Top 10 destroyers

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,417
9,603
2dff331ea84b00bc7cd88535689194af.jpg
Nr.1 Zumwalt Class (USA)

Hizi meli vita mpya kabisa ndani ya jeshi la Maji la Marekani,zilikabidhiwa rasmi kwa jeshi hilo mwaka 2016.
Zumwalt class imetengenezwa na kampuni ya General Dynamics Company kama mkandarasi mkuu ikishirikiana na Lockeed Martin,BAE na Boeing.
General Dynamics ilihusika kwenye kubuni na kuifanyia majaribio,Lockeed Martin na Boeing zilihusika kuweka na kudesign mifumo ya umeme na programu mbalimbali(software's).Meli hii pia inatumia mfumo mpya kabisa wa DDG 1000 system ambao ni mpya na wa kisasa wenye teknolojia ya hali ya juu kabisa uliobuniwa na Norhrop Grumman watengenezaji wa ndege ya B-2 spirit stealth bomber ambao unaiwezesha Zumwalt kua na advanced gun system, integrated power system, composite deckhouse, peripheral vertical launch system,integrated sonar system (with advanced towed array and high frequency active sonar) na dual band radars(passive and active).
Muunganiko wa mifumo yote hii inaifanya meli hii kua ni ya hatari sana mfano. Mfumo wa vertical launch system unaifanya kuweza kulaunch makombora mengi kwa mda mfupi zaidi(mfano kombora moja la Tomahawk kwa kila baada ya sekunde 15-30),mifumo ya kisasa ya sonar kwa ajili ya kudetect nyambizi(submarine) za kisasa,radar za kisasa kwa ajili ya kudetect makombora kwa umbali mrefu zaidi pia ndege, drones,nk pia mifumo mingine kwa ajili ya kuifanya iwe na kasi sana (speed) hata kwenye mawimbi makubwa.
Zumwalt inaweza kuitwa baba wa railguns kutokana na kua na railguns za kisasa na hatari zaidi zenye uwezo wa kufika hadi umbali wa 180km.
Pia meli vita hii ina uoni hafifu kwa rada za adui (stealth), licha ya ukubwa wake lakini inaweza kuonekana kama meli ndogo za uvuvi kama ikiwa karibu sana na rada ya adui.
Kutokana na gharama kubwa za utengenezaji wake jeshi la Marekani litatengeneza meli hizi tatu tu badala ya 32 zilizotakiwa hapo awali.


11cadbff7d05ae6d63a7e3360b2a8553.jpg
Nr.2 Sejong the Great Class(South Korea)

Hizi ni moja ya meli vita aina ya destroyer hatari zaidi duniani, ilitengenezwa chini ya mpango ulioitwa KDX-III program.Lengo la mpango huo ilikua ni kuipatia Korea kusini meli vita ya kisasa ambayo itakidhi mahitaji kwa kitisho chochote majini,ardhini na hata angani.
Meli hii inafanana sana na ile ya Arleigh Burke ya Marekani na Atago Class ya Japan hii ni kutokana na kutengenezwa na vifaa na mifumo inayokaribia kufanana.
Meli hii ina mifumo ya kisasa kabisa ikiwemo ya radar(AEGIS) ambayo ina uwezo wa kudect kwa pamoja zaidi ya 100 targets.
Pia ina silaha nyingi nzito na za kisasa kama vile makombora ya kuharibu meli(Hyunmoo III ant ship missile),makombora ya cruise (Hyunmoo IIIB) yenye range zaid ya 1000km, SSM-700K Haeseong ant ship missile yenye range zaid ya 150,makombora ya kuharibu nyambizi(submarines) -Red shark missiles, torpedoes, nk.
Pia ina sehemu ya kubebea helicopter mbili.

423f28bfdb532757d1cda7be050e7d81.jpg
Nr.3 Arleigh Burke class (USA)

Kwa sasa ndio destroyer kubwa kabisa ndani ya jeshi la majini la Marekani.Pia ni moja ya destroyer kubwa kabisa duniani ikisheheni mifumo ya kisasa kabisa pamoja na silaha kali.
Destroyer hizi zilianza kazi mnamo mwaka 1991 ambapo zilkua meli vita kubwa ndani ya jeshi la majini la Marekani zilizobuniwa kwa mtindo unaoisaidia kutoonekana kirahisi na rada za adui(Low radar Cross section).
Meli vita hii ina mfumo wa ulinzi wa AEGIS kwa ajili ya kudetect vitisho vya majini, ardhini na pia angani,Phalanx Closed In Weapon system na mashambulizi kama vile Tomahawk, ASROC ant sub missile,torpedoes, etc.
Meli vita hii ina mifumo mingine mbalimbali kama vile SPY-1D na Mark 99 kwa ajili ya kuelekeza silaha (missile) kwenye target kama vile ndege au kombora la adui kwa umbali mrefu.Pia mfumo huu unaweza kudetect mamia ya targets kwa wakati mmoja kama vile ndege, nyambizi, drones, kombora, ICBMs, nk yakiwa umbali mrefu toka ilipo. Rada zake zinaona pande zooote yaani 360° bila kusahau silaha aina ya gun(127mm) kwa ajili ya mashambulizi dhidi ya meli nyingine.
Mpaka sasa meli vita hizi jumla zipo 62 zikiwa kwenye matoleo matatu tofauti yajulikanayo kama vile Flight I, Flight II na Flight IIA. Hizi za Flight IIA wakati mwingine hujulikana kama Austin class. Hizi huwa sehemu maalumu kwa ajili ya kubebea helicopter.

