ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Entered service: 1997
Diving depth : 480m
Torpedo tubes: 8×660-mm
Weapons: Mk-48 torpedoes,Sub-Harpoon anti-ship missiles and Tomahawk cruise missiles
Seawolf class inaelezwa kwamba ndio submarine yenye teknolojia ya hali ya juu duniani lakini pia ndio submarine ghali zaid duniani.Zilitengenezwa kwa ajili ya kutafuta na kuzishambulia submarines za kisoviet km vile Akula na zile za kurushia makombora ya balistiki kama vile Typhoon class.
Jumla ya Submarine 12 za aina hii zilitarajiwa kutengenezwa lakin kutokana na gharama zilitengenezwa 3 tu ambazo zinafanya kaz kwenye jeshi la Marekani.
Seawolf class inaarifiwa kwamba ndo submarine kimya sana(quietest submarine) kuwahi kutengenezwa duniani.Ikiarifiwa kwamba ni kimya sana hata pale inapokimbia kwa spidi kubwa.Inaarifiwa kwamba submarine nyingi hulazimika kupunguza/kutembea kwa speed ya 5knots ili kukwepa kuonekana/kugundulika na Passive sonar arrays(kiswahili chake sijui ila nahisi itakua kwenye kundi la Sound) lakini Seawolf inaweza kwenda hadi 20knots bila kugundulika na hizo Passive solar arrays.
Submarine hizi zinaweza kuzama kwenye kina kirefu zaidi kuliko submarine nyingi zilizo ndani ya jeshi la Marekani pia ina uwezo wa kusafiri kwenye maeneo yenye barafu.
Entered service: 2004
Diving depth: Over 250m
Vertical launched tubes: 12
Torpedo tubes: 4×533-mm
Weapons: Mk-48 torpedoes, Harpoon ant ship missiles, Tomahawk cruise missiles.
Hii ilitengenezwa kama mrithi wa Los Angeles Class sub.Ilibuniwa kua ndogo kiumbo pia kuendeshwa kwa bei nafuu zaid. Jumla ya submarine 30 zimepangwa kutengenezwa.
Inaarifiwa kwamba submarine hizi zimebuniwa na kutengenezwa kwa materials mbalimbali ili kuisaidia kutokuonekana kirahisi kwenye mitambo ya adui na pia kua na Low acoustic signature(inaendana na stealth kwa kiasi ila sijapata kiswahili chake fasaha).Inaarifiwa kwamba ukimya wa submarine hizi unaendana/kulingana na ule wa Seawolf class sub.
Pia submarine hizi zinaweza kutumika kwa operations maalumu ikiwemo ya kupeleka na kurudisha Navy Seal nyumbani.
Entered service: 2010
Diving depth: over 150m
Torpedo tubes: 6×533-mm
Weapons: spearfish torpodes, Harpoon, Tomahawk.
Ilianza kazi ndani ya jeshi la Uingereza mwaka 2010.Jumla ya submarine 7 za aina hii zimepangwa kutengenezwa. Hizi zitachukua nafasi ya Swiftsure class attack submarines ambazo zinatarajia kupumzishwa.
Submarine hizi inaarifiwa kwamba ni stealth pia zinabeba silaha nyingi na nzito kuliko nyingine ndani ya jeshi la Uingereza.
Entered service; 2013
Diving depth: ~300m
Vertical launch tubes:24
Torpedo tubes: 8×650mm
Weapons : various torpedoes, ant ship ,cruise missiles.
Ilianza kaz ndani ya jeshi la Urusi mwaka 2013 ikitarajiwa kua mrithi wa Akula Class sub.Jumla ya subs hiz 6 zimepangwa kutengenezwa.
Inaarifiwa kwamba Graney class subs ni kimya sana kushinda Akula Class subs hivyo ni ngumu kuonekana na adui.
Entered service: 1992
Diving depth : 400m
Torpedo tubes: 4×650-mm, 4×533-mm
Weapons:Torpedoes, SS-N-Starfish or SS-N-16 Stallion ant sub missiles, SS-N-21 Samson cruise missiles
Inaarifiwa kwamba hiz ni moja kati ya subs hatari na pia za gharama ndani ya jeshi la Urusi. Inaarifiwa kwamba ina uwezo wa kuzama kina kirefu pia na speed kubwa.
