Tongotongo,Kwikwi Za Uongozi Mbovu

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,172
1,074
Sijui wanajisikiaje waliokuwa viongozi nyakati zile wakati vilele vya uovu,matumizi mabaya ya madaraka,utaperi wa kisiasa,teuzi zenye ukakasi,Utendaji mbovu wa wateuliwa,kulega lega kwa maamuzi yenye tija kwa taifa..

Roho zinawauma,nafsi zimepondeka,mioyo imebaki uchi kwa hatua kali zinazochukuliwa dhidi ya makuwadi na watuhumiwa wazandiki wa ufisadi na udebwedo kiutendaji..hakika nuru ya maendeleo kwa ambao hawakustahiri kuila keki ya nchi yachomoza..walio wengi walibezwa kwa manufaa ya wachache,walinyanyaswa,waliogopeshwa,waliibiwa haki zao,walinyonywa {kupitia kodi,ushuru}...

Tunayo mengi ya kujifunza tunapopewa dhamana ya kuongoza taifa tajiri lenye wimbi la maskini..Yatupasa kujikana nafsi zetu,kuwakana marafiki zetu,kuwakana wapendwa wetu ,kuikana harufu ya ukwasi,na kuepuka ubwanyenye...Maisha ya uongozi ni kujitoa sadaka dhidi ya wale wanaoongozwa..

Ni mwiko kuwa na Uongozi wa kunufaika binafsi,Uongozi wa kujitajirisha,Kutajirisha watoto,kunufaishwa kimadaraka,kunufaisha wapenzi wa dada zetu,kunufaisha marafiki,kunufaisha chama,kunufaisha wafadhiri,kunufaisha wakoloni mamboleo,kunufaisha wanadini,kunufaisha washikaji,kunufaisha wa kwetu.....

Mungu Ibariki Afrika,Mungu wabariki na kuwalinda viongozi wenye kupigania maslahi ya wanyongwe,wanyonywaji,maskini,malofa....
 
Back
Top Bottom