TPA, TRA, TICTS 'wakamatana uchawi' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TPA, TRA, TICTS 'wakamatana uchawi'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jun 2, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,265
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  TPA, TRA, TICTS 'wakamatana uchawi' [​IMG] [​IMG] [​IMG] Thursday, 28 May 2009 16:30 Na Edmund Mihale

  MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA),Kampuni ya Kupakua Mizigo Bandarini (TICTS) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameanza 'kukamatana uchawi'kuhusu chanzo cha ucheleweshaji utoaji mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.

  Bandari hiyo imekuwa ikilalamikiwa mara kwa mara kwa kushindwa kutoa mizigo kwa wakati na kusababisha nchi zilizokuwa zikiitumia zikiwemo Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na Rwanda kupitisha mizigo yao Bandari ya Mombasa, Kenya.

  Wakati TRA ikitarajia kuwakilisha ripoti yake leo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Fedha na Uchumi ya Bunge, jana TPA ilirusha lawama kwa TRA na TICTS kuwa ndio chanzo cha ucheleweshaji mizigo bandarini hapo.

  Hayo yalijitokeza wakati TPA ikiwakilisha ripoti ya utendaji wake kwa kamati hiyo ya Bunge katika ukumbi wa Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam.


  Mjumbe wa Kamati hiyo, Bw. Richard Ndasa ambaye ni Mbunge wa Sumve, alishangaa Tanzania kuwa masikini wakati imebarikiwa kuwa na bandari inayokubalika kutumika na nchi jirani kutokana na hali ya kijiografia lakini imeshindwa kufaidika nayo.

  "Tunalalamika eti hatuna fedha wakati fedha zipo na tunazikimbiza wenyewe, hili linanifanya nishangae, nafasi ambazo Mungu ametujalia tunashindwa kuizitumia tunasema hatuna fedha na hii bandari ya nini ? "Alihoji Bw. Ndasa.

  Alisema Bandari imebeba dhamana kubwa kuhakikisha uchumi wa Taifa unakuwa kutokana na kuhamasisha wateja wengi kusafirisha na kupokea mizigo yao sehemu mbalimbali kwa wamati.

  Bw. Ndasa alisema imefika wakati Bandari hiyo kujifunza kutoka Dubai ambayo imekuwa ikiitumia bandari yake kikamilifu na kukuza pato la Taifa hilo

  Alisema Bandari hiyo imekuwa ikipakua kontena 100 na kuondoa msongamano wa mizigo hivyo kukidhi mahitaji ya wateja wake.


  Alisema haoni sababu kwa Mamlaka hiyo kuendelea kuikumbatia TICTS kwa kuipa nafasi kuwa kampuni pekee ya kupakua mizigo bandarini hapo bila ushindani jambo linalochangia kushuka kwa ufanisi.

  Alisema imefika wakati wa mamalaka hiyo kujua kuwa dunia ya sasa ni ya ushindani na si ya kulindana wakati uchumi wa nchi unaendela kudidimia.

  Naye Mbunge wa Mvomero,Bw. Suleiman Sadiqq, alisema taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo ni nzuri kusoma lakini haiendani na hali halisi ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo kutoka na kulundikana mizigo bandarini hapo.

  Alisema taarifa zinazotolewa na mamlaka hiyo zimekuwa zikificha ukweli jambo ambolo limekuwa likiipa kamati hiyo wakati mgumu kushindwa kusaidia mamlaka hiyo inapobidi

  "Unajua kama taarifa hii ingekuwa na ukweli tungejua ni wapi tuwasaidiane hapa mnasema kuna mafanikio mimi sioni kama kuna mafanikio hayo mnayosema, ni mafanikio yametokana na msukumo kutoka ngazi za juu hatujaona nguvu yenu hapa!" alisema Bw. Sadiq.


  Alisema ushahidi wa kushindwa utendaji kazi kwa bandari unadhihirishwa na baadhi ya nchi kuamua kupitisha mizigo yao Mombasa, Kenya.


  Bw. Saddiq alisema kuzorota Sekta ya Bandari kumesababisha pia kuyumba sekta zingine kama usafirishaji, hoteli, nyumba za kulala wageni na ushuru mbalimbali unaotolewa katika barabara zetu, hali ambayo inachangia Taifa kukosa mapato.


  Awali akitoa taarifa hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bi Hapiness Senkoro, alisema katika kipindi cha 2007 na 2008 mamlaka hiyo iliendesha shughuli zake kwa ufanisi mkubwa zaidi ukilinganishwa na miaka ya nyuma.

  Alisema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine kama TRA TICTS, SUMATRA MoID, TASAA, TAFFA, TRL TATOA na ICDs, walipunguza msongamano mizingo katika bandari hiyo.

  Alisema idadi ya meli imendela kupungua siku hadi siku kutoka meli 23 hadi 8 kwa siku.


  Alisema wastani wa meli za kontena kusubiri nje ya bandari umepungua kwa wastani wa siku 1.7 ikilinganishwa na wastani wa siku 9 siku za nyuma .

  Akijibu hoja za wajumbe hao, Naibu Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo, Bw.Dustan Mrutu, alisema ucheleweshaji utoaji mizigo bandarini hapo unatokana na kushindwa kufanya kazi kwa wakati kwa TRA na TICTS

  Bw Mrutu alisema kuwa vitengo hivyo vina uwezo mdogo katika utendaji wake hali ambayo inasababisha malundikano wa mizigo katika bandari hiyo na kusema si TPA inayokwamisha mizigo hiyo.

  Alisema kumekuwa naurasimu wa kutisha sehemu ya 'long room' hali inayosababisha kero kubwa wateja wengi.

  Alisema sababu nyingine ni ubovu wa miundombinu nchini hususan ukosefu mabehewa katika reli ya kati na TAZARA jambo linalokwamisha wateja wengi kusafirisha mizigo yao.
   
 2. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yaani hapo loong room kuna rushwa hamna mfano. Ni kweli documents za kutoa mizigo huchelewa sana hapo, wakati mwingine hata kupotea kwa muda mpaka utoe chochote. Zingine hutoka ndani ya dakika chache tu kwa kutoa rushwa. Loog room pamulikwe. Hao jamaa wanaofanyakazi humo ni mamilionea huku wakihujumu uchumi wa nchi.
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Mie nishaachana nao hao tangu wangoe radio na vitu vingine kwenye gari yangu
  hivi bado kuna watu wanatumia hiyo bandari?

  by the way TPA wana mpango kambambe wa kutumia zaidi ya BILIONI 100 kujenga ghorofa na mambo mengneyo ili kuifanya bandari ya Dar ionekane kama DUBAI MARINA

  Yes, mpango upo architects washapewa tenda na speciment ya ghorofa tayari na litajengwa pale pembeni ya TRA ..pale kwenye petrol station ya CALTEX

  watu hawa hawa hawana hata CRANES na WINCHI kwa ajili ya kutolea mizigo

  says alot where their priorities lie

  JK ndio wanamdharau kama nini maana aliwapiga mwakara kuwa angerudi mwezi wa 4 sasa hivi ni mwezi wa SITA na meli zimejazana kule nje kama kawaida
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kwani ule mfumo wa asycan awaliouanzisha imekuwaje? si walisema kuwa huo unaondoa urasimu kwa sababu documents zinakuwa lodged electronicaly?
   
Loading...