VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,492
- 1,466
Uwanja wa ndege wa Nzibira, huko Kivu kusini, uliopo katika eneo lililokuwa likilindwa na Wazalendo kushilikiana na jeshi la Burundi, jana tarehe 10 August, ulibaki mikononi mwa M23 baada ya waliokuwa wanatwaa eneo hilo kuzidiwa nguvu na waasi hao. Baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea huko Doha kutoendelea, kutokana na serikali ya DRC kughaili kuachia huru wafungwa wa M23, huku ombi la serikali la kuachia huru wanajeshi wake waliokuwa mjini Goma lenyewe likitekelezwa, vita vimekuwa vikiendelea katika Kivu zote mbili(Kusini na Kasikazini), huku M23 ikizidi FARDC, Wazalendo, Mercenalies na jeshi la Burundi nguvu na kujiongezea ukubwa wa maeneo inayotawala kwa sasa.