Tovuti ya polisi tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tovuti ya polisi tanzania

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtazamaji, Nov 28, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu
  Leo nimetembelea tovuti ya Tanzania Poice Force .

  kwanza nilifurahia ule muonekano wake. Hatua ya pili nikasema ngoja nijaribu functionalities kahaa Nikaenda kwenye feedback. Hapo kwenye feedback nikataka kuandika ujumbe .Nikashindwa kutuma sababu lazima uweke attachemnt. Sijui ni attachment gani. na vile naambiwa "Please specify your position in the company". Nikachoka Kabisa. Sasa sijui dhumuni la dhumuni la hii tovuti ni nini . Ni kutoa tu habari au ni kutoa na upokea.......??????

  Kama kuna watu wako karibu na wahusika wa ICT wa polisi basi nawashauri wajaribu kutazama Tovti hii i ya Polisi ya UK na wajaribu kuchukua yale mazuri wayapachike kwenye tovuti yao. Tovuti ya Polisi isiwe ya kutoa tu habari bali iwe ya kupokea habari kirahisi na ziwe habari za wanachi wanazotaka kusoma au kuona.

  Mambo kama ya URASACCOS sio muhimu kwa watembelaji wa tovuti kama ilivyo matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa au yanayofanyiwa kazi.........

  Na scanning niliyofanya kwa nyenzo za ku- Audt mtandao kwenye webserver zinaonyesha wametumia CMS ya joomla na template ya comaxium wich is good , lakini tatizo sanning inaonyesha kuna risky loophole kadhaa inabidi waifanyie kazi moja wapo ni
  Otherwise taratibu tutafika...............
  Nawasilisha
   
 2. f

  fungamesa Senior Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nenda ukawashauri wajaribu kuwa Updates
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwenda kuwashauri ndio hivi nimeshafanya electronically . Faida ya internet moja ni kuwa imefanya Dunia kuwa kama kijiji. Au kama niko kigoma mwisho wa reli unatak nifunge safari mpaka kwenye ofisi ya Mwema na vijana wake.
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mtazamaji unasema kweli. Kama wana nafasi ya kuja kufuatilia watu wanaisema nini serikali yao sasa kwa nini wasisome haya na kufanyia kazi?
  Kama, hawana nafasi ya kutembelea maeneo ya huku hiyo ni shauri yao. Ushamba ni mzigo.
   
 5. geprony

  geprony Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  No suprise nimeicheki yaani inaelekea wataalamu wao ni mambo ya undugu tu sio competent kabisa shame on them.
   
 6. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu mtazamaji,

  Ni wazo zuri sana hilo lakini Metropolitan Police ni taasisi kubwa sana na ndio maana unaona kuna mambo mengi mno.

  Kuna thread moja nilizungumzia kuhusu uundwaji upya kwa jeshi letu la polisi na nilitoa baadhi ya mapendekezo nafikiri ni mbali mno (si unafahamu tena sisi watu wa siku nyingi hapa JF?)

  Met police ni kama wizara nzima na wana kamishna na ambae ndio kama IGP wetu, halafu ana assistant wake na pia anatawala jeshi la police la London au City of London Police, kwahio tovuti yake inabeba mambo mengi sana.

  Baada ya hapo kuna vikosi vya polisi nchi nzima vikiongozwa na chief constables ambao ni kama RPC wetu. Ukitoka hapo unakuja kwenye taasisi zingine kama vile chama cha maofisa wa polisi ambao wana asili ya Afrika na Asia.

  Halafu kuna idara shiriki au partners kama vile fire brigade, ambulance service na national health service. Baada ya hapo unakuta kuna taasisi za kimataifa ambazo zinashirikiana na met police kama vile CIA, Interpol, FBI na internationall police association.

  Sasa mwenye jukumu la kuandaa website ya jeshi la polisi la anatakiwa awe amepewa blue print yenye maana yaani iliyojaa mambo mengi ambayo yamesheheni elimu msaada kwa wasomaji na mambo mengi tu, ili siku ikiwa tested online watu tuseme alaa kumbe!

  Lakini mtu hawezi kukurupuka na kuja na tovuti kama hii ambayo ni ya mtoto wa sekondary anaejifunza kutengeneza tovuti. Tumefika miaka 50 ya uhuru halafu ndio mtu anakuja na hii tovuti yaani ni mambo ya ajabu kabisa.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Wa Tanzania kwa Mambo ya Computer bado tupo nyuma sana sijuwi tutakuwa mbele lini?
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Rchard Naukbalina na wewe lakini naomba nifafanue kwa nini nimetolea mfano wa Tovuti ya Polis ya UK. Sijafanaisha structure na muundo ya polisi wa Tanzania na UK bali nimefanisha mhitaji na presentatin tovuti. Hata kama strucrure , ukubwa na department ni tofauti bado infomration zinazotakiwa kutolewa au kupokelewa ni zile zile

  Mfano utaona MET ya UK wanapokea na kutoa habari kwa njia mbali za ICT
  • twiitter ya Polisi ya uk . Saijawai kusikia official page ya polisi ya fb na twtter. Na hii ilitaiwa kila mkoa ziwepo.
  • Yutube channel ya MEt UK Kwa hii siwezi kuwalaumu sana sababu hata chombo cha habri kama Tbc hawana channell
  • Feedback hii nimetlea mfano nimejaribu kutoma maoni nimeshindwa. tovuti ya Polisi inataiwa iwe inatoa naupoea habari. Matoeo yake wanatuwekea mambo ya Saccos. Sasa saccos ya Polisi ina maslahi kwa mtu anayetembea tovuti.
  Watu wanataka kujua kufahamishwa
  • watu gani ni wanted
  • wahalifu gani wamekamatwa
  • vitu gani vinafanyiwa kazi
  • matukio gani ya kihalifu yanashamiri na yanatkoea wapi na wanashauri nini

  Ni mambo kama hyo ndiyo mtazamao wangu waangalie Presentation ya tovuti ya Polisi ya UK wachukue mazuri. katika karne hii hatuhiaji idaraya habri maelezo ya Posta . twiiter/ facebbook ndio idara ya habari maelezo za kisasa ambayo iitumiwa vizuri itatoa taarif kwa wakati sahihi. Polisi jamii ya kweli na ya kisasa inatakiwa kuwa na official account facebook na twiter
   
 9. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mtazamaji,

  Tupo pamoja kabisa na hizi "social network" ndizo mtu unapata habari nyeti.

  Nikuchekeshe kidogo siku hizi watu wote wa intelligence Ulaya na Marekani wanapita humo kuchagua "recruits"
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  unataka mwenzio atiwe kizuizini kwa uhaini? Unachezea polisi waliopewa leseni za kuua raia wasio na hatia?
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hahahaha na wa hapa kwetu bongo wanapita wapi tuwaombe kazi au bado sheria zao ni mpaka uende CCP moshi ndio uwe web admin au ICT officer wao?
   
 12. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu mbona umeenda mbali sana, umesahau kuwa hata emergence call number yao kuna wakati haifanyi kazi, ndio itakuwa tovuti?
  Kimsingi kuna udhaifu mkubwa katika kitengo hiki, hawaamini kama raia mwema anaweza kusaidia kutoa/kupata taarifa za kiusalama ktk tovuti yao, wao wanaamini kila kitu kitapatikana kwa kutegemea intelijensia yao na press confrence za Kova.
   
Loading...