Toka Bungeni: Mali mpya za Makonda zatajwa, atakiwa aseme pesa anatoa wapi

Msitutoe kwenye lengo, Lingo hapa ni dawa za kulevya sio vinginevyo, makonda tutamjadili siku ingine.
Acha tuendelee na yote kwa pamoja, inawezekana yako related. Tuna muda ndugu yangu, wengi hatuna kazi.
 
MAKONDA mungu akutie nguvu, Tulipulie na wabunge waliopo ndani ya Bunge, wanacho jaribu ni kusimamisha harakati zako kwa nguvu zote ili wasitajwe
Na yeye ajilipue vile vile. Naona kama mahakama ya mafisadi karibu itapata kesi!
 
Mlikuwa wapi kuhoji hayo, hilo shimo lililomwagiwa mafuta ya taa sasa na kenge wameanza kutoka.

Mbona alitoa bilioni nane za ujenzi wa makao makuu ya bakwata, mbona katoa pickup kwa kila mwenyekiti wa mtaa.

Eti kampa mkewe benzi ya mil miatano! Hata gari la obama halijafikia hiyo bei, kwahiyo kwenye hiyo birthday ulikuwepo? Upumbafu mtupu.
Tatizo huwa hamsikii wengine wakihoji mpaka waje wazalendo namba wakisema ndio kweli.
 
Je, walikuwa wapi kabla ya Makonda kuanza operation ya madawa ya kulevya kusema wanayosema leo? Ina maana Makonda asingeanzisha hii vita wangemwacha tu na hizo mali zake?
Yaani ndio nature ya mwanadamu ukimchokonoa na akachokonoleka..atakuchokonoa kweli sio utani....sasa watu wameanza kumchunguza sana baada ya hili sakata
 
Hivi tuhuma za kweli? Kamanda Siro kazi kwako, Makonda aripoti sentro ijumaaa ijayo kutoa maelezo ya kutosheleza venginevo- rumande! HAKI! HAKI sawa kwa wote.
Siri nae si aliwaambia anachukua pesa za watu wa shisha, Takukuru wanaendelea na uchunguzi.
 
Wanasema ukimwaga mboga na mie namwaga ugali, haya sasa hii muvi sijui utaishia wapi....?

Naona baadhi ya waheshimiwa wabunge biashara zao za kuuza ngada zimeibuliwa sasa, wakaona isitoshe nao wakaanza kurudisha mapigo
Mbona mhusika (people's choice) kimya wala hapingi ndio kwanza anaunga mkono vita dhidi ya madawa. Jitahidi usome saikolojia ya watu.
 
MAKONDA mungu akutie nguvu, Tulipulie na wabunge waliopo ndani ya Bunge, wanacho jaribu ni kusimamisha harakati zako kwa nguvu zote ili wasitajwe
Brabraa stako kuskia..
Mwambie dogojanja atangulie mjengoni akakalie kitimoto Aeleze kwanini amesema mjengoni ni kijiwe cha porojo na kusinzia
 
Povu lote hili kutajwa Mbowe!Mlikuwa mnataka mapapa sasa,wanaanza kutajwa watu wametaharuki.
Wabunge wanatumia kinga yao vibaya,waite waandishi maelezo watoe tuhuma hizo kama kweli wanajiamini.
Tunasubiri kwa hamu kesho hotuba ya Rais.Makonda endelea na kazi usitishwe na wabunge,tumewazoea hao,wakiguswa tu maslahi yao hawakawii kutumia kinga ya kibunge kurusha uongo
Mbowe mbunge katajwa kwa chuki. Majina hayana mbunge Mbowe yana muuza madawa Philemoni Mbowe. Sasa Makonda kwa sababu zisizoeleweka anataja Freeman badala ya Philemoni. Ndo ujue anaekichukia hata ukikaa kimya atasema unapayuka. Chokochoko tuuuuuu kazi hafanyi.
 
Unapotaka kusafisha njia nilazuma use msafi kwanza,kama ni mchafu yeye!atasafishaje yeye wenzake?
 
Tuache unafik unamuatack mtu baada ya Kuingilia maslahi yako kabla ya hapo ulikuwa unamsifia,
Iko hivi, watu huwa hawapigani hadi wachokozwe. Maisha yako usisahau hilo. Yeye makonda alipoamua kuanzisha vita kubwa kama hii alipaswa kujua anapigana na nani.

