Hivi ulimuona yule jamaa aliekufa kwenye Hilux? Alibanwa yuko hai kuanzia usiku hadi saa nane hivi ndio akafa anajiona. Yaani watu hawawezi kumtoa wanabaki wanapiga nae stori. Simjui yule jamaa ila roho iliniuma sana. Hatuna rescue team wala nini, ukipata ajali hadi kupata msaada ni masaa, halafu madogo bado wanafanya mchezo na haya magari. Nakumbuka maneno ya yule jamaa 'haya magari haya...'