Licha ya kua na gharama sana katika uendeshaji wake lakini jeshi la Urusi bado linaendelea kua na hizi subs hii ni kutokana na faida zake ikiwemo kuzama kwenye kina kirefu cha bahari hivyo kufanya uonekani wake kua mgumu.
Entered service: 1988
Diving depth: 450m
Torpedo tubes: 4×533-mm
Weapons: Mk-48 torpedoes, Harpoon, Tomahawk.
Ilianza kazi mwaka 1988.Jeshi la Marekani linamiliki sub hizi 40.
Ni kimya sana pia ina uwezo wa kuzama kwenye kina kirefu hii kufanya kua ngumu kuonekana au kushambuliwa na adui.Pia ina uwezo wa kutembea kwenye sehemu za barafu.
Entered service: 1986
Diving depth: ~300m
Torpedo tubes: 4×650mm, 4×533mm
Weapons : Torpedoes and missiles
Hii ilikua ni pasua kichwa kwa nchi za magharibi kipindi hcho kutokana na kua uwezo wa kutembea kimya sana kuliko subs nyingi za magharibi(hasa US) kipindi hicho hvyo kuifanya kua ngumu kuonekana na mifumo ulinzi ya aadui.
Entered service: 2009
Diving depth: ~250
Torpedo tubes: 6×533-mm
Weapons: Type 89 torpedoes,Harpoon anti ship missiles.
Ilianza kaz ndani ya jeshi la Japan mwaka 2009.Tofauti ya subs hizi na nyinginezo ndani ya jeshi la Japan ni kwamba hizi hutumia Diesel(diesel-electric-propulsion)ili kuziendesha na sio nishati ya nuclear.Submarine hizi zimefungwa mfumo maalum na wa kipekee uitwao Air-independent-propulsion-system. Japan ndo nchi ya pekee kutumia mfumo huu.
Mfumo huu unasaidia submarine hizi kukaa mda mrefu kidogo bila kuibuka nje kuja kuchajiwa.Mfumo huu umeongeza mda wa submarine hiz kukaa ndani ya maji toka siku kashaa mpaka wiki kadhaa.Pia inasaidia submarine kua ngumu kuonekana na mifumo ulinzi ya adui(stealth).
Udhaifu wa subs hiz ni kwamba hazina uwezo wa kubeba mzigo mkubwa wa silaha kama zile zinazoendeshwa na Nuclear.
Entered service: 2006
Diving depth: 300m
Vertical launch tubes: 24(154)
Torpedo tubes: 4×533-mm
Weapons: Mk-48 torpedo, Harpoon anti ship, Tomahawk.
Hizi zilitengenezwa maalumu kabisa kwa ajili ya kubeba makombora mazito ya masafa marefu(ICBM) hata hivyo kuanzia mwaka 2002-2008 Jeshi la Marekani ilibadili submarine 4 za aina hii maalumu kwa kubeba makombora ya Cruise kama vile, Tomahawk,nk.
Submarine hii ina uwezo wa kubeba makombora hadi 154 ya Tomahawk.
Hizi ndo submarine zinazobeba yale makombora ya Trident.
Entered service: 1986
Diving depth: 500m
Missile tubes: 24
Torpedo tubes: 2×650mm, 4×533mm
Weapons: torpedoes, ant ship missiles, Cruise missiles.
Ni submarine za tatu kwa ukubwa duniani ukiacha Typhoon(Russia) na Ohio class (USA).
Zilitengenezwa 11 huku 4 zikiwa bado zinafanya kaz ndani ya jeshi la Urusi mpaka Leo.
Inaarifiwa kwamba subs hizi zina uwezo mkubwa sana wa kujificha kutokuonekana na adui (very stealth) na zilitengenezwa pia kwa ajili ya kushambulia aicraft carriers za Marekani.
Submarine hizi pia zina uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia.
nankumene Dotworld Elungata Mount Kibo MTOTO WA KUKU mohamedidrisa789 izzo Root Chenchele
Wakuu mtanisamehe kuchanganya kiswaGlish maaana maneno mengine ya kitaalum siyajui kiswahili. Pia sorry abt Inaarifiwa kwamba ila natumaini mmeleewa.