Tottenham Hotspurs Thread

Tafuta ulinganifu wa alichopata Tottenham kuingia finals UEFA vs alichopata Chelsea kwa kushinda Europa.

Utabadili haya mawazo.
Hapo sijatafsiri mafanikio kama mapato ambayo klabu imeingiza. Kama shabiki, mafanikio ni kile kinachovunwa kutoka uwanjani, vikombe. Kwa shabiki wa Spurs ambayo ina kikombe kimoja tu cha kombe la ligi kwa miaka 20 iliyopita ni aheri timu ishiriki kikombe kisicho na ushindani mkubwa na ikakibeba kuliko kwenda michuano migumu isiyoshindika kirahisi (assumption ni kwamba hawatafanya squad overhaul dirisha hili hivyo huenda wasiwe na kikosi kilichoshiba).
 
Oyaa kikundi kinginee cha Vibakaaa... wasalimieni Arsenal...Chelsea na taka taka zingineee salamu kutoka Man u
 
Ligi ndiyo hiyo imeisha na angalau tutacheza kombe ambalo Jose kasema kufuzu maana yake kulibeba tayari! Kacheza mara mbili na kalibeba mara hizo. Kwa maneno yake mwenyewe kasema siyo mbaya kushiriki kwa mara ya 3 na kulibeba kwa mara hiyo.

Siyo mbaya. Kipi bora? Kushiriki UCL na kuishia fainali au kushiriki UEL na kulibeba? Mafanikio hupimwa kwa vikombe na si idadi ya fainali ulizocheza.

Natarajia kutakuwa na sura mpya dirisha hili la msimu wa korona. Binafsi nadhani kuna maeneo yafuatayo yanahitaji uwekezaji.

1. CD. Hapa tuna Dier, Sanchez, Tanganga, Toby na Foyth. Super Jan anaondoka. Pia inaonesha kocha hajamkubali dogo Foyth. Eric Dier kasaini mkataba mpya kwa sharti la kucheza kama CB. Napendekeza anunuliwe CB mnyumbulifu wa kuimarisha safu ya ulinzi.

2. DM. Hapa tayari dogo Oliver Skipp kasaini mkataba wa kudumu mpaka 2024. Hata hivyo bado tunahitaji holding midfielder wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Wanyama/Dier. Hapa nadhani apatikane mkongwe wakati dogo Skipp anaendelezwa mdogo mdogo.

Kwenye DM's wanyumbulifu nadhani Sissoko angeuzwa tu. Nafasi yake ichukuliwe na Sergej Milinkovic Savic wa Lazio. Akawaongezee nguvu Ndombele, Gedson, Winks, na Lo Celso.

3. RW. Hapo Lamela atoswe tupate ingizo jipya umri na calibre ya Steven Bergwijn. Hivyo tutakuwa na Sonny/Bergwijn kwenye LW. RW tutakuwa na Moura na hilo ingizo jipya.

3. No. 10. Hapa kwenye namba 10 tunaye Lo Celso tayari ambaye kimsingi ndiye mbadala wa Eriksen. Wasiwasi wangu ni "The Dele Alli problem" kama anavyosemaga Mourinho. Dele hawezi mbenchi Lo Celso nyuma ya ST. Dele kukaa benchi kutapelekea chokochoko kutoka kwa English media. Ningekuwa Mourinho ningemuuza tu na pesa hiyo plus ile ya Lamela ningenunulia winger mzuri wa kulia.

4. FB. Suala la full backs liko wazi. Ssengnon hawezi kuwa full back karibuni. Anaweza zaidi kama wingback na Mourinho angependa full back. Hivyo ni ama auzwe Ben Davies au dogo C
Sess. Suala la kuleta mabeki wapya kulia na kushoto ni la lazima hslihitaji mjadala.

5. ST. Hapa itategemea na ikiwa Kane ataondoka au laa. Nimesikia tunamnyatia Zaniolo wa AS Roma japo kocha wao kakanusha.

Ngoja tusubiri tuone.
Sasa ni dhahiri tutakuwa na ingizo jipya golini. Hii ni baada ya Michael Vorm kuaga rasmi.
Screenshot_20200728-205918.jpg
 
Mdogo mdogo mpaka tutatoboa. Hapo wasiojua mpira bado utasikia "Ooh, Mourinho hapendi makinda". Sasa alianza dogo Skipp (holding midfielder) na sasa ni Japhet Tanganga. Huyu debut yake ilikuwa kwenye game na Looserpools na Mane na Mo Salah wanaifahamu vema kazi yake. Suka kikosi bwana Jowzey.

#COYS

 
Mdogo mdogo mpaka tutatoboa. Hapo wasiojua mpira bado utasikia "Ooh, Mourinho hapendi makinda". Sasa alianza dogo Skipp (holding midfielder) na sasa ni Japhet Tanganga. Huyu debut yake ilikuwa kwenye game na Looserpools na Mane na Mo Salah wanaifahamu vema kazi yake. Suka kikosi bwana Jowzey.

#COYS

Mourinho hata akiwa Man Utd aliwatumia vijana kama Jesse Lingard, Lindlof na hata alivyoanza kumchezesha McTominay mashabiki walikuja juu eti anachezesha watoto wasiojua mpira. Hivi kuna anayekumbuka ile namna ya Lingard ya kushangalia magoli iliishia wapi?
 
Mourinho hata akiwa Man Utd aliwatumia vijana kama Jesse Lingard, Lindlof na hata alivyoanza kumchezesha McTominay mashabiki walikuja juu eti anachezesha watoto wasiojua mpira. Hivi kuna anayekumbuka ile namna ya Lingard ya kushangalia magoli iliishia wapi?
Hui ni ukweli ambao mashabiki wengi hawana vifua vya kuuhimili. Jamaa alijibu vema hilo swali hivi karibuni. Kwamba ni kweli anapendelea kufanya kazi na wachezaji wenye umri mkubwa? Kajibu kwamba yeye hupendelea mchezaji mwenye ukomavu wa kiakili, haijalishi umri wake.

McTominay mwenye miaka 19/20 alikuwa kapevuka kiakili kuliko Pogba aliyejawa na kiburi. Alipolazimisha kumchezesha dogo kutupiwa kila aina ya tusi. Leo kila mmoja anajua shughuli ya dogo Scott.
 
Back
Top Bottom