Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,976
Jamani wanaJF nimetembelea tovuti (au wavuti? Not sure with this) (website) ya Bunge letu tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuona kama wameweka Sheria mbali mbali zilizopitishwa na Bunge hilo kwa mwaka 2009 lakini kwa bahati mbaya Sheria zimeishia mwaka 2008! Tatizo ni kwamba hakuna mafungu ya ku-edit hiyo tovuti (wavuti?) au namna gani?
Sasa hivi tunasikia kwamba wanajadili Muswada wa Matumizi ya Fedha za Kampeni za Uchaguzi, si ingekuwa vema tukaupata Muswada huo kutoka kwenye tovuti (wavuti?) ili tuujadili kwenye "Bunge Letu Tukufu la JF" ambalo huwa liko makini kupita maelezo? Maana hapa JF waandishi wa habari wenyewe huwa wanakuja kuchukua taarifa na kwenda kuandika kwenye magazeti yao! Spika 6, do something please!