Upotevu wa Mafuta bandarini: Mtendaji Mkuu WMA, Meneja Vipimo wasimamishwa kupisha uchunguzi

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
SERIKALI imeamua kuwasimamisha kazi watendaji wawili kutoka Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kufunga kwa mita kwa zaidi ya miaka mitano.

Waliosimamishwa kazi ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa na Meneja Vipimo Kitengo cha Bandari, Bi. Bernadina Mwijarubi. Bi. Mwijarubi ndiye anashughulikia kitengo cha mafuta bandarini.

Akitangaza uamuzi huo kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika leo (Ijumaa, Februari 12, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Adelhelm Meru awaandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi huo.

“Katibu Mkuu Viwanda, waandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi. Katika kipindi hiki hawatatakiwa kusafiri kwenda popote hadi uchunguzi utakapokamilika. Pia utafute mtu wa kukaimu nafasi hiyo ili kazi ziendelee,” alisema.

Waziri Mkuu pia amesema ofisi yake itawaandikia barua ofisi ya TAKUKURU na polisi ili wafuatilie suala hilo mara moja na ikithibitika kuwa walihusika hatua rasmi zitachukuliwa na itathibitika hawakuhusika basi watarudishwa.

Waziri Mkuu pia aliagiza mfumo wa upimaji mafuta kwa kutumia flow meters uendelee kutumika na ule upimaji wa kukadiria uache kutumiwa mara moja.

Jana (Alhamisi, Februari 11, 2016) Waziri Mkuu alifanya ziara kukagua flow meters za zamani zilizopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty) na kisha akatembelea na kukagua flow meters mpya ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni 6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).

Pia Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na kampuni ya Oryx Energies.

Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.

“Jana niliagiza kuwa bomba hilo ling’olewe. Nimetoa mwezi mmoja ili kurekebisha mfumo huo. Simamieni vizuri na kuhakikisha kuwa na wao pia wanarudi kwenye manfold kama ilivyo kwa wengine,” alisema Waziri Mkuu.


IMETOLEWA NA:


OFISI YA WAZIRI MKUU,

MTAA WA MAGOGONI,

S. L. P. 3021,

DAR ES SALAAM.

Hili jibu limetoka ofisi ya Profesa Muhongo. Naomba mlibandike hapo juu kama. Sehemu ya ufafanuzi kwa wanaomhusisha waziri huyo na saga hili la flow meters.....

Nawasilisha kama nilivyolipokea:

Flow meters za kupima mafuta ziameachwa kutumiwa Mwaka 2011. Prof Muhongo hakuwapo nchini wala Serikalini mwaka 2011.

Wenye dhamana ya kusimamia mita hizo ni Wizara ya Viwanda na Biashara na siyo Wizara ya Nishati na Madini.

Huyo mama na wenzake (Weights & Measures) wako chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Mwenye jina la Mwijarubi hana undugu na Prof. Muhongo, Mwijarubi ni jina la kawaida sehemu za Ukerewe na Musoma Vijijini.

Tusidanganywe.
 
Hawa wadogo wanaonewa tu.Kwanini Mawaziri wenye dhamana hawaguswi??Hivi Muhongo hakuliona hilo???Naona kuna shida mahali fulani..............

Mkuu, kwani Muhongo alikuwepo bandarini kwa miaka yote 5 wakati hujuma zinafanyika?

Labda useme Mwakyembe ambae alianza kushughulikia hili la mabomba na sifahamu aliishia wapi.
 
Inamaana hizo Machine zilinunuliwa za nini kama hazitumiki??? Huo ni ufisadi wa makusudi kabisa. Wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi wahusika wote.
 
Hawa wadogo wanaonewa tu.Kwanini Mawaziri wenye dhamana hawaguswi??Hivi Muhongo hakuliona hilo???Naona kuna shida mahali fulani..............
Kwa hiyo una maana ni makosa kuwasimamisha kazi wakati uchunguzi unaendelea?
 
Mwijarubi???? huyu ana uhusiano na prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo?
0088_fcbb.jpg
 
Muhongo anahusikaje hapo!!??? Wewe unajua Wakala wa Vipimo Nchini iko chini ya Wizara gani!!??? Au unakurupuka tu, naona MUHONGO amewakalia pabaya sana.

Hujui kwamba ndiyo Waziri wa Nishati na ndiye aliyetuma SMS kulingana na muulizwa swali??ALikuwa pia Waziri wa NISHATI awamu iliyopita au tunakosea
 
wewe utakuwa chizi kwani muhongo lini aliwahi kuwa waziri wa uchukuzi watu wengine sijui mnagenye za aina gani.

Pole hapo wameongelea MAFUTA na SMS.Umeisikiliza hiyo Clip??Muhongo si ndiyo mtumaji wa SMS na Waziri wa Petrol na diesel au??
 
Back
Top Bottom