Toka mtandaoni: Wapungie mkono!

Toka mtandaoni: Wapungie mkono!

Siku moja nilichukua taxi nikiwa naelekea uwanja wa ndege. Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara.

Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu. Pasipo kutegemea dereva wa gari la taka akaanza kufoka na kutoa matusi kwa kelele kubwa!

Katika hali ya kushangaza dereva wa taxi alitabasamu na kuwapungia mkono waliokuwa kwenye gari la taka na ndipo kwa mshangao nilimuuliza; "Inakuwaje ufanye hivyo wakati walitaka kutuua na hata kuharibu mali yako?"

Akajibu kwa upole akinitazama kwa tabasamu akasema. “Katika maisha yetu, kuna watu wako kama gari la taka. Wamejaa misongo, hasira, maumivu, wamechoka kifikra, kiuchumi na kimaisha, na wamejaa masikitiko mengi. Watu hao takataka zao zinazopowazidi hutafuta mahali pa kuzitupa na haijalishi mazingira wanakozitupia.
Hivyo jIfunze kutogombana nao. Wapungie mkono, wape tabasamu, songa mbele. Haikupunguzii kitu. Wala usiruhusu takataka zao zikupate."

Uliumbwa kuyafurahia maisha. Usiyafupishe kwa kuamka asubuhi na kinyongo, na hasira, na ghadhabu kwa sababu ya mtu fulani.

Neno linasema ; “Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.”

Watafiti wanasema 10% ya maisha ni vile ulivyoyatengeneza lakini 90% ya maisha ni vile unavyoyachukulia .
USIACHE KUMTEGEMEA MWENYEZI MUNGU
Aisee!!
Andiko hili ni kama Tundu Lissu analitumia kwa asilimia 100 kila siku, sura yake imejaa tabasamu, mikono yake muda wote anaipunga hewani, ezi ifu hajawahi kukumbwa na umauti.
Mimi ni nani nijaze hasira kifuani pangu na kukunja ngumi kwa kiburi?

Kuanzia sasa nitapunga hewani.

Ubarikiwe sana
 
Ustaarabu/Uungwana/Uvumilivu ni lazima uwe na kikomo.

Sometimes in life we need to fight a good fight in order to defend our dignity, dignity of loved ones or those who are weak and therefore unable to defend themselves.

We need more Lissus in our beloved country.



So unampinga mtumishi wa Mungu.
 
Punga mkono
f4ebc421a2f4457f954494386610c6ff.jpeg
 
Haah,eti ''mtumishi'', ebo, humjui huyo Mshana tu, tafuta nyuzi zake humu za uchawi,wee utakoma.
Amejulikana mpaka kwenye nyuzi za kikenya kama tabibu asilia mkuu.
Mmh ila huyo mdau ananifahamu vilivyo
 
Ustaarabu/Uungwana/Uvumilivu ni lazima uwe na kikomo.

Sometimes in life we need to fight a good fight in order to defend our dignity, dignity of loved ones or those who are weak and therefore unable to defend themselves.

We need more Lissus in our beloved country.
BAK nakuelewa sana ila wapungie tu mkono
 
Aisee!!
Andiko hili ni kama Tundu Lissu analitumia kwa asilimia 100 kila siku, sura yake imejaa tabasamu, mikono yake muda wote anaipunga hewani, ezi ifu hajawahi kukumbwa na umauti.
Mimi ni nani nijaze hasira kifuani pangu na kukunja ngumi kwa kiburi?

Kuanzia sasa nitapunga hewani.

Ubarikiwe sana
Kuanzia sasa nitapunga hewani.
 
Mtani wangu ukiachana na mambo ya tunguli, wewe ni mwalimu mzuri sana wa neno la Mungu.
 
Kwa neno lake hilo la hekima,his malevolent,wizard ,sir mshana jr,the great one,kwa heshima na taadhima na kwa unyenyekevu mkubwa ninamuomba ikimpendeza aniruhusu niutumie uzi wake kuwapungia mkono CCM.
Usijaribu jiwe ata kufokea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom