Rais Samia anawezaje kujenga zahanati 564, Vituo vya Afya 304 na Hospitali 68?

ISRAEL JR

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
1,439
631
IMG-20220423-WA0012.jpg

===
Kunawakati huwa nikimsikia mtu anamsema vibaya huyu Mama natamani kumpiga na kitu kizito kichwani,basi ni vile sheria tu hairuhusu na Mungu hataki,

Hebu jiulize,tangu tupate Uhuru ni lini umewahi kuona jumla ya Zahanati mpya 564 zinajengwa kwa mpigo tena nchi nzima?

Hebu jiulize tena,tangu tupate Uhuru ni lini umewahi kuona vituo vipya vya Afya 304 vinajengwa kwa Mpigo nchi nzima?

Hebu jiulize zaidi, tangu tupate Uhuru ni lini tuliwahi kujenga hospitali 68 ikiwemo ile ya Mbagala kwa mpigo?

Hebu pitia kwa utulivu hii taarifa toka TAMISEMI, then umsikie mtu anamsema vibaya mama kama hujatamani kufanya ninayotamani Mimi.

=====
HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI-TAMISEMI

27. Mheshimiwa Spika
, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais - TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 28.20 kupitia ruzuku ya Serikali Kuu.

Fedha hii ni kwaajili ukamilishaji wa ujenzi wa maboma 564 ya Zahanati katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hadi kufikia Februari 2022, zimepokelewa Shilingi bilioni 23.32 sawa na asilimia 82.69 ya fedha zilizoidhinishwa.

28. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Shilingi bilioni 110.60 ziliidhinishwa kupitia ruzuku ya Serikali Kuu.

Fedha hii ni kwaajili ya kuendeleza na ujenzi wa Vituo vya Afya 304.

Kati ya hivyo, Vituo 52 vilianza kujengwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

Jumla ya Vituo 252 vimeanza kujengwa Mwaka wa Fedha 2021/22.

Jumla ya Vituo 18 vimejengwa kwenye Halmashauri zenye Mapato madogo.

Vituo 234 vimejengwa katika Tarafa zisizo kuwa na Vituo vya Afya na Kata za Kimkakati kupitia tozo za miamala ya simu.

Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 108.05 zimepokelewa sawa na asilimia 97.69 ya fedha zilizoidhinishwa na ujenzi unaendelea.

29. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali ilitenga Shilingi bilioni 81.10.

Fedha hizi ni kwaajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali 68 .

Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 66.80 sawa na asilimia 82.36 zilikuwa zimepokelewa na ujenzi upo katika hatua mbalimbali.

NB, Hizi Zahanati 564,Vituo vya Afya 304 na Hospitali 68 vyote hivi vinajengwa na TAMISEMI tu achili mbali vile vinavyojengwa na Wizara ya Afya sijaviorodhesha hapa.
 
Bila kusahau shule moja za kisasa kwa kila halmashauri ndani ya mikoa yote. Kwa bajeti isiyopungua milioni mianne sabini.
470, 000, 000 piga hesabu tunazo halmsahauri ngapi? Na hizo ni tofauti na yale madarasa ya uviko19
 
Naona una maaba makubwa na rais wako. Kwa hiyo mikopo ya Matirioni ya fedha yaliyokopwa huko Ulaya hujawahi kuyasikia?. Si ndivyo?. Hauishi Tz?. Hizo fedha za Matozo ya simu tunazikatwa tunapoenda kwa wakala kutoa visijenti vyetu kununulia nyanya na zile tunazotuma kwa bibi zetu wanunue mafuta ya taa nazo hukuwahi kusikia. ?. Acha ushabiki.
 
Haya magonjwa yametoka wapi? Badala ya kuua mazalia ya mbu tunagawadawa ya mseto
 
Naona una maaba makubwa na rais wako. Kwa hiyo mikopo ya Matirioni ya fedha yaliyokopwa huko Ulaya hujawahi kuyasikia?. Si ndivyo?. Hauishi Tz?. Hizo fedha za Matozo ya simu tunazikatwa tunapoenda kwa wakala kutoa visijenti vyetu kununulia nyanya na zile tunazotuma kwa bibi zetu wanunue mafuta ya taa nazo hukuwahi kusikia. ?. Acha ushabiki.
Wewe unasemaje kuhusu haya matokeo mkuu
 
Back
Top Bottom