Tom Clancy Without remorse 2021

Tom Clancy Without remorse 2021

Yako Atta

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2016
Posts
288
Reaction score
467
Tom Clancy.2021.WITHOUT REMORSE

Je, Nadharia zilizotumika zinaakisi uhalisia wa Mambo?


"You know who won WW II?"

"It wasn't the Generals or the Admirals."

"It was the Economists."

"More tanks, planes, ships."

"And all that spending lifted this entire nation out of poverty."

"Freed the world from Tyranny."

"A big Country needs big Enemies."

"The best enemy we ever had was the Soviet Union."

"Our fear of them unified our people."

"Gave us purpose."

"The problem today , John, is half of this country thinks the other half is its enemy, because they have no one else to fight."

"So we gaive them a real enemy."

"One with the power to threaten their lives, their freedoms."

"Freedom you take for granted."

"And It works John, It works."


Maneno ya US Secretary of Defence Thomas Clay akimwambia Senior Chief John Kelly baada ya failed False flag mission in Russia iliyomfanya mwamba aende kwa lengo la kulipiza kisas kumbe kila kitu kimepikwa na CIA kwa lengo la kutafuta sababu ya kuingia vitani na Russia.

Sasa katka harakat za kutafuta nini kilichopo nyuma ya pazia cha team mates wake wote walioshiriki mission ya awali ya Allepo kuuwawa mmoja baada ya mwingine hata yey kuponea chupu chupu licha ya mkewe mjamzito kuuwawa jumlisha na fake mission nyingine ya kwenda Russia kumkamata Rykov (mdaiwa wa mauaji ya Allepo Mission X Commandos pamoja na mke wa John Kelly bibie Pam Kelly). Baada ya kufumbuliwa maskio na Rykov mwenyewe kabla hajajilipua, mwamba ndo akaamua kurudi kuusaka ukweli kwa kumteka Wazir wa Ulinzi na kumtishia kuiangamiza familia yake, katika kumhoji Secretary wakiwa ndani ya gari ndo akapewa majibu hayo hapo juu.

Movie: Tom Clancy.Without Remorse.2021.

Je,Majibu hayo ya kweny movie yanaakisi ile kauli aliyowahi kunukuliwa George Bush Jr. Katka harakat zake za kumsaka Osama Kuwa America inahitaji Adui mwenye nguvu?

Nature ya mwanadamu sio kurelax, Asili ya mwanadamu ni uasi na mapambano ya namna gani atashinda na kusonga mbele (Survival of the Fittest is Real)
Mwanadamu akikosa upande wa kupambana nao ataanza kupambana na nafsi yake au vyeny kunasibika naye ili aweze kupata natural pace ya kuweza kusonga mbele. Yaan Kwa kifupi akili ya mwanadamu haifanyi kazi kwa ufanisi wa juu kama hakuna changamoto ya kutatua.

Vision ya Mwalimu Nyerere kuwa UPINZANI weny nguvu nchi hii utatokana na CCM, vision ile iliegema katka nadharia hii ya kifikra. Ishara kuu juu ya hili ilikuwa n G55. Na mwenendo wa siasa za Hayati Magufuli, naamin kwa siku za usoni zingetufikisha kule kwa G55. Kile alichotabiri Mwalimu Nyerere ndo itakuwa zama yabutukufu wetu?

Mikhail Gorbachev aliwah kusema kuwa Vita siku zote n matokeo ya kufeli kwa sera. Uimara wa sera za America automatic uliifanya USSR kuwa na ukomavu mkubwa wa kisera jambo ambalo US Deep State walilihitaji mno. Ni katka kipindi hiki Kulikuwa na kile kilichojulikana kama Cold War, matokeo ya Cold War yatendelea kubaki na kuhesabiwa kama moja ya mageuzi makubwa ya sayansi na kiteknolojia yaliyowahi kufanywa katika historia ya mwanadamu.

Palipo na Changamoto ndo huchangamsha akili ya mwandamu timamu(The fittest one).

Changamoto ya uwepo wa USSR ilitokeza mshikamano baina ya waamerika na bongo zao kufanya kazi isivyo mithilika vile vile kwa USSR.

Tishio la kufeli kwa Sera za USSR zilizohatarisha amani ya Dunia hata zilizopelekea Kumpandikiza Mikhail Gorbachev na Petrstraika yake, haikuwa tu ushindi kwa America bali ishara ya kwisha kwa zama na ugumu wa kifikra wa mwanzo wa zama mpya za jinsi ya kuuendesha ulimwengu.

Jaribio la kuunda na kufadhili makundi ya kigaidi bado halikufanikiwa kutokeza suluhu ya moja kwa moja ya kuwafanya Waamerika warud kuwa wamoja na kufikir kwa kasi katika mageuzi ya kiulimwengu. Hawana Adui mwenye Nguvu. Hawana adui mwenye mikakati ya kuwatishia kuwatawala zaid ya kuwatishia na matukio ya kigaidi.

Je, Kuibuka kwa Trump na kile alichokipandikiza kwa Waamerika juu ya uhatari wa China na Iran ilikuwa ni kete muhimu na yenye uhalisia wa Adui mweny nguvu?

Je, huenda tunaweza ona mabadiliko ya sera yatakayolifanya dola la America kushikamana kwa nguvu na kuchakata bongo zao katika kujinusuru na tishio la kasi ya China?

Je, nadharia ya kuwa America aliitengeneza USSR ili kutimiza malengo ya kuhodhi mamlaka ya kiulimwengu ina mashiko?

Tafakuri yetu kama Taifa kwa sasa, ni kipi kinachotuunganisha watanzania ilhal tukijisifia Amani yeny chembechembe nyingi za woga na makandokando ya Ujamaa uliofeli?

Taqabaliallahu minna waminkum.

IDDUL MUBARAQ
 
Back
Top Bottom