Mimi nimependa kufananisha hizi za Monduli na za Zulu, ili kuonyesha jinsi akili zilivyo tofautiana. Hizi za Kizulu zinaonyesha elimu na IQ kubwa kuliko zile za Monduli.
Sidhani uko sahihi unapolinganisha
IQ ya
waZulu na
waMaasai kwa kufananisha namna nyumba zao zilivyojengwa tu.
Maoni yangu:
1. Nyumba za
waMaasai ni za muda mfupi (sio za kudumu) kulingana na maisha yao ya kuhamahama. Kwa sababu hii wanatumia pembejeo za ujenzi zinazopatikana kiurahisi na zisizogharimu pesa. Pembejeo hizi za ujenzi ni kama vile
kinyesi cha mifugo yao,
udongo na
vitawi vya miti ilio karibu katika kutengeneza hizi nyumba zao. Msimu ukiisha wanabeba virago vyao tu na kuhamia sehemu nyingine ambako watajenga vibanda vingine.
2. Nyumba za
waZulu ni za kudumu kwa sababu hapo kijijini ndio makazi yao makuu zilipo familia zao na ya
chifu wao. Wanaume wataondoka kwenda kuhemea, kuchunga, au kupigana lakini mwishowe wanarudi kijijini kwenye familia zao. Hii inawafanya wawe na nyumba za kudumu zinazokarabatiwa miaka nenda miaka rudi, na ndio maana zinaonekana hivyo.
3. Lakini pia kwa mfumo ulivyo na ulivyokuwa
Afrika