Total shutdown MOI hakuna huduma

uongozi ni busara, uongozi ni maono, uongozi ni upevu wa fikra, uongozi ni maono, uongozi kamwe hauwezi kuwa nguvu!ffu, police mnajisikiaje kutumika kama remote!hamuwazi, hamfikirii, hampambanui!ama kweli igeni wenzenu wa misri, yemen na tunisia
 
JackBauer taratibu....kuna m'bibi mmoja humu JF ataanza hedhi sasa hivi wakati ni post-menopause tangu loongi!

Wako ma'bibi wawili wameamua kuitetea serikali utadhani wanalala na vigogo
 
Madaktari wakishinda vita vyao na serikali na walimu nao nahisi watajipanga upya manake wao huwa hawafani kiwagi
 
Lakini hebu tuone,mwanansiasa anawezaje alipwe pesa nyingi na posho llukuki kuliko mtaalam hasa dr wa binadamu? Wanaongeza posho,mfuko wa jimbo una kazi gani kwa mbunge? Maisha yanwezaje kuwa magumu kwa wanasiasa tu huku wakiacha walimu,maaskari,ma dr.? Serikali sikivu,sikivu wapi,sikio la kufa.Hapa TISS,FFU,POLICE wapo kazini hawalali ucku na mchana huku wakiingiza per diem zao ingali wazazina ndugu zao wakiumia.
Anyway,hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha,yataisha tu.
 
uongozi ni busara, uongozi ni maono, uongozi ni upevu wa fikra, uongozi ni maono, uongozi kamwe hauwezi kuwa nguvu!ffu, police mnajisikiaje kutumika kama remote!hamuwazi, hamfikirii, hampambanui!ama kweli igeni wenzenu wa misri, yemen na tunisia

Mkuu, yote hayo ya nini! Hebu fikiria endapo jamaa wakiamua kuonekana wapo kazini halafu hawafanyi kazi. Hao ffu watafanya nini? Pinda atafanya nini? Mimi naona mgomo baridi una impact kubwa kuliko kuliko kitu chochote. Wao si wataangalia daftari la mahudhurio tu.

Jana PM alisema watafutwe madaktari kutoka sehemu mbalimbali wakatibu, hivi anajua impact yake? Fikiria daktari aliyemaliza degree yake miaka kumi na zaidi iliyopita halafu hakufanya kazi hospitalini (aliwekwa pale wizarani), leo hii tuaminishwe kwamba akatibu watu, hili si bomu?! Tujiulize, kwa kipindi cha miaka kumi, tumebadili dawa za malaria mara ngapi? Au, kabla ya kuanza kutibu watapata fresher couse. Lakini pia, hivi tuna wanajeshi wangapi maMD jamani? Au labda mkuu alimanisha madaktari wa sampuli gani.

Kwa mtazamo wangu, naona kuna mabaya zaidi yanafuata.......
 
Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wametumia zaidi ya BILIONI 64 halafu pesa ya kuwalipa madaktari hawana hivi hii serikali yetu ina fikiria kwa kutumia akili ama vigole gumba vya miguu....

Heri wafukuzwe serikalini watafungua hospital zao binafsi wanaheshimika
 
Back
Top Bottom