Tottenham Hotspurs Thread

Shedafa

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
195

Waswahili husema "avumae baharini papa, kumbe wengi wapo". Msimu huu nasi tumo, hatujikongoji bali tumo!.

Tottenham Hotspurs F.C wengine upenda kufupisha kwa Tottenham au Spurs, Timu ya England inayopatikana Tottenham,Haringey,London ambayo inashiriki Premier League.

Wembley Stadium ndio uwanja wa nyumbani kwa Spurs msimu (2017-2018) wenye uwezo wa kuchukua watu 90,000, wakati uwanja wake wa nyumbani ukiwa kwenye matengenezo(White Hart Lane).

Kuzaliwa: 5 September 1882 (Hotspurs F.C)

Major honours
DomesticLeague competitions
Premier league: 2nd position(2016-2017)

First Division/Level 1:
Winners (2):
1950–51, 1960–61

Second Division/Level 2:
Winners (2):
1919–20, 1949–50

Cup competitions
FA Cup: Winners (8):

1900–01, 1920–21, 1960–61, 1961–62, 1966–67, 1980–81, 1981–82, 1990–91

League Cup: Winners (4):
1970–71, 1972–73, 1998–99, 2007–08

FA Charity Shield/FA Community Shield: Winners (7):
1921, 1951, 1961, 1962, 1967*, 1981*, 1991* (*shared)

European
UEFA Cup Winners' Cup: Winners (1):

1962–63

UEFA Cup/UEFA Europa League: Winners (2):
1971–72, 1983–84

Other honours/friendlies
Historical competitions

Southern League:[120]
Winners (1): 1899–1900

Western League:[120]
Winners (1): 1903–04

London League Premier Division Champions:
Winners (1):
1902–03

Football League South 'C' Division Champions:
Winners (1):
1939–40

Southern District Charity Cup: Winners (3):
1901–02, 1904–05, 1906–07

Sheriff of London Charity Shield: Winners (2):
1901–02, 1933–34

London Challenge Cup: Winners (8):
1910–11, 1928–29, 1936–37, 1947–48, 1958–59, 1963–64, 1970–71, 1973–74

Friendly tournaments
Anglo-Italian League Cup:
[129]
Winners (1): 1971

Costa Del Sol Tournament:
Winners (2):
1965, 1966

Nolia Cup: Winners (1): 1977

Kirin Cup: Winners (1): 1979

Sun International Challenge Trophy: Winners (1): 1983

Peace Cup: Winners (1): 2005

Vodacom Challenge: Winners (2): 2007, 2011

Feyenoord Jubileum Tournament: Winners (1): 2008

Barclays Asia Trophy: Winners (1): 2009

AIA Cup: Winners (1): 2015

Spurs Motto: To Dare is to Do
 
Eqlypz

Eqlypz

JF-Expert Member
May 24, 2009
4,065
0
Spurs wako kwenye dreamland, wakifungwa mechi mbili nguvu yote inaisha.
 
Shedafa

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
195
Nguvu haiwezi kuisha kwa kufungwa, kumbuka msimu uliopita tulizinduka wakati gani na hatukulala tena. Safari hii tumeanza mapema, ila kuna timu tukikutana nazo tunakuwa na mcheche. Sitazitaja ingawa nazijua, hapo tukipata hata droo tu itakuwa kama ushindi. Ila watu wakae sawa, tumeaziamia kutoa watu nishai hasa wale wenye mdomo mrefu.
 
Mbu

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,738
1,500
Waswahili husema "avumae baharini papa, kumbe wengi wapo". Msimu huu nasi tumo, hatujikongoji bali tumo!.
...kumbe mpo? safi sana. Msimu huu mtajitokeza wengi sana, Man City weshajipendekeza pia hapa, ...msikimbie tu!

Gunnerz 4Lyf!
 
Eqlypz

Eqlypz

JF-Expert Member
May 24, 2009
4,065
0
...kumbe mpo? safi sana. Msimu huu mtajitokeza wengi sana, Man City weshajipendekeza pia hapa, ...msikimbie tu!

Gunnerz 4Lyf!
Hahaha mtani waeleze hawa wanafikiria kushabikia timu zilizoko kwenye top four ni shughuli ndogo.
 
Shedafa

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
195
...kumbe mpo? safi sana. Msimu huu mtajitokeza wengi sana, Man City weshajipendekeza pia hapa, ...msikimbie tu!

Gunnerz 4Lyf!
Akimbiae si mwana michezo, tutanyong'onyea kwa simanzi tu. Tunajua mpira ni kufunga na kufungwa, unapofunga shangilia, kunjua moyo!. Ndivyo tufanyavyo, mambo yakigeuka unasikitika. Lakini atakayekaa sawa ni vidonge tu kwa sana!
 
..haya bana, yangu macho.

