Toka mtandaoni : Elimu yetu... Tunakosea wapii?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
*By Prof Kamuzora RAS Kagera:*

Tatizo lile lile nililolisema awali. Falsafa ya Elimu yetu ni kuwa watu wanasomea taifa na si kusomea maisha yao. Hivyo, wote mnaingizwa kwenye behewa kuelekea kwenye combinations ambazo Taifa limechagua yaani PCM, PCB, PGM, CBG, CBN, ECA, EGM, HGL, HGE, HGK. Ukikosa nafasi kwenye behewa sasa ndio ukatafute hizo fursa zingine za NACTE na VETA.

Falsafa hii na mfumo huu una athari za kisaikolojia. Kwanza unafanywa watu wakikosa nafasi kwenye behewa la form five wajione kuwa ni watu waliofeli na waliopoteza ndoto za maisha. Pili, inafanya elimu ya NACTE na VETA kuonekana kama ni sitara na hifadhi kwa waliokosa nafasi behewani. Matokeo yake, tunapeleka huko kwenye NACTE na VETA waliopoteza matumaini. Yaani tumegeuza NACTE na VETA kuwa ni elimu mbadala na si chaguo tu kama kwenda form 5.

Katika hili nitapenda kutoa mfano wa jamii ya watanzania wenye asili ya asia. Hivi hawa wanaishiaga wapi? Mbona wengi hawaendi form 5 na hata wanaoenda hawasomi HGL, HGK na HGE bali utawakuta aidha kwenye PCB, PCM na ECA na EGM? Na je mbona huko chuo hawaonekani kwenye vitivo vya Sheria, Sayansi ya Siasa, Sociolojia na Historia na Archaeology? Mbona ni kama hawapo kabisa kwenye Masters degree zinazotolewa na Chuo Kikuu kipendwa cha UDSM na pia hawapatikani kule kwenye Masters za jioni za Mzumbe wala zile za Open University? Lakini mbona pamoja na kutowaona huko kote hatuwaoni mtaani wakipita na bahasha za khaki zenye photocopy za vyeti na barua za kuomba ajira?

Wenzetu hawa walishajinasua siku nyingi katika mtego wa fikra tuliouingia wa kusomeshea watoto kwenda kujaza nafasi za wanaostaafu na kufa katika sekta ya umma. Wenzetu wanajifunza stadi zaidi. Anayetaka uhasibu, akifika form four anajisajili kwenye mitihani ya Bodi za Uhasibu (NBAA na ACCA) anaendelea huko. Wengine watakwenda kujifunza masuala ya kukatisha tiketi za ndege IATA system, wengine watakwenda kujifunza stadi za Hardware na Software Engineering na stadi nyingine nyingine. Wengine watasomea u-pilot, wengine insurances nk. Leo nenda kwenye nursery schools walimu wengi ni watanzania waasia kwa kuwa wanakwenda kusomea fani hiyo. Kwao behewa la form 5 ni moja tu kati ya mabehewa mengine na si behewa takatifu au la wateule.

Wenzangu na sisi tunakwenda na behewa, tunaingia chuo tunapigwa sumu ya DS 101 tunakuwa wanamapinduzi na wachukia mabeberu huku tukisoma archaeology, Sociology, Political Science na Kiswahili mwisho wa siku tunasubiri Sekretariati ya Ajira itangaze kazi tunajikuta inaajiri asilimia 10 tu ya waliomaliza chuo. Mwishowe hao hao wasomi wanarudi kuajriwa na mabepari waliokuwa wanawachukia wakiwa chuo.

Kuna kitu tunakosea mahala.
 
Shida hata viongoz na wasomi mbalix2 wanajua elimu yetu inakwama wapi ila hawataki kuikwamua iwe bora kwa watanzania wanataka waendelee kututumia mpaka
 
Tunakwama, sababu watu wenye akili zao;wanaweka akili zao tumboni sababu ya ushabiki wa kivyama badala kukaa ku-discuss mambo muhimu ya kulijenga taifa.
 
shida ni kuwa hivyo vyuo mbadala mfano vya veta na technician type huwa havipewi kapaombele sana na vingine vimefanyawa kuwa vyuo vikuu na sasa vinatoa degree badala ya ma technician kama zamani baada ya watu kuona mentality ya watu ni kuwa na degree .Ila issue nyingine ni exposure kaka watu hatuna ,wale waliopata hiyo akili wanajiunga na hizo soft skills badala ya kujikita kwenye hard skill type of knowkedge.
 