Sun Tzu kwenye "The Art of War" (karne 6 K.K.) anakwambia kushinda/ndwa vita hubainika mkingali mezani (intelijensia?). Na usiende vitani kama hujajua uwezo wa adui.

Huko kote mbali. Hapa kwetu wahenga walisema..... "Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji". Na huenda hawakumpenda sana mgema maana walimnanga kwa kauli........ "Cha mgema huliwa na....."

Makonda aidha hajamsoma au amempuuza Sun Tzu na pia ameakisi ya Mgema. Sie ni kuangalia sinema ya bure hadi ukomo wake. Mwishoni tutajua inatufunza nini?
 
Watu wanapotishia maslai ya Mfalme ni jambo la kawaida kwa walinzi wa boma la mfalme kuchukua hatua zozote zinazowezekana kumlinda Mfalme pia kuna kauli JPM alisema kuwa wapo wanaccm mchana usiku ni wanamgambo nadhani ni wakati mwafaka wa kuwajua Double Agent

So siwezi kushangaa leo Bunge kutetea wahalifu na wauza unga kwani ndio sehemu ambayo mtu yeyote anaweza kuingia tu akiwa na fedha ,hakuna vetting kama vile Serikalini au Mahakamani ukiona sehemu ambayo wanasema mtu yeyote tu anaweza ingia bt ajue kusoma na kuandika tu. Basi jiandae kupokea vilaza, majambazi, magaidi, wenye elimu, wasio na elimu na wote interview ni kushinda uchaguzi tu .hakuna cha vetting kujua hawa wanaoingia ni watu gani au wanajihusisha na nini kabla ya kuingia hapa ndo maana tunaona wakina Msukuma , Lema watu waliokuwa ............... wapo Bungeni leo

Bunge ni Muhimili muhimu kila kitu kinaanzia pale then ndo kinakwenda Mahakamani au Serikalini Bunge ni kama Maji ya kunywa na maji ya kunywa ni lazima YACHEMSHWE NA KUCHUJWA VIZURI kitu ambacho kwa wabunge wetu hakipo.
Povu lote umesahau kusema Makonda alimpiga Warioba. Akafunga viatu vya Ridhiwani. Unadhani mtu wa hivyo ana dhamira safi?
 
Iko hivi, watu huwa hawapigani hadi wachokozwe. Maisha yako usisahau hilo. Yeye makonda alipoamua kuanzisha vita kubwa kama hii alipaswa kujua anapigana na nani.

Sun Tzu kwenye "The Art of War" (karne 6 K.K.) anakwambia kushinda/ndwa vita hubainika mkingali mezani (intelijensia?). Na usiende vitani kama hujajua uwezo wa adui.

Huko kote mbali. Hapa kwetu wahenga walisema..... "Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji". Na huenda hawakumpenda sana mgema maana walimnanga kwa kauli........ "Cha mgema huliwa na....."

Makonda aidha hajamsoma au amempuuza Sun Tzu na pia ameakisi ya Mgema. Sie ni kuangalia sinema ya bure hadi ukomo wake. Mwishoni tutajua inatufunza nini?
uko sahihi mkuu wacha tuone hii Sinema
 
Kinachoendelea sasa hivi ni kumuattack Makonda na familia yake ili kumpunguza speed..mtu unasema kanunua appartment lete hapa hata ownership certificate kutushawishi mara mke wake anaendesha MB na gharama unaijua kama ni ya rafiki au ndugu...simtetei makonda ila Wabunge wanamwongelea makonda kuliko majukumu yao wananchi tunashida za kijamii nyingi sanaa Wabunge wetu wanakaa wanamjadili makonda kisa yeye hayupo bungeni hawezi kusema na kupinga....sugu anamtolea maneno yakashfa makonda afu Mbowe analalamika anafamilia anawatoto mara kiongozi wa jamii...kwani mke wake makonda anafurahia hayo maneno ya kashfa na matusi wabunge wanaomtukana Makonda? Sioni kesho ya kizazi kijacho khabisa.
Nani alianza? Ukichokoza ujue na kupigana
 
Back
Top Bottom