BTW, team yenu imewika kipindi fulani, enzi hizo Gaza, Linekar wanakichapa hapo, ...enzi za Klinsmann pia Spurs hamkuwa 'nyuma'. Mna matarajio gani mwaka huu?top ten, bottom ten au midtable?

Karibu tena...
 
Top ten wala si ya kuwekea malengo, tumekuwa humo mara nyingi. Kumbuka sisi ni moja ya timu chache (nafikiri hazizidi 5) ambazo hazijawahi kuikosa premier toka iwe premier. Matumaini yetu mwaka huu ni 4 bora, ni lazima tushushe kigogo kimoja. Ila naona kuna wanaotaka kuja na mbinu chafu, wanataka kutubomoa kama mwaka jana. Tumewapa Babatov na mwaka huu tena wanataka, hawaoni pengine!.
 
Eqlypz

Eqlypz

JF-Expert Member
May 24, 2009
4,065
0
Michael Carrick na million 10, hiyo deal nzuri mkikubali sasa hivi mnaweza kuleta replacement ya maana kabla ya msimu wa usajili haujaisha. Msisubirie yakaja kutokea ya mwaka jana, after all Spurs na Manchester United wanafanya biashara vizuri tuu.
 
Mwaka huu tunataka kucheza mpira sio biashara, kwani mkuu huwa hamuwaoni huko wanakotoka mpaka wafike Spurs?. Acheni na sisi tupate raha jamani!
 
Mvina

Mvina

JF-Expert Member
Aug 2, 2009
999
1,225
Waswahili husema "avumae baharini papa, kumbe wengi wapo". Msimu huu nasi tumo, hatujikongoji bali tumo!.
Tangu lini mzee mtoto akalala na hela wakati baba,mama,kaka na dada wapo! Zaidi ataishia kulala na mikojo tu na mkojo wenyewe ni wa saa 11 asubuhi.
Sasa hv nappy bado hazijaloana zikiloana tu!
:rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes:
 
Shedafa

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
195
Na zile nepi zilizoanza kuloana nazo, zitakauka?, we subiri uone. Labda jamaa wafanikiwwe mbinu zao chafu za nje ya uwanja, siku zote hawakumuona Modric kuwa mzuri ndio wanamuona sasa.
 
Jile79

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
13,836
2,000
ziacheni timu ndogo zipande juu kwani ufalme wa ligi kuu ni wao.........
Waswahili husema "avumae baharini papa, kumbe wengi wapo". Msimu huu nasi tumo, hatujikongoji bali tumo!.
 
K

Konaball

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
2,864
2,000
mkuu ustie shaka ata kama ataondoka hakuna taabu, angalia hii:

Spurs are in talks with Internacional over £15m-rated Brazil midfielder Sandro, while also exploring a loan deal for Le Havre midfielder Kevin Anin and Dinamo Zagreb striker Mario Mandzukic
 
MduduWashawasha

MduduWashawasha

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
1,652
2,000
mpira wa uingereza ni kama upepo.kuna kipindi timu inakuwa juu then inashuka kutokana na masuala mbalimbali.nitakuja na link baadae inayotoa historia ya ligi ya uingereza toka ilipoanzishwa.kwa msiojua spurs ya mika ya 80 ilikuwa kama ilivyo chelsea labda manake kipindi hicho liver ndo alikuwa mtawala wa ligi .man u ilikuwa kama wigan ya sasa
 
Manda

Manda

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
2,075
1,225
...kumbe mpo? safi sana. Msimu huu mtajitokeza wengi sana, Man City weshajipendekeza pia hapa, ...msikimbie tu!

Gunnerz 4Lyf!
Kwa taarifa yako ''sisi Totenham" tumekuja chukua nafasi yenu, nyi ni mabakhili banaaa....
 
Shedafa

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
195
mkuu ustie shaka ata kama ataondoka hakuna taabu, angalia hii:

Spurs are in talks with Internacional over £15m-rated Brazil midfielder Sandro, while also exploring a loan deal for Le Havre midfielder Kevin Anin and Dinamo Zagreb striker Mario Mandzukic
Asante mkuu kwa taarifa, umenifanya nijisikie raha sana.
 
Mbu

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,738
1,500
Kwa taarifa yako ''sisi Totenham" tumekuja chukua nafasi yenu, nyi ni mabakhili banaaa....
...khaaa, kumbe nawe ni Spurs? haya bana, nami nasubiria nepi zenu zikishaanza kulowana, :D:D:D mtashuka tu nyie wala siku si nyingi...
 
Shedafa

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
195
...khaaa, kumbe nawe ni Spurs? haya bana, nami nasubiria nepi zenu zikishaanza kulowana, :D:D:D mtashuka tu nyie wala siku si nyingi...
Kwa taarifa yako tu, wakati wewe una 3 dhidi ya Celtic. Sisi tushambamiza mtu 5 na mpira unaendelea. We kaa na msemo wa kizamani "aliyejuu mngoje chini", mfuate huko huko!
 
Top Bottom