Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,551
- 8,310
Nilianza safari yangu kutoka Mwanza kuelekea Mbinga kwa raha mustarehe ila nikijua huko mbele kuna tabu kwelikweli sababu ya barabara mbovu kutoka njia panda ya Peramiho hadi Mbinga, lakini nilichokikuta ni uroda! yaani ni barabara ya lami safi sana toka pale Peramiho hadi Mbinga.
Ni barabara ya kiwango kwa kweli make pia kuna sehemu barabara imechongwa ikawa chini zaidi kiasi cha kutengeneza ukuta mrefu ambapo mtu hawezi kupanda kutoka barabarani kwenda kwenye makazi, lakini hawa jamaa wametengeneza ngazi ambapo watu wanapanda kiulaini tu. Duh niliposoma vibao pembeni kumbe ile barabara nzuri tumejengewa na watu wa Marekani.
Hongerani sana wamarekani sisi wamatengo tunawapenda mno.