Sijui na mie sijawaelewa?! Kwa hayo makampuni ya simu kukutana, ina maana warekebishe humo humo kwenye sekta ya mawasiliano (ambayo haitakuwa tofauti na tozo la sim card), au wawatafutie chanzo kipya?! Aiseee......choka kabisa.
Sasa wanategemea kampuni za simu ziiambie serikali mahali pengine pakupata mapato yake?
Kama hawazitegemei kampuni za simu kujua sehemu nyengine mbadala wa serikali kupata mapato yake, ina maana wanataka hiyo kodi ibadilishiwe sehemu iingizwe huko huko kwenye kampuni za mawasiliano
Sasa umesikia wapi kampuni ikasema tutozeni sisi extra kodi ili wateja wasipate udhia?
Maana yake ni kwamba kodi hiyo tutailipa sisi wananchi kupitia mawasiliano kwa njia moja ama nyengine
Siyo kwenye madini tu hata hizi kodi ndogondogo wafanya biashara wanazikwepa sana wakishirikiana na baadhi ya Maofisa wa TRA wasio waadirifu. Hebu fikiria majuzi nimechenjiana sana na Muhindi mmoja kaniuzia kitu kwa Tshs100,000 akanifungia vizuuri then akauchuna,
Nilipomdai risiti akadai nikitaka risiti niongeze elfu18, nika mbana kwamba kumbe huwa anakwepa kodi kwa kuwashirikisha wateja, nikajifanya napiga simu some where niliporudi mezani kwake nikakuta kaniwekea risiti yangu ikiwa wamemfyeka Tshs18,000 kama VAT, hebu jiulize kama mimi nimekomaa kidogo tu nimeikolea Serikali Tshs18,000 kwa dakika chache tu vipi mamilioni ya Transaction yanayofanywa kila siku bila watu kupewa risiti wala mfanya biashara kuweka rekodi ya mauzo?
Vipi wafanya biashara wakubwa wanaokwepa kodi kwa kiwango cha Mabilioni kila siku??/...................(Lazima tuige mifano ya walipa kodi wazuri kama HOME SHOPING CENTRE).
Mwezi huu mwanzoni gharama za mawasiliano ziliongezwa kinyemela! Kwa mfano nilikua nikinunua kifurushi cha maongezi cha wiki moja kwa shilingi 4999/- na kupata dakika 210,lakini siku hizi kwa fedha hiyo hiyo napata dakika 150 tu!
Kwa mawazo yangu nlijua wameanza tozo tayari maana tuliahidiwa punguzo katika mawasiliano, wakapunguza kisha wakaongeza!
Je watakapofuta hii kodi kisanii kwa jina kisha kubakiza makato katika simu zetu kama kawaida itakuje?
True mimi nadhani tuongeze bidii katika kukusanya mapato na kuzisimamia vizuri sheria na sera za matumizi ya kodi za sisi wananchiwazo lako ni zuri sana. Swali ni je, matumizi ya serikali kutoka hata hayo mapato kiduchu yanazingatia mahitaji halisi ya wananchi? Hakuna asiyepennda kulipa kodi, lakini je matumizi ya kodi hiyo yanawekwa wazi na mwananchi anaimani kuwa kodi yake inatumika vizuri? Napendekeza wanaharakati watafute namna ya kupata fedha halafu waendeshe utafiti kwa kuuliza wananchi kama wanaridhika na mapato na matumizi ya serikali yao sikivu. Waweke na mapendekezo.
watatuongezea tu kwenye beer najua,si wakachukue huko kwenye madini!!!
Nimevutiwa na hii kituikulumawasiliano@yahoo.com
Kama hawazitegemei kampuni za simu kujua sehemu nyengine mbadala wa serikali kupata mapato yake, ina maana wanataka hiyo kodi ibadilishiwe sehemu iingizwe huko huko kwenye kampuni za mawasiliano
Sasa umesikia wapi kampuni ikasema tutozeni sisi extra kodi ili wateja wasipate udhia?
Maana yake ni kwamba kodi hiyo tutailipa sisi wananchi kupitia mawasiliano kwa njia moja ama nyengine
Nimesikitika sana, eti Rais anaomba makampuni ya simu nayo yashiriki kutafuta vyanzo mbadala vya kuziba pengo hilo??
Hii ni level ya juu sana ya kutokuwajibika...
Yaani wanampa fisi ulinzi wa bucha ya nyama.Sasa wanategemea kampuni za simu ziiambie serikali mahali pengine pakupata mapato yake?