Toyota brevis: Kwanini haya magari yanaonekana ni luxury lakini ni rahisi?

bugzbunny

JF-Expert Member
Mar 9, 2013
839
755
Hivi ni kwanini haya magari yanaonekana kama ni luxury cars lakini thamani yake sokoni ni ndogo sana? Yana shida gani?

Mfano Toyota Allion/Premio yenye engine size mdogo labda 1500cc au 1800cc inauzwa ghali sana kupita hii gari.

Wadau nijuzeni.

Nimeisahau na Altezza yani jina na bei tofauti.
 
Hivi ni kwa nini Haya Magari yanaonekana kama ni luxury cars lakini thamani yake sokoni ni ndogo sana? Yana shida gani? Mfano Toyota allion/premio yenye engine size mdogo labda 1500cc au 1800cc inauzwa ghali sana kupita hii gari, wadau nijuzeni. Nimeisahau na altezza yani jina na bei tofautii.
...ni kwasababu gari kama brevis inakula mafuta kuliko premio yenye injini ndogo....ukweli ni kwamba gari ambayo inakula mafuta kidogo (fuel economical) ina bei kubwa kuliko yenye kutumia mafuta mengi..ndio maana utashangaa ka gari kama IST kana bei kubwa kuliko altezza....
 
Nadhani pia mwaka wa matengenezo unaleta tofauti kubwa kwenye bei
Mfano Brevis zilianza production 2001-2007 ukilinganisha na Premio ambazo ni kuanzia 2001 mpk ss hv..
Kwenye soko uangalie na hilo wakati unalinganisha..

Maledhi
 
Hivi ni kwanini haya magari yanaonekana kama ni luxury cars lakini thamani yake sokoni ni ndogo sana? Yana shida gani?

Mfano Toyota Allion/Premio yenye engine size mdogo labda 1500cc au 1800cc inauzwa ghali sana kupita hii gari.

Wadau nijuzeni.

Nimeisahau na Altezza yani jina na bei tofauti.
Jaribu kuinunua Brevis ndio utajua kwanini ni luxury
 
Back
Top Bottom