Kwanini vyombo hivi hupendelewa zaidi na watu kutoka Taasisi za Ulinzi haswa wa Jeshi la Wananchi?

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
May 17, 2018
358
670
Salam wana jukwaa.

Kwa maoni yetu zifuatazo ni sababu za kwa nini walinda amani wetu hupendelea zaidi gari za aina flani kuliko aina nyingine kwa gari zote za biashara na binafsi.

1. Toyota IST, Toyota Vitz, Toyota Starlet, Run X, Allex na Raum na Subaru Impreza.

Hizi hupendelewa zaidi kwa wale ambao ni vijana kama sisi na bado wana malengo ya mda mrefu ya kimaisha hivyo hupendelea gari hizi ndogo na za chini kwa kua zinatumia mafuta kidogo wastani wa kilomita 16-18 kwa lita moja. Lakini pia vifaa vyake vina gharama nafuu na vinapatikana kila kona ndani ya nchi yetu. Jambo jingine ambalo huvutia zaidi kwa gari hizi ni gharama nafuu ya kuzimiliki. Kwa kuagiza IST ya miaka ya 2002 mpaka 2004 hugharim jumla kuanzia 10.3m wakati Vitz ni old na new model huanzia 8.9mm, na Starlet pia gharama zake ni 8.8m kwa zile za milango 5 na 9m kwa ambazo ni milango 3 maarufu kama Starlet Granza, kwa upande wa Toyota Raum nayo ina gharama nafuu kuanzia 10.5m, wakati Allex na Run X huanzia kwa jumla ya 10.8m. Gharama hizi hujumuisha Manunuzi ya Japan, Usafiri kutoka Japan, Ushuru wa TRA na gharama za bandari na Usajili. Kwa impreza hufika kuanzia 11.8m na mafuta kidogo kama IST ya Cc 1500 lakini hii ni imara zaidi iwapo barabarani.



2. Toyota Spacio, Porte, Sienta na Fun Cargo

Kivutio cha gari hizi hakitofautiani sana na Gari za kundi la Kwanza. Hizi nazo hutumia mafuta kidgo japo kwa mwonekano huonekana kua na bodi kubwa ambalo lingeweza kuchangia matumizi ya mafuta yakawa juu kidogo ya hizo nyingine, ukweli ni kua hizi gari bodi zake ni nyepesi na hazipishani mbali uzito na gari hizo hapo juu. Wengi hupendelea gari za kundi hili kwa kua kidogo ziko juu, na mvuto zaidi hunogeshwa na ukubwa wa nafasi ya ndani. Kwa ndani kun nafasi kubwa kidogo haswa kwa watu watakao kaa nyuma kwani mara nyingi hua miguu haigusi viti vya mbele. Uzuri wa gari hizi huvutia zaidi askari wetu kwa imani kwamba hizi zilizotengenezwa miaka ya kuanzia 2004 zitakua zimeboreshwa zaidi kwa kua teknolojia hukua siku hadi ziku, tofauti na zile zilizoanzia miaka ya 1998 kuja mpaka miaka ya 2002. Mwisho kabisa kwa gari za kundi hili ni kwamba zote manunuzi yake hucheza kuanzia 8.2m mpaka 9m na hivyo kuleta unafuu zaidi kwa mnunuaji.

3. Toyota Premio, Allion, Mark 2 Gx 110, Alteza, Brevis, na Carina T.I na S.I

Hizi gari huvutia askari wetu kwa sababu kadhaa lakini kubwa ni muundo wake ambapo ndani ziko huru zaidi haswa kwa kua zina sehem za kuegemea kwa sehem zote za mbele na nyuma, na dash board yake hua na mvuto zaidi kwa kua hua na marembo kama ya ubao ulionakshiwa kwa rangi za kuvutia. Hizi ukilinganisha na gari nyingine tulizoona hapo huu, hizi huonekana zaidi kua ngumu kwa upande wa kuhimili shida, lakini pia hata kwa safari ndefu zinaenda bila wasi wasi. Kwa upande wa mafuta hapo ni gari moja aina ya Brevis ndio huonekana kutumia mafuta mengi zaidi kwa kua injini yake ni Six Cylinder na hivyo kuifanya iende wastani wa kilomita 10 kwa lita ikifuatiwa na GX 110 ambayo huenda wastani wa kilomita 12 kwa lita wakati hiz nyingine huenda kilomita 15 kwa lita. Mvuto mwingine kwa gari hizi hua ni nguvu yake nzuri ya kufua ubaridi au AC. AC yake husambaa kwa kasi na ikimpata fundi mzuri zaidi hua ni kali kulinganisha na hizo za juu. Gharama za uagizaji mara nyingi huanzia 11.8m kwa aina zote ispokua kwa Carina T.I na S.I ambazo hua zinaanzaia 10m

4. Toyota Rav 4, Harrier (Kluger), Nissan Dualis, Pajero IO, Nissan X trail na Toyota Voltz, na SUbaru Forester

Kwa baadhi ya wanajeshi akishakuja anaipenda gari ya aina hiyo hapo juu hua hakuna mjadala lazima apate ya hivyo hivyo. Hizi wanazipenda zaidi kwa kua ziko juu juu, gari za safari, zina 4WD, lakini kwa uzuri wa sifa zake ikilinganishwa na manunuzi yake hua ziko chini kidogo tofauti na baadhi ya gari nyingine za juu juu zaidi ambazo pia manunuzi yake hua juu zaidi. Kwa upande wa maintanance, hapo gari za Toyota ziko chini zaidi kwa kua injini zake hazina masharti magumu, ni rahisi kwenye matengenezo na vifaa vyake vinapatikana kila kona na kwa gari baadhi ya nyakati vifaa vya Harrier old model huingiliana na vya Rav 4 old model.

Gari kama Nissan Dualis wanaipenda pia lakini matengenezo yake kidogo yana masharti haswa kwenye aina za oil gani itumike na kwa ujumla vifaa vyake vinapatikana ila sio kila sehem kwa kua hizi gari bado ni chache hapa kwetu na gharama yake pia inakua juu kidogo, hii ni kwa pamoja na SUbaru forester. Kwa upande wa Nissan X trail, ni nzuri pia ila haswa hizi za miaka ya 2008 kuja juu, zile za chini ya hapo yaani miaka ya 2007 kushuka chini nyingi mfumo wake wa rejeta huzifanya kutoweza kuhimili safari ndefu haswa kwa nchi yetu hii yenye joto na hivyo kuchemsha katika baadhi ya nyakati, ingawa siku za hivi karibuni mafundi wengi wameziweza na kuzifanyia modification kwenye rejeta hivyo kuziwezesha kufanya safari ndefu bila shaka. Pajero IO ni ina sifa za kua gari ngumu na nzuri sana mbadara wa Suzuki Escudo na utumiaji wake wa mafuta ni wa wastani kwa kua nyingi zina injini ya GDI ambayo ni kama VVti ya toyota kwenye matumizi ya mafuta. Mafundi wapo na spea ni nyingi sana hapa nchini isipokua 4WD yake ina nguvu ya wastani tofauti na gari kama Harrier, Rav 4, Subaru au hata X trail. Gharama kwa gari hizi zote huanzia wastani wa 14.5m mpaka 19m isopokua kwa Pajero IO na Nissan Old Model ambazo gharama yake huanzia 11.8m

5. Noah na Alphard

Hizi wanazipenda zaidi kwa kua ni gari za familia na hubeba watu wengi zaidi. Rahisi kwenye matengenezo na vifaa vinapatikana kila sehem hapa nchini. Kwa wastani Alphard inatumia mafuta zaidi ya Noah lakini pia iko na balance nzuri barabarani tofauti na Noah. Noah ni kama tolea la kizamani la gari za Toyota kwa matumizi ya Familia, wakati hizi Alphard ni toleo la kisasa haswa kwa kuzingatia zimekuja kuingia sokoni miaka ya mbeleni baada ya Noah. Gharama za kuagiza gari hizi zote kwa wastani hua ni kuanzia 14.5m na kwa Noah new model hua ni 12m

6. Nissan Civillian, Mitsubishi Rosa na Mitsubishi Canter

Hizi ni gari za biashara za mizigo na abiria. Ikitokea tukapata wanaotaka kuagiza gari za biashara kama hizo hapo juu mara nyingi huchagua za majina hayo kwa kua Cillian na Rosa hua na gharama nzuri sokoni, Rahisi kuzihudumia lakini pia zinafaa zaidi kwa safari za ndani ya mji kama daladala na mizigo ya safari fupi kwa hizi Canter. Ki ujumla gharam za Rosa hua ni kuanzia 33m wakati Canter hufika kwa 23 kwa ile ambayo so ya kubinua na kwa 28m kwa ile ya kubinua.

Kwa uchache tumeweza kukuandalia hayo, karibuni nanyi ndugu wadau muweze kutoa maoni yenu.

0746267740
 
Back
Top Bottom