Tozo Tsh. bil. 117, Vituo vya afya 234

AnyWayZ

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2022
Posts
4,885
Reaction score
8,483
Salaaam sana wakuu.

Vituo vya Afya;

Vingine vya kitambo Baba wa Taifa kaviacha, navyo vipya hivyo?

Vingi kavijenga mjomba, navyo vipya hivyo?

Vichache wameongeza jengo tu, navyo vipya hivyo?

Nitajie kituo cha afya kimoja tu mtaani kwao unachojua tumepigwa, usisahau kunitajia na kipya ambacho wamefanya kweli.
(Soma kwenye list)
 
Nchi hii viongozi wakiamua kutetea jambo lao, wanatumia mbinu za kila aina bila kujua kwamba mbinu zao zinaibua maswali zaidi.

Kwa mfano, kama tozo pekee imeweza kukusanywa kwa kiwango hicho na kujenga hiyo miundombinu, je kwa miaka kadhaa iliyopita fedha za uwekezaji, utalii, ushuru wa masoko, mikopo, ufadhili nk, si tungeshajenga viwanda vingi kila mkoa???

Kwanini tozo zionekane kupewa nguvu zaidi kwenye matumizi kuliko makusanyo mengine???

Tozo ni wizi!
 
Bajet kubwa zisizo na maana zenye lengo la kuwanufaisha watawala hutokana na kodi zetu hivyo kila anaepigia debe tozo ni mlamba asali kwa namna moja au nyingine,

Huyu waziri wa tamisemi sura yake haifanani kabisa na kazi anazofanyishwa.
 
Duuh.

Sasaaa zile pesa za covid.

Mikopo WB si mlituambia kuwa zilifanya kazi hizi hizi??

Kwanini mtudanganye lakini.

Hamjui kuwa hayo madaraka yenu ni ya muda tu??

Mtakuja umbuka na msiamini yatayowapata.
 
Kweli kabisa.
Yaani Bashungwa na Biteko, sura zao hazifananii kabisa kusema uongo!
Angepewa tu wizara nyingine, hayo mambo ya uongo uongo wakawaachia akina mwigulu.
Maana amedanganya hadi mawe, yanajua yeye ni rais wa 2015😲🤔
 
Nawashangaa wanavyotumia nguvu kubwa kutetea hizi tozo.

Uwepo wa tozo unaacha maswali mengi sana, wanatakiwa waje na majibu ya kuridhisha, sio kulazimisha kama wanavyofanya.

Hivyo vituo wanavyodai ni vipya vilijengwa lini, ukakamilika lini ujenzi wake, kwa thamani ipi kila kituo?

Haiwezekani wanakusanya tozo karibia kila dakika, hawatuambii mapato na matumizi yake kila mwezi, halafu ghafla wanaibuka na majibu ya jumla kutuambia bil kadhaa zimejenga vituo 264 nchi nzima, huu ni wizi wa mchana.
 
Wangetuwekea michanganuo yote ya Kodi za wananchi na matumizi husika! Sioni haja ya kushupalia tozo kama taifa halijawahi kujengea vituo vya afya
 
Duuh.

Sasaaa zile pesa za covid.

Mikopo WB si mlituambia kuwa zilifanya kazi hizi hizi??

Kwanini mtudanganye lakini.

Hamjui kuwa hayo madaraka yenu ni ya muda tu??

Mtakuja umbuka na msiamini yatayowapata.
Mungu atutetee.Mungu hawezi kutuacha kwenye mikono yavm dhuluma.
Kama kuna dhuluma Mungu hatawaacha salama wao na familia zao
 
Duuh.

Sasaaa zile pesa za covid.

Mikopo WB si mlituambia kuwa zilifanya kazi hizi hizi??

Kwanini mtudanganye lakini.

Hamjui kuwa hayo madaraka yenu ni ya muda tu??

Mtakuja umbuka na msiamini yatayowapata.
234 Health Centers/117bil.=2bil.

Naona awamu hii wametumia bilioni Mbili tu kukamilisha kituo kizima.

Sasa najiuliza zile bajet zinatolewaga mpaka 50bil. Kwa kituo kimoja huwa zinaenda wapi hizo 48bil[emoji848]
 
Value for money na uwazi na uwajibikaji!! Saving ya hazina kuu imekwenda kwenye matumizi Gani!?
 
Ahahah Mwigulu ni Mfalme wa pepo wachafu serikali hii. Namfananisha na hao wadau walokaa juu ya hayo Mawe.
 
Value for money na uwazi na uwajibikaji!! Saving ya hazina kuu imekwenda kwenye matumizi Gani!?
Hivi siku hizi wizara hazichangii chochote katika maendeleo hata zile wizara nyet kabisa zenye kuingiza pato kubwa nchini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…