63fddec54c898a2880180b617023b1a9.jpg
Nr.4 Type 052D class(China)

Kwa wamagharibi inafahamika kama Luyang III class ikiwa ni muendelezo wa Luyang II class (Type 052C).
Meli vita hii ni kubwa kimaumbile lakini inaelezwa kua na uoni hafifu kwa rada za adui(Low radar cross section).Pia meli vita hizi zinabeba silaha nyingi na za hatari.
Meli hii ina radar mpya zilizoundwa mwaka 2012 ambayo inaatajwa kua sawa na ile ya Marekani Aegis SPY-1 ikiwa na uwezo wa kudetect vitisho mbalimbali majini,ardhini na angani.
Mifumo yake ya ulinzi ni pamoja na HHQ-10 ambayo ina makombora ya masafa mafupi pia 30mm Closed In Weapon System (CIWS) ambapo inaelezwa kua na uwezo wa kurusha roundi 10000 kwa dakika moja ikidaiwa kuweza kuharibu makombora ya kushambulia meli(ant ship missiles) kwa kiwango cha 96% kwa speed ya Mach 4.
Destroyer hizi pia zina 130mm gun, makombora ya kuharibu nyambizi, torpedoes, nk.
Pia zina uwezo wa kubeba helicopter.


6ae4f54b6dce2e72d20a68a97a4001ca.jpg
Nr.5 Kolkata class (India)

Japokua Kolkata class kuelezwa kutokua na mifumo ya kisasa kama inayopatikana kwenye vyombo vya magharibi au wachina lakini inatajwa kua na uwezo wa kiasi chake.
Meli vita hii ina mifumo,silaha na vifaa mchanganyiko ikiwemo vya magharibi na ile ya Urusi.
Mifumo ya kujilinda ni pamoja na Barak 8 air defence system uliotengenezwa kwa ushirikiano na Israel, 76mm gun na AK-630 CIWS.Ile ya mashambulizi ni pamoja na makombora ya Brahmos yaliyotengenezwa kwa ushirikiano na Urusi, torpedoes, nk.
Pia zina uwezo wa kubeba helicopter.


fd3b0b61cdaca90b493571eeff864ccd.jpg
Nr.6 Atago class(Japan)

Hizi ni destroyer kubwa kabisa ndani ya jeshi la majini la Japan zikiwa na uwezo mkubwa wa kujilinda au kulinda anga(strong ant-air warfare capability) .
Meli vita hii imefungwa mfumo wa Aegis ambao ni wa kisasa na hatari zaidi duniani.Jambo lingine juu ya meli vita hii ni kwamba imejumuisha mifumo, silaha, radars zilizotengenezwa pande mbili tofauti Marekani na Japan. Inaelezwa mifumo hii yote imeunganishwa vizuri ili kuongeza ufanisi wake.
Kazi kubwa ya meli vita hii ni dhidi ya vitisho vya anga ikiwemo uwezo dhidi ya makombora ya ballistic ikijumuisha mifumo ya kisasa kama vile SM-2MR,SM-3 ant ballistic missiles(2500km range),20mm Phalanx CIWS,Mk 41 VLS. Pia ile ya mashambulizi kama vile RUM-139 ASROC missiles, Tomahawk, Harpoon anti ship, SSM-1B anti ship(150km range) ,torpedoes,nk.
Inaelezwa kwamba meli vita hii ina mifumo mingi ya kujilinda kuliko ile ya mashambulizi(tunaweza kusema ya mashambulizi no hafifu kulinganisha na ya kujilinda).


8fa43d0daab0145619790d0b2f0467cc.jpg
Nr.7 Kongou class (Japan)

Kwa kipindi cha miongo minne iliyopita kitu cha kwanza ambacho jeshi la majini la Japan ilitilia mkazo ni anga na dhidi ya nyambizi (submarine).Kuongezeka kwa kitisho cha Uchina na upungufu wa shughuli za kijeshi za Marekani katika eneo la Asia kwenye miaka ya 1980 na 1980 iliifanya Japan kutilia mkazo ukuaji na uwepo wa jeshi lake la majini.
Kongous class ina mifumo ya hali ya juu ya ulinzi na ile ya mashambulizi. Pia ni moja ya destroyers kubwa kabisa duniani ikiwa na ukubwa kukaribiana na cruisers.
Meli vita hii ina silaha, rada pamoja na mifumo mingine ya kisasa yenye ufanisi mkubwa.
Kazi kubwa ya meli vita hizi ni dhidi ya ulinzi wa anga ikiwa na mifumo ya masafa marefu ya kulinda na kuharibu kitisho chochote kile kwa umbali mrefu.
Mifumo ya ulinzi ni pamoja na SM-2MR(SAM),Mk 41 VLS, 20mm Phalanx CIWS(dhidi ya anti ship missiles).Ile ya mashambulizi ni pamoja na makombora ya Harpoon(anti ship), nk.


