Togo Yapiga Marufuku Adhabu ya Kifo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Togo Yapiga Marufuku Adhabu ya Kifo.

Discussion in 'International Forum' started by Junius, Jun 25, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Lome-Togo,
  Bunge la Togo hapo jana limepitisha sheria ya kupiga marufuku utekelezwaji hukumu ya kifo.
  Waziri Mkuu wa Hispania Jose Luis Rodriguez Zapatero alishuhudia Bunge hilo la wajumbe 81 likipitisha sheria hiyo.
  "Ni hatua nzuri kwa taifa la Togo katika kurejesha demokrasia na kulinda haki za binaaadamu" alisema Zapatero.
  Rais wa taifa hilo la Magharibi ya Afrika Faure Gnassingbe anatarajiwa kusaini sheria hiyo tayari kuanza kutumika.
  Togo inakuwa nchi ya 15 kati ya wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na ni ya 94 duniani kupiga marufuku adhabu ya kifo.
  Mara ya mwisho kwa nchi hiyo kutekeleza adhabu ya kifo ilikuwa ni mwaka 1978 na tokea hapo imebakia katka vitabu vya sheria bila ya kutekelezwa.

  SOURCE: VOA/AP
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Taarifa hii inafurahisha. Sisi tanzania tunangoja nini kubadilisha sheria zetu ili kuondoa adhabu ya kifo, does it really make sense kuzuia kitendo cha kuua kwa kuua? Je toka adhabu hii imekuwa ikitekelezwa kumekuwa na kupungua kwa makosa hayo? in the sense kuwa inadeter watu kurudia kufanya hivyo?

  Tume ya kurekebisha sheria iamke!!!!!!!!
   
 3. Eliaona

  Eliaona Member

  #3
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Thumbs up Togo, you are in the right direction
   
Loading...