Tokyo: Mashindano ya Olimpiki 2020 yakamilika

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Baada ya kushuhudia wiki mbili za mashindano ya aina yake katika historia, hatimaye Michezo ya Olimpiki mjini Tokyo nchini Japan imeahirishwa hii leo na kijiti kukabidhiwa kwa Paris, muandaaji wa mashindano hayo mwaka 2024.

Mashindano ya mwaka huu yalikuwa ya tofauti kutokana na maambukizi ya virusi vya corona, na yaliahirishwa mwaka jana kutokana na virusi hivyo. Michezo ilifanyika kwa tahadhari kubwa, huku visa 430 vya maambukizi vikigundulika, vikiwamo visa 32 ndani ya Kijiji cha Olimpiki.

Mashindano ya mwaka huu yameshuhudia aina 50 za michezo, iliyochezwa katika jumla ya matukio 339. Mataifa yaliyoongoza kwa kuwa na medali nyingi ni pamoja na Marekani iliyokuwa na medali 113. China yenye medali 88, Urusi ikiwa na medali 71, Uingereza ikiwa na medali 65 na Japan ikiwa na medali 58.

Barani Afrika, Kenya inaongoza kwa kutwaa medali nyingi zaidi, ikiwa na medali 8, ikifuatiwa na Uganda na Afrika Kusini.

Wanariadha watatu waliiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo, ambao ni Gabriel Gerald Geay, Alphonce Felix Simbu, aliyemaliza katika nafasi ya 7 katika mbio za marathon kwa wanaume na Failuna Matanga aliyemaliza katika nafasi ya 24 katika mbio za marathon kwa wanawake.

1628441485423.png


1628441108627.png


Mashindano yajayo yanaanza ndani ya siku 180 tu zijazo, kwa michezo ya msimu wa baridi mjini Beijing, licha ya visa vipya vya maambukizi ya corona nchini humo. Ufaransa inajiandaa kukamilisha maandalizi ndani ya miaka mitatu ijayo, kabla ya michezo hiyo kufanyika tena Los Angeles (Marekani) mwaka 2028, na Brisbane (Australia) mwaka 2032.
 
Paris nitayakosa lkn ya USA 2028 nikiwa hai lzm niende,naanza kujipanga kuanzia leo
Nalog off
 
Back
Top Bottom