36d2f4c13e4ba8cc3ae5f634b94b54f1.jpg
Nr.8 Aikizuki class (Japan)

Lengo kuu la utengenezwaji wa destroyer hizi ni kwa ajili ya kuzisindikiza meli maalumu za kubebea helicopter (helicopter carrier) za Hyuga na Izumo class kwa ajili ya kuzilinda.
Meli vita hizi pia zinatajwa kua na rada cross ndogo kwa hivyo kutoonekana kirahisi na rada za adui. Pia ina mfumo maalum uliotengenezwa na Japan wenye kufanana na ule wa Aegis uitwao ATECS battle management system.
Ina mifumo mbalimbali ya ulinzi kama Sea sparrow(SAM), ASROC(anti submarine) ,127mm gun, 20mm phalanx CIWS, nk pamoja na ile ya mashambulizi km vile Harpoon missiles (ant ship),torpedoes, SH-60K ant submarine, nk.
Inaarifiwa kwamba baadhi ya mifumo iliyopo kwenye meli hii inafanana na ile inayopatikana kwenye Zumwalt class.


8477c704d52b0c224dd2b6888e80ff10.jpg
Nr.9 Daring class( United kingdom)

Destroyer hii ni zao la mradi uliojulikana kama Project Horizon uliohusisha pia Ufaransa na Italy japo baadae Uingereza iliamua kujitoa kwenye mradi huo. Lengo kuu la utengenezwaji wa meli vita hii ni kuipatia uwezo Uingereza kuweza kufanya doria katika eneo kubwa na pia kulinda anga.
Zilianza kazi mwaka 2009 huku nyingine 6 zikikabidhiwa mwaka 2013.Hizi ni meli vita kubwa kabisa kwenye jeshi la majini la Uingereza tangu vita kuu vya pili vya dunia.Pia ni meli vita zenye teknolojia ya juu kabisa ndani ya jeshi la majini la Uingereza.
Jukumu kuu la hii meli ni ulinzi dhidi ya anga ikijumuisha mifumo kama vile PAAMS(SAM),nk. Mifumo mingine ya ulinzi ni pamoja na torpedoes, nk.
Meli hii ina rada zenye nguvu na za teknolojiabya hali ya juu inayofanya kazi ya kudetect vitisho mbalimbali pia kuelekeza mashambulizi ya silaha mahala husika na kuunganisha silaha na vifaa vingine na mawasiliano ya satellites.


76d2519f51417ce6e2804581231e88f9.jpg
Nr.10 Horizon class (France/Italy)

Ni zao la mradi uliojulikana kama Project Horizon ulioanza mwaka 1992.Lengo kuu la mradi huu ilikua ni kutengeneza meli vita ndogo ambazo zingeweza kufanya doria kwenye maeneo ya Mediterranean jambo lililofanya Uingereza kujiondoa kwenye mradi huo kutokana na kuhitaji meli kubwa yenye kuweza kufanya doria kwenye maeneo makubwa kama vile yale ya Atlantic.
Meli vita hii ina rada za kisasa kwa ajili ya kudetect na kusaidia silaha kupiga mahali husika.
Upande wa anga ina makombora ya Asters(range 120km)
Ulinzi dhidi ya meli nyingine ina makombora ya Exocet (French made), OTOMAT Teseo(Italian made)-180km range.
Pia ina mifumo mingine ya ulinzi na mashambulizi ikiwemo torpedoes, nk.
Meli hii ina uwezo wa kubeba helicopter.


Ps; Uzi Umerudi.

izzo MTOTO WA KUKU Elungata Nalendwa The bold nankumene
 
Nilianza kujua tu huwezi kuzipata data za jeshi la K.Kaskazini

Juzi tulituma ferry Russian.....

Ndege za China zaizuia ndege ya Marekani...
Kwan hao Korea ukiacha hzo nuclear wana nn cha ajabu?!, maaana ht ndege wanazotumia ni za 1950's.Submarines zao za zaman mpk huwa zinapotea zenyewe baharini.

Hyo issue ya China na Marekani mbn sio ngeni.. Ni ya miaka na miaka... Km Marekani anapeleka meli karibu na Urusi(black sea) sembuse hpo China (south China sea)...
 
Kwan hao Korea ukiacha hzo nuclear wana nn cha ajabu?!, maaana ht ndege wanazotumia ni za 1950's.Submarines zao za zaman mpk huwa zinapotea zenyewe baharini.

Hyo issue ya China na Marekani mbn sio ngeni.. Ni ya miaka na miaka... Km Marekani anapeleka meli karibu na Urusi(black sea) sembuse hpo China (south China sea)...
Mpaka zinapotea zenyewe baharini!
 
Uzi na details sambamba, saante!, huwa natamani kuyajua vizuri haya ma enormous vessles.
Mrusi ana miss hapa lakini Mhindi yupo. Hawa watu huwa hawabaki nyuma.
 
Back
Top Bottom