja...
 
Hii nchi hadi wale wanaotakiwa kupambana na rushwa nao wanaitafuna rushwa, hapo sababu inaweza isiwe kujuana pekee, hata rushwa za aina tofauti zinaweza kuwa sababu ya kupachika majina yasiyokuwepo mwanzo.
 
Hilo ni moja, kuna interview flani tulifanya pale Dodoma, ni hayo hayo tuu yalitokea, yaan tumetoka kwenye oral tukaambiwa majibu baada ya siku mbili,
Tulikaa mwezi mzima ndio wanatoa majibu,
Ambao hawakuwepo kwenye list ya oral wakaitwa kazini, ni kawaida tushazoea ila yana mwisho, sisi ambao wazazi wetu ni wakulima au Fundi mchundo hizi ajira rasmi tutasikia tuu,
Nipo mtaani na maisha yanasonga
Duuuh ☹☹
 
Hii ni mbaya sanasana kwa taifa.
 
Kuna uhuni na utapeli mkubwa unaratibiwa na Utumishi kwenye suala zima la ajira nchini. Malengo ya uundaji wa chombo hiki yanapotea, tuombe Mungu tushuhudie yajayo

Kuna haja pia UTUMISHI ichunguzwe. Malalamiko juu ya utumishi ni mengi sana ... hata hizo taasisi zinazopelekewa hao wafanyakazi zimekuwa zikilalamika kuwa watumishi wanaopelekwa wengi ni hawana uwezo kama ilivyokusudiwa. Utumishi inaanza kupoteza sifa taratibu na suala la kupenyeza vimemo limeshindwa kuzuilika pale utumishi. Njia pekee ya kuondoa haya mambo ni katiba mpya. Kwakuwa vijana mmekuwa wagumu kuiondoa ccm , endeleeni kula machungu ya nchi. Mama anaupiga mwingi
Kazi iendelee,
 
Jamaa alikamatwa na Afisa takukuru akitoa rushwa ili makontena yake yapite. Afisa takukuru nae akamwambia mfanyabiashara ampe hela kidogo ili asimchomee kuwa alikuwa akitoa rushwa. Ndio mjue Aliyeiroga tanzania alishakufa mbaya zaidi aliondoka na tunguli zote. Hata Mama anapoteza poteza muda na Blah Blah za kiunguja Kisha aje mwingine ....
 
TAKUKURU walitangaza ajira nafasi mbalimbali ikiwemo nafasi za "WACHUNGUZI WASAIDIZI" .Hatua ya kwanza watu waliomba wakajaza taarifa kwenye mfumo na kuambatanisha nyaraka zote zilizohitajika.

Hatua ya pili kuna walioitwa kwenda kwenye usahili wa maandishi (Written Interview),Orodha ya majina ilitoka wakaitwa huko Dodoma chuo cha Mipango na chuo cha UDOM tar 08/Januari 2022.

Hatua ya tatu ,waliopita hatua ya pili ya Usahili wa maandishi (Written Interview) waliitwa kwenye hatua ya tatu ya Usahili wa kuongea (Oral Interview) ambao ulifanyika Kuanzia tar 1 Machi hadi tar 18 Machi 2022 huko Dodoma (Nane nane ). Na Orodha ya walioitwa kwenye Oral Interview iliwekwa wazi .

Sasa kuna changamoto mbili ambazo zinaleta ukakasi sana katika huu mchakato wa ajira ,ambapo TAKUKURU wanapaswa kutoa ufafanuzi wa kutosha sababu kuna viashiria vya Rushwa hasa Upendeleo (Nepotism) ,mjuano au hongo ili kuwapa watu nafasi ya ajira jambo ambalo linatengeneza taswira mbaya kwa TAKUKURU.

1.Kuna documents mbili zenye orodha ya majina ya watu walioitwa kwenye Usahili wa maandishi (Written Interview) na Usahili wa kuongea (Oral Interview) , Usahili wa maandishi ndio ulianza baadaye ukafuata usahili wa kuongea (Oral Interview) . Jambo la kushangaza kuna majina ambayo katika orodha ya usahili wa maandishi ulioanza hayakuwepo ila usahili uliofuata wa Oral Interview yapo.Yametokea wapi majina hayo?.

Mfano ,Jina la "Sadick Msabaha Komba " hili jina ni miongoni mwa majina ambayo katika hatua ya awali ya Written Interview halikuwepo katika orodha ya walioitwa ila katika hatua iliyofuata ya walioitwa Oral Interview ambayo ni hatua ya pili baada ya hatua ya Written Interview lilikuwepo.

2.Changamoto nyingine, baada ya Oral Interview , hakuna orodha ya majina ya watu waliopita katika Oral Interview zaidi kuna hiyo taarifa ya TAKUKURU waliyoitoa "Tangazo la kuitwa kwenye Mafunzo ya awali ya Uchunguzi". Wakisema waliopita Oral Interview watatumiwa taarifa kwa njia ya Emails.

Kwanini orodha isiwe wazi ? .Zinatolewa sababu eti ni siri hawapaswi kujulikana kwa sababu wanaenda kuwa ma afisa wa TAKUKURU sio kweli ni njia ya kupachika watu wao.

Kwanini mtu aliingizwa hatua ya Oral Interview ikiwa hakuwepo hatua ya Written Interview,? .

kwa logical Argument ya Syllogism , kupitia Proposition, inferences na conclusion ni wazi mchakato uliharibiwa ,kwani kuna viashiria vyote watu wengi waliotumiwa emails sio waliopita hatua ya Oral Interview .

Ndio maana hata majina ya waliopita katika Oral Interview hayajawekwa wazi.Hoja ya kusema hao watu ni siri hawapaswi kujulikana sababu ya majukumu yao ya kichunguzi ni hoja nyepesi inayotumiwa kuchomeka watu wao .

Uwazi ni jambo muhimu sana katika kupambana na Rushwa na TAKUKURU ilipaswa kuonesha uwazi katika mchakato wote wa utolewaji ajira .Watu wengi wanalalamika kwamba kulikuwa na mambo yasio fuata taratibu (Irregularities) katika mchakato wa usahili wa kazi .

Wengi waliokwenda kwenye hatua ya Oral Interview hawajapata hizo emails na hata marafiki zao walioshiriki pia hawajapata hizo emails,Swali hizo emails za kuitwa kwenye Mafunzo ya awali ya Uchunguzi ametumiwa nani ?.

Kuna haja suala hili mamlaka wakaliangalia kwani linaacha dosari kwa taasisi nyeti ya kupinga rushwa na yenyewe kuhusishwa na Rushwa .

Abdul Nondo .View attachment 2184085View attachment 2184086View attachment 2184089
Recruitment process zilizopita walifanyeje? Je, wana kanuni za recruitment?
 
Back
Top Bottom