*By Prof Kamuzora RAS Kagera:*

Tatizo lile lile nililolisema awali. Falsafa ya Elimu yetu ni kuwa watu wanasomea taifa na si kusomea maisha yao. Hivyo, wote mnaingizwa kwenye behewa kuelekea kwenye combinations ambazo Taifa limechagua yaani PCM, PCB, PGM, CBG, CBN, ECA, EGM, HGL, HGE, HGK. Ukikosa nafasi kwenye behewa sasa ndio ukatafute hizo fursa zingine za NACTE na VETA.

Falsafa hii na mfumo huu una athari za kisaikolojia. Kwanza unafanywa watu wakikosa nafasi kwenye behewa la form five wajione kuwa ni watu waliofeli na waliopoteza ndoto za maisha. Pili, inafanya elimu ya NACTE na VETA kuonekana kama ni sitara na hifadhi kwa waliokosa nafasi behewani. Matokeo yake, tunapeleka huko kwenye NACTE na VETA waliopoteza matumaini. Yaani tumegeuza NACTE na VETA kuwa ni elimu mbadala na si chaguo tu kama kwenda form 5.

Katika hili nitapenda kutoa mfano wa jamii ya watanzania wenye asili ya asia. Hivi hawa wanaishiaga wapi? Mbona wengi hawaendi form 5 na hata wanaoenda hawasomi HGL, HGK na HGE bali utawakuta aidha kwenye PCB, PCM na ECA na EGM? Na je mbona huko chuo hawaonekani kwenye vitivo vya Sheria, Sayansi ya Siasa, Sociolojia na Historia na Archaeology? Mbona ni kama hawapo kabisa kwenye Masters degree zinazotolewa na Chuo Kikuu kipendwa cha UDSM na pia hawapatikani kule kwenye Masters za jioni za Mzumbe wala zile za Open University? Lakini mbona pamoja na kutowaona huko kote hatuwaoni mtaani wakipita na bahasha za khaki zenye photocopy za vyeti na barua za kuomba ajira?

Wenzetu hawa walishajinasua siku nyingi katika mtego wa fikra tuliouingia wa kusomeshea watoto kwenda kujaza nafasi za wanaostaafu na kufa katika sekta ya umma. Wenzetu wanajifunza stadi zaidi. Anayetaka uhasibu, akifika form four anajisajili kwenye mitihani ya Bodi za Uhasibu (NBAA na ACCA) anaendelea huko. Wengine watakwenda kujifunza masuala ya kukatisha tiketi za ndege IATA system, wengine watakwenda kujifunza stadi za Hardware na Software Engineering na stadi nyingine nyingine. Wengine watasomea u-pilot, wengine insurances nk. Leo nenda kwenye nursery schools walimu wengi ni watanzania waasia kwa kuwa wanakwenda kusomea fani hiyo. Kwao behewa la form 5 ni moja tu kati ya mabehewa mengine na si behewa takatifu au la wateule.

Wenzangu na sisi tunakwenda na behewa, tunaingia chuo tunapigwa sumu ya DS 101 tunakuwa wanamapinduzi na wachukia mabeberu huku tukisoma archaeology, Sociology, Political Science na Kiswahili mwisho wa siku tunasubiri Sekretariati ya Ajira itangaze kazi tunajikuta inaajiri asilimia 10 tu ya waliomaliza chuo. Mwishowe hao hao wasomi wanarudi kuajriwa na mabepari waliokuwa wanawachukia wakiwa chuo.

Kuna kitu tunakosea mahala.
huyu mwalimu wangu kumbe nae kashatolewa pale mliman ...hi kutoa wasomi kutoka kufundisha vikuu je inaimarisha uongozi wa kisiasa au inahatarisha maisha ya ujifunzaji pale vyuo vikuu?
 
Behewa la wengi hili, nafikiri changamoto ni lugha, waasia wanatuzidi kwenye lugha ya malkia. Naamini kwa wakati huu ambapo jamii imeamka kupeleka watoto English Medium itasaidia kutoka kwenye behewa.
 
Lakini ilo is ligha halitakuwa mkombozi wa elimu yetu fikra na muongozo mpya kuusu elimu unaitajika najiulizaga sana tunanchi kubwa sana na tuko nyuma kwenye teknolojia ya kila kitu si kwenye vifaa vya kilimo,Afya, na kuendelea na kibaya ata wataalamu ni wachache hasa kwenye sekta ya kilimo ila vyuo vingi ni vya management na serikali haioneshi juudi ya kuvipunguza na kuongeza ivi cha teknolojia kwa kushirikiana na wadau wa elimu tuna wakati mgumu sana kufikia uchumi wa kati
 
Back
Top Bottom