Toyota Premio inakimbia kuliko X- Trail new Model

Haya mambo ya sijui gari fulani inakimbia sana ni utoto wa chekechea na darasa la kwanza!Nilipokuwa chekechea ndiyo umri pekee ambao nilikuwa nashobokea gari kukimbia sana.Ukimuona mtu mzima anashobokea magari kukimbia jua huyo ni punguani.Mtu mzima unapaswa uzungumzia mambo ya features za usalama,comfortability,durability ya gari,fuel economy,upatikanaji wa mafundi wa kisasa na kadhalika.
Mtu mzima kuzungumzia fuel economy ni utopolo...
 
Mtu mzima kuzungumzia fuel economy ni utopolo...
kabisa.. . kuna jamaa alisema mtoa ile comment ni mtoto. yaani eti anaona kuulizia gari yenye mbio ni utoto kumbe yeye ndo anaonesha utoto. angeambiwa aende mwanza akiendesha tractor basi au akiendesha bajaji au aende mwanza na passo bila kulala njiani. watu wanataka magari na wengine wanatak amagari yenye speed kubwa.
 
Nakubali kwa 100% mkuu,hata 10 2 position naona nayo ishakataliwa na wataalam.

Hio comment yako nimecheka sana maana najua huyo blaza hua anapenda kuonekana unique kwny vitu vyote so hawezi kubali kama anakosea kwny hilo,hahah.
Najua nakosea ila ndo nshzoea.

Saa 9 kamili nimezoea sana kiasi kwamba naweza kufanya manuvers zozote kwa urahisi.
 
Kijiji kwenu mko vizuri.
Yaan unakuta mtu hana hata nyumba ya tofari ila kapaki premio njee. ni maajabu

Kuna binamu/ kaka yangu ana kijumba kidogo sio cha tofari 😂chenye vyumba vitatu, ana watoto 6😂 tunalingana umri😂😂 lakini nje kapaki premio yake.humwambii kitu. kweli gari ni basic need.
Maisha ni kuchagua.
 
Crown inabidi utumie akili, ukiivamia kichwa kichwa inakuumbua. Dawa ya Crown kama una VW au Audi yenye engine ndogo msubiri sehemu ndefu. Lakini mbio fupi,tuta hapa na pale itakusumbua sana.
Vinachanganya chap chap sana. Kuipata 120+ ni chap. Maana kwa mfano kutokea mwanzo wa kijazi hadi mwisho tayari mtu 160 + na hizo zilizobaki huwa naweka reserve, na kutokea usiku hakuna noma, mwisho wa kijazi hadi taa za kivulini 180+ vizuri tu umemaliza na mguu wa kwenye wese hauna kazi tena
 
Back
Top Bottom