Toyota Tanzania

well spoken, kujipanga ujipange haswa !!! Toyota VX V8 200, bila kodi ndani ya nailoni 175 mil Tsh, Prado TX ya kawaida bila manjonjo 135 mil Tsh, Prado Tx (executive) 147 mil. hapo bila kodi zote hizo. sasa ukiinclude na kodi sasa ni habari nyingine, unless otherwise you are about to purchase kwa ajili ya matumizi ambayo yana msamaha wa baadhi ya kodi.

OMG....kama bei ndo hizo bac wabongo ss ni matajiri sana mana hayo magari nayaona mengi tu kila kona ya nchi hii...duh
 
Hivi mkitoka Dar kwenda Mwanza mwenye gari jipya na la used nani anaanza kufika? Nauliza tu jamani
 
Rizwan sikia Hiyo Mifano yako imekaa kimagamba gamba (Msukule) umetumwa wewe!

Watu wasio na uwezo wapo wengi sana tanzania hii hata Kikwete haelewi kwanini, wewe upo nje unataka watu wafanye kazi kwa bidii zipi?
kazi za Tz kuanzia saa kumi na mbili Mornie hadi giza lianze kuingia kipato ni chini ya dola moja sasa kununua gari mpya tujuavyo si chini ya 20,000 usd labda Tata ile ndogo india wanauza 2500 usd ikifika bongo ni 5000 hadi sita hicho kipato cha chini ya dola moja akikusanye kwa muda wa miaka mingapi aache kula ili anunue gari mpya ? dah sipati picha Watanzania 75% Ni Misukule Nimeamini...

Pesa zinawawasha wakopesheni hao wasio na uwezo wanunue gari Mpya!

Babu mi sio Rizwan, naomba unipi heshima yangu. Mtu kuitwa Rizwan ni tusi! Mi sio fisadi. Mi nategemea kurudi na kuiendeleza nchi yangu.

Tuiendelezeni nchi yetu, na narudia tena TUFANYE KAZI KWA BIDII na kuiendeleza nchi yetu. We kama una tatizo lolote linalokukwamisha katika maisha yako jaribu kiujifunza na kupata elimu zaidi. Utaniambia hauna hela ya ku take classes, sasa bajeti yako unayoitumia kuingia internet cafe na kuandika ujinga kwenye jamiiforum na kushindia facebook siku nzima, kwanini usitumie muda huo kuangalia semina mbalimbali kwenye internet zinazofundisha mambo ya maana na kutatua matatizo yako? Nasema hivi kwasababu mimi mwenyewe nimeitumia internet kujifunza mambo mengi sana mpaka najua mambo ambayo watu waliomaliza chuo kikuu wengine hawayajui. Sijisii au vipi ila nasema kwamba tuitumieni hii elimu ya bure iliyoko kwenye internet kutatua vikwazo vinavyotupata katika jamii. Si lazima kufanikiwa katika maisha lazima upitie chuo kikuu. Mi namjua jamaa mmoja hapa Finland alifeli high school uko bongo then bro wake akamwalika kuja kusafisha mamcho huku. Jamaa alipofika huku akawa anatumia muda mwingi kujifunza mambo ya web design kwa kutumia videos zilizoko kwenye website. Baada ya miezi miwili jamaa akapata ajira kwenye kampuni flani ya web development hapa sasa ameamua kubaki huku na anapata mshahara wake.

Nachosema ni kwamba badala ya kukaa nyumbani na kusema kwamba huna elimu na kikawa kisingizio chako cha umaskini ulionao, nadhani ni wakati wa kuingia kwenye internet na kutafuta vitabu na videos zitakazo kufundisha mambo mbalimbali mfano biashara nawe unatoka na kuanzisha biashara yako, kopa hela hata kwa ndugu zako anzisha kinyozi au biashara yoyote baadae itakua. Kuanzaisha biashara ni kujiamini tu na kitakachokufanya ujiamini ni kujiongezea ujuzinkwa njia yoyote ile na hapa ni internet. Hivi hujawahi kujiuliza kwa nini sasa hivi uchumi umedondoka lakini kuna watu still biashara zao zinakua?? Wanatumia uchawi? Hapana! Na asilimia 75 ya matajiri walikimbia shule kwa taarifa yako! Wengi wao walitumia ile nafasi ya kwenda shule kutumia zile library na vitabu kujifunza wenyewe kisha wanatimka zao!
 
OMG....kama bei ndo hizo bac wabongo ss ni matajiri sana mana hayo magari nayaona mengi tu kila kona ya nchi hii...duh

Wabongo sisi ni matajiri sana kama tukiamua kuwa. Na haimaanishi kwamba matajiri wote waliopo bongo ni mafisadi! Watu wameshaweka ile mentality kwamba huwezi kuwa tajiri unless uibe! hawaamini tena kwamba hata wao wanaweza. Tajiri mmoja alisema, 'kama umezungukwa na umaskini, ukitaka utoke huko unahitajika uongeze ujuzi kwa njia yoyote ile iliyopo na ujifunze na kufanya wanachofanya waliofanikiwa nawe utafanikiwa'. Kuna watu wanaamini kwamba akianzisha biashara ya maana ndugu zake au jamii itamloga!! so wanabaki maskini! Uliza mitaani huko utaambiwa.

Ngoja nikupe mfano mwingine, mi hapa nasomea biashara so wakati wa practical training yangu nilikutana na jamaa moja ana kampuni yake na alikuwa ana matatizo kidogo kwenye upande wa sales akawa anahitaji ushauri. Usiku wake niliporudi home nikaingia kwenye internet nikajifunza mambo ya sales kwa masaa kadhaa. Kesho yake nilipokutana nae nikamshauri, akafurahi sana akanilipa hela ambayo nililipa rent ya mwezi ule! Nachosema ni kwamba ukikiamnini nachojifunza kwenye internet unaweza kukitumia na ukafaniikiwa sana. Watu hawaiamini elimu inayopatikana kwenye net coz hawajaipatia chuo kikuu!! Kila kitu ni kujiamnini tu washkaji. Tena huko bongo ideas kibao hazijawa introduced so opportunity za kutengeneza hela ziko kibao

Yaani wewe kila wakati ukifikiria tu tatizo linalokusumbua, ingia kwenye internet jifunze jinsi ya kulitatua!
 
Back
Top Bottom