Jerlamarel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 843
- 2,517
ππβ€π βπ»ππ βπππΈ βπΌππΌπΌ ππΈ ππβ€ππΉπΈ πΎπΈβπΌ ππΈ ππΈππ π½πββπΌ β€πΈ πβπ?
π½π ππππππ πΎππ πΌππππ.
Ukiniambia niishauri Serikali yangu kuhusu Tozo nitawashauri kwa haraka kama ifuatavyo.
Rais Samia Sio muumini wa task Force kama zile za Magufuli za kupambana na matajiri pamoja na wafamya Biashara kwenye kukusanya kodi. Rais Samia anaamini kuwa Wafanyabiashara pamoja na matajiri watalipa kodi yao vizuri na kwa kiwango ambacho ni halali na kwa wakati.
UKWELI
Ukweli ni kwamba kwa Afrika na hasa Tanzania hakuna mtu huwa anafanya kitu kwa hiyari yake bila kusukumwa tena jambo lenyewe liwe ni kuhusu kulipa kodi uipeleke serikalini kama inavyohiyajika sio rahisi kama tunavyofikiria. Kwa kulifahamu hilo Serikali iliyopita iliamua kutembea na wafanyabiashara kwa Task force kukusanya fedha.
Kwa mwafrika kukwepa kodi ni ufahari wakati kwa wenzetu ulaya ni aibu. Katika hali kama hiyo Serikali haiwezi kupata Mapato kwa kiwango inachokihitaji na matokeo yake lazima hizi Tozo ziwepo.
KINACHOTOKEA
Kutokana na Hali hiyo option pekee ambayo Mwigulu Nchemba anayo ni kutoza tozo mbalimbali. Matokeo yake kuna kundi linaumia zaidi. Mathalani kundi la wafanyakazi kwa mfano huyu unamkata PAYE, baadaye akinunua Kitu dukani analipa VAT, baadaye akituma pesa au kutoa anakatwa, sasa hivi ule mshahara ulioukata PAYE unaufuata tena Kule bank unaukata nk.
Unakuta Mfanyakazi huyu karibia Mshahara wote umerudi ulikotokea au umebaki kiduchu sana na hali yake inazidi kuwa mbaya.
Kwa mfanyabiashara yeye halipi PAYE.... hivi Dr. Mwigulu aliwahi kufikiria kama akiwawekea kina Mo, GSM, Baharesa PAYE atapata pesa shilingi ngapi? Hivi unajua kuna Mfanyabiashara anaingiza kwa mwaka Shilingi milioni 100 lakini analipa Kodi chini ya shilingi milioni moja? wakati Mfanyakazi anayelipwa mshahara wa mwaka milioni 10 analipa Kodi zaidi ya Milioni moja?
MATOKEO
Matokeo ya hizi tozo ni kwenye madhara ya kisiasa. Mahali pekee ambapo wananchi wataweza kukuhoji kwa vitendo na kukuonyesha kuwa hawakubaliani na wanayofanyiwa ni kwenye Sanduku la kura.
Juzi nilisema hapa kuwa Upinzani wa kina Mbowe upo kimya lakini hizi tozo zimechukua nafasi ya upinzani. TuIangalie na tusicheke na watu kwa lengo la kuwafurahisha. Duniani kote toka zama za Roma hawakucheka na watu kwenye masuala yanayohusu kodi. Bora wachache walie lakini wengi wakupende ambao ndio Voters.
Dr. Mwigulu hebu kakae na Makamu wa Rais mwambie huko kwenye Chungu akiwa waziri wa Fedha kulikuwaje? alikuwa anapata Fedha wapi? halafu muombe muende Kwa Rais ninyi wawili tu mjadiliane je hatuwezi kurudi kule tulikotoka kwenye Task Force? nawaambieni hawa wafanyabiashara hawawezi kulipa kodi kwa style tunayoitaka bado waafrika ni washenzi hivyo naamini kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi hapa nchini.
Mwisho tukubali ndani ya watanzania milioni 50 plus kuna watu wengine ambao hawapo kwenye mfumo ambao wana mawazo ya vyanzo vipya vya mapato. Tangaza kama kuna mtanzania mwenye chanzo kipya cha mapato au kwa namna moja au nyingine anafahamu chanzo kinachopoteza mapato awasilishe mawazo yake na apewe asilimia 5 tu ya chanzo atakachoibua ambacho hakimuumizi mwananchi au eneo linalopoteza mapato na atambulike na Serikali. Naamini tuna mawazo mengi sana toka kwa watanzania ambayo yanaweza kuleta mwanga mpya...
Achana na mawazo ya wale wabunge 393 hamna kitu wanajua πππ
Kupanga ni kuchagua:- Tukubali kugombana na wafanyabiashara au tuwafurahishe halafu tugombane na wananchi au tuwafurahishe.
Ole Mushi
0712702602.