Touched: Kwa nini tusivunje muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Touched: Kwa nini tusivunje muungano?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LUPITUKO, Jan 26, 2012.

 1. LUPITUKO

  LUPITUKO JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 60
  Nimekuwa nafatilia sana malumbano ya wenzetu wa ZNZ toka nikiwa shule ya msingi na sasa nazeeka, mwanzo ilikaa kisiasa zaidi kwa hio nilikuwa sitilii maanani ila sikupenda sana walipokuwa wanatumia umeme wetu bara na hawalipi na kwenda kwao kwa passport wakati wao wanaingia ovyo kwetu.
  Hayo nadhani yalishughulikiwa nadhani hasa la passport.
  Kinachoniumiza mimi sasa hivi ni jinsi Watanganyika wenzetu wanavyonyanyasika ZNZ kwa kubaguliwa na kunyimwa haki ya kujijenga kimakazi na kibiashara kiasi imefikia makanisa kuchomwa moto na biashara za pombe, na hata watu kuuawa kwa misingi ya dini(kanisa) au kuuza pombe.
  Nakerwa zaidi nipoona hawa wa ZNZ wamejazana kwetu Tanganyika na wanaishi peponi kwa raha zao wakifanya chochote wapendacho bila bugudha! Yaani wamesambaa nchi nzima na wanajimlikisha ardhi , biashara, na miradi mikubwa mikubwa bila tatizo lolote.
  Kwao kila kitu ni issue, ukiomba kupanua mpaka wa bahari ni issue, IOC, FIFA,URAIS, KODI,BENDERA,MAHAKAMA nk yaani mabo meeengi kucha kuchwa ni malalamiko tena hata bungeni na kwa lugha chafu.
  Ninachojiulizaga mm ni hv hawa jamaa tuna faida gani nao ambayo mm kwa umri huu siijui na nisiri kubwa kiasi hazungumziki na ndio maana tumeng'ang'ania muungano usiokuwa na faida yeyote kwetu?
  Kwa nini tusiuvunje tuwatimue warudi kwao na sisi tukae kwetu?
  Naomba majibu jamani wenye kuelewa kwa undani zaidi faida ya Muungano Huu Fake, zaidi ya kusikia kila siku oooooh tunamuenzi Baba Wa Taifa!
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kwani tuwe na muungano?
  then u wl get on why tuvunje muungano...:nerd:
   
Loading...