Tozo ya VAT katika kununua salio kutoka kwenye simu

kizo83

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
354
332
Umefanikiwa kuongeza Sh 500.00 Tsh.VAT 76.27 Tsh,Salio lako jipya ni 501.28 Tsh.Tumia WhatsApp&FB WIKI NZIMA kwa Sh 1000tu.Piga *148*00#

Sijaelewa hili Naomba mwenye uelewa anieleweshe tafadhali

-----
Sasa ni rasmi kuwa vocha za simu zinatozwa kodi ya ongezeko la thamani maarufu kama VAT. Dakika chache zilizopita nimenunua vocha ya shilingi 5000 kupitia tigopesa.

Katika vocha hiyo,shilingi 752.71 imekatwa kama VAT. Kweli Serikali imechachamaa kukusanya kodi. Ndiyo mambo ya kinchi hayo.

Hiyo VAT inatoka ndani ya hilo salio ulilonunua na si ktk account yako.

Wamekuonesha vat ila haiathiri pesa zako zilizopo.
 
Ndugu, kutokana na agizo la mamlaka ya mawasiliano TCRA,taarifa zote za ununuzi wa huduma ni LAZIMA zionyeshe gharama za VAT.HII HAIATHIRI GHARAMA ZA HUDUMA
Iyo message nilitumiwa kutoka Tigo wameagizwa na tcra kuwa manunuzi yote yanatakiwa yaoneshe VAT kwa mteja
 
Umefanikiwa kuongeza Sh 500.00 Tsh.VAT 76.27 Tsh,Salio lako jipya ni 501.28 Tsh.Tumia WhatsApp&FB WIKI NZIMA kwa Sh 1000tu.Piga *148*00#

sijaelewa hili Naomba mwenye uelewa anieleweshe tafadhali
maana yake n kuwa, tsh 76 ni VAT ILIYOTUMIKA KWENDA SERIKALINI KUTOKA TIGO KUTOKANA NA MUAMALA WAKO
 
Hapa ndipo uongo wa serikali unajidhihirisha, walisema watakao lipa kodi ni makampuni ya simu na si mteja, leo wanatusisitiza tuone kodi TUNAYOKATWA?! Kweli walioichagua ccm octoba 2015, Mungu anawaona.
 
Umefanikiwa kuongeza Sh 1850.00 Tsh.VAT 282.20 Tsh,Salio lako jipya ni 1501.03 Tsh.Tumia WhatsApp&FB WIKI NZIMA kwa Sh 1000tu.Piga *148*00#
 
Habari za jioni wakuu. Nisiwachoshe sana. Nimeshangazwa sana na VAT niliyokatwa sasahivi nilipo nunua mda wa maongezi kwa tigopesa. Nimenunua mda wa sh700 VAT wamekata sh106. Sasa sijui ningeongeza mda wa sh1000 au sh10000 ningekatwa sh ngapi? Barabarani wanatukaba ,kwenye mabeki wanatukaba, sasa wamehamia kwenye muda wa maongezi. Mpaka 2020 nadhani tutakatwa VAT ya kichwa.
8bbee8750cd6a17a5fc8f13dafda4576.jpg
 
Mkuu kumbe bado unatumia tochi?, mbona unaonekana mtu wa heshima sana
 
Habari za jioni wakuu. Nisiwachoshe sana. Nimeshangazwa sana na VAT niliyokatwa sasahivi nilipo nunua mda wa maongezi kwa tigopesa. Nimenunua mda wa sh700 VAT wamekata sh106. Sasa sijui ningeongeza mda wa sh1000 au sh10000 ningekatwa sh ngapi? Barabarani wanatukaba ,kwenye mabeki wanatukaba, sasa wamehamia kwenye muda wa maongezi. Mpaka 2020 nadhani tutakatwa VAT ya kichwa.
8bbee8750cd6a17a5fc8f13dafda4576.jpg
Uongo hausaidii kitu 700-106.78 = 593.22 na ukiangalia vizuri hio huduma kwa wateja haijaisha vizuri yawezekana umeedit hivi mbona watu ni wagumu sana kuelewa...
 
Hapa ndipo uongo wa serikali unajidhihirisha, walisema watakao lipa kodi ni makampuni ya simu na si mteja, leo wanatusisitiza tuone kodi TUNAYOKATWA?! Kweli walioichagua ccm octoba 2015, Mungu anawaona.
Douh kuwa bavicha ni janga la taifa.
Hiyo shlng 76 inakatwa kutoka kwenye mia 5
 
Hiyo VAT inatoka ndani ya hilo salio ulilonunua na si ktk account yako.

Wamekuonesha vat ila haiathiri pesa zako zilizopo.
Hizo fiksi mi jana nimenunua vocha ya 1500 wamekata vat

Umefanikiwa kuongeza Sh 1500.00 Tsh.VAT 228.81 Tsh,Salio lako jipya ni 1500.27 Tsh.Tumia WhatsApp&FB WIKI NZIMA kwa Sh 1000tu.Piga *148*00#

Sasa mi nilisoma message mpaka hapo umefanikiwa kuongeza 1500 basi sikusoma maelezo mengine. Nikarudi menu kuu ili nijiunge university offer ile kujiunga tu wakanikatalia eti sina salio la kutosha ......

Duu nilirudi fasta kusoma vizuri message ndoo nikaona hayo ma vat.

Saizi ukitaka kujiunga university offer ya 1500 nunua tigo rusha ya 2000 .
 
Uongo hausaidii kitu 700-106.78 = 593.22 na ukiangalia vizuri hio huduma kwa wateja haijaisha vizuri yawezekana umeedit hivi mbona watu ni wagumu sana kuelewa...
Mkuu usikurupuke kusema uongo,nilikua naongea na mtu salio likakata ikabaki vishilingi na visenti vyake ndio maana ikabaki sh600.Nilitaka kujiunga kifurushi cha minikabang cha sh600na kitu,nikashangaa naambiwa hauna salio la kutosha kucheki ndio nakuta imebaki hiyo mkuu.
 
jana nilimiywa pesa kweye akaunti yangu ya AIRTEL MONEY , MESSAGE ya mrejesho ikaonyesha kuwa nimekatwa VAT, lakini kungalia Salio hamna kilicho katwa, na leo nimenunua VOCHA ya Tigo kuingiza kwenye simu,message ya mrejesho ukaonyesha nimekatwa VAT lakini kungalia Salio hawakukata chochote. ndio hapo sasa nikaijiwa na wasiwasi kwamba, hawa wanataka kutuanzishia kodi kwenye VOCHA na muamala wa kutuma pesa
 
Leo nimenunua Muda wa maongezi wa 1000/- kutoka airtel money kuja kwenye simu yangu nikakatwa 18% ya tozo ya VATambayo ni tsh 152.54, na kupata salio jipya 731.00.

Je hii ni halali mimi kukatwa VAT?

Mwenye airtel ajaribu sasa ivi aone. Ama kweli tutaisoma namba.
 
Back
Top Bottom