Toyota Ipsum Model 240S (PICNIC)

Toyota Ipsum Model 240S (PICNIC)

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
18,116
Reaction score
28,018
Wadau nina mpango wa kununa hiyo Gari,nimejaribu kuifuatilia kwenye internet inakwenda 12km kwa lita1 na kwa upande wa engine ni VVTi sasa ningependa kujua ubora wa hii gari,utumiaji wake wa mafuta kwa matumizi ya safari ndefu na mjini,upatikanaji wake wa spare na mafundi kwa aina hiyo ya engine kama wapo hapa mjini n.k.
 
Wadau nina mpango wa kununa hiyo Gari,nimejaribu kuifuatilia kwenye internet inakwenda 12km kwa lita1 na kwa upande wa engine ni VVTi sasa ningependa kujua ubora wa hii gari,utumiaji wake wa mafuta kwa matumizi ya safari ndefu na mjini,upatikanaji wake wa spare na mafundi kwa aina hiyo ya engine kama wapo hapa mjini n.k.

gari tamu sana hyo mkuu,chukua,ila dola imepanda sana kaka msimu huu kama unataka kuagiza,kila la kheri
 
Mkuu steveachi nichambulie kidogo nipate huo utamu wa hiyo gari pls.
 
Last edited by a moderator:
Hii kitu ni nzuri sana. kwanza ni spacious- ukikunja viti utabeba mizigo mingi ajabu.
nguvu-hii kitu ina nguvu balaa, na kwa vile ni ndefu, imetulia barabarani na unawezafika 160km/hr bila kuona tofauti yoyote.
Parts- zinapatikana kiurahisi, kama ilivyo kwamagari mengi ya toyota.
Mafundi- mafundi wengi wa kibongo ni wababaishaji kama kawaida. inabidi utulize moyo wakati wa kumtafuta fundi.
Vvti engine- ukizingatia service , uendeshaji sahihi na mafuta mazuri, itachukuwa muda mrefu hata miaka 8 bila hitilafu ktk engine.

kwa ujumla, ni gari zuri mno, usiliache
 
Mkuu steveachi nichambulie kidogo nipate huo utamu wa hiyo gari pls.


Hiyo gari Mkuu kwanza body yake ni kubwa,inaweza kuchukua watu saba bila tabu,kwa hiyo kama una family trips to up-countries(mikoani) ni usafiri maridhawa sana

Mbali na hilo pia injini yake ni kubwa kama cc2360 hivi hivyo kwa sfari ndefu inaweza sana tu, pia pamoja na ukubwa wa injini yake,pia inakula mafuta sio vibaya sana,inakwenda kati kilometa 10-13 kwa lita na

Upatikanaji wa spea zake ni mzuri kwani zinapatikana kwa wingi sana si unajua tena hiki ni kitu cha TOYOTA hivyo spea kibao zinaingiliana na toyota nyinginezo,ipo vizuri sana mkuu

Kwa nyongeza zaidi kwa kuwa ina body inayovutia,unaweza kuitumia kuikodisha katika shughuli mbalimbali za sherehe ukapiga mkwanja mdogo mdogo huku maisha yakisogea na watoto wakipishana vyooni tu

Kila la kheri Mkuu stephot
 
Last edited by a moderator:
Nina miliki hiyo gari na kwa sasa ni ya Mama kw ajili ya kuendea watoot shule na tukiw ana safari ndefu au za beach au mtoko wowote w akifamilia hili ndio gari maana humu unaingia wewe na wife, watoto, housegirl na house boy na hata majirani na bado kitu kimetulia.

Cha kuzingatia ni kuwa hiyo model PICNIC achana nayo maana huw anaiona ni ndogo na huwa nahisi sio Imara, tafuta 240s/i ya kwaida isiyo kuwa na nembo ya Picnic.

Pia kwenye mafuta kiukweli wenyewe wansema ni 12Km na wadu humu wnasema ni 10Km, Mimi yangu inatembea 6Km na nahisi inamatatizo ila nimekataa kuitengeneza maana sijuhi ni fundi gani wa kulitatua hili tatizo na naogopa kuanzisha tatizo lingine juu ya tatizo lilopo, as long as ni gari amabyo haitumiki sana na ni kwa safari fupi fupi nimekubaliana n ahayo matokeo ya 6Km, kuliko kwenda jufanya majaribio.

Pia matatizo mengine ya hili gari ni Ball Joint mara ntingi zina kuja zimekwisha au zimechoka na baada ya mwaka utaweza kugundua kuwa kuw azimekwisha na utabadilisha.

ila tatizo jingine amablo ni Common ni Brake hizi huwa azichuki miezi 6 gari likifika mjini unabidi ubadilishe ni me experiance hili kwa magari mawili ya haina hiyo yalioagizwa kipindi tofauti yote yalipo fika ilibidi ubadilishe brake badal ya miezi michache.

zaidi ya hapo kilalaheri.
jitahidi upate lenye camera front na rear pia lenye controling button kwenye usukani, ni tamu sana ukipata kam hili.
Pia kama upo serious naweza kukusaidia kutafuta kw amaan ya kupoint(sio kukuagizia) na ukaagiza wewe mwenyewe.


attachment.php



i.jpg
 

Attachments

  • f.jpg
    f.jpg
    32.6 KB · Views: 161
  • b.jpg
    b.jpg
    35.3 KB · Views: 164
  • e.jpg
    e.jpg
    40.7 KB · Views: 139
Back
Top Bottom