Kinachoitwa wizi wa ORYX Infact sio wizi. Ni ujanja tu wa ORYX kwenye mkataba wao.
Waliingia mkataba kwamba serikali ni 50% na Oryx ni 50% lakini oryx wanaendesha shughuli za kila siku za kampuni.
Ujanja wanao fanya oryx ni kutunza mafuta yao mengi Tiper na kwa storage fee ndogo kuliko kampuni nyingine yoyote (faida namba moja, hapa oryx ina nufaika, serikali imelala).
Faida nyingine ni Oryx ndio wateja namba moja wa MI losses za Tiper. MI loss ni kitu ambacho naweza kielezea hivi.
Unapeleka mafuta yako Tiper, tuseme lita 20,000 lakini mkataba kati yako na Tiper unasema mafuta sio mawe,yapo yatakayo potea kwa evaporation, yapo tayakayo potea kwa leakages etc. Hiyo ni 0.02 ya mafuta yako. So kwenye lita elf 20, kuna lita 400 hautapewa siku ukitaka mafuta yako. Sasa Piga hesabu ukileta milioni 2 kula lita elf40 hautapewa etc.
Baada ya muda Tiper inakua na accumulation ya mafuta ya namna hiyo. Inawezekana ikifika tani 1000 dizeli, 500 pms, 300 jet nk.
Hizi wao wanaziita MI loss (gains) ambazo mwingi wa siku zitauzwa na zita lipiwa kodi (ingawa mwanzoni walikua wanakwepa hadi masamaki alivo wakomalia).
Sasa oryx inafaidi kwenye uuzaji huu. Maana yanauzwa kwa bei ndogo na mnunuaji wa karibu na wa haraka ni Oryx. (hapa ndipo TPA walipo chukua Ile idea kwamba Tiper inaiba mafuta na kumuuzia oryx).
So kwenye Hilo la pili pia serikali kama 50% share holder hanufaiki, zaidi ata subiria DIVIDEND mwisho wa mwaka na hii inakua maybe 1billion na serikali ikipewa in CHEKELEA kweli kweli.
Kampuni inaweza tengeneza more than 20billion kwa mwaka, lakini matumizi ni ya kijinga na yasiyo ya kuipeleka mbele kampuni. Matumizi ni kuajiri wazungu kufanya kazi wanazo weza kufanya watanzania. Kwa mfano yupo anae simamia stocks, yeye analipwa dola 23,000 kwa mwezi. Pesa ambazo zinaweza kulipa wazawa zaidi ya 20 waliopo kwenye kitengo hicho hicho.
Haya tuliyasema toka zamani, atleast Muhongo alianza fuatilia kabla hajang'atuka.
Kuna watu humu ndani ni mashahidi wangu, nili wasimulia 2012 jinsi tunavoliwa watanzania na jitihada zote zinagonga mwamba.
Hawa wadosi wa ORYX sio watu wadogo, walikua wamekamata hadi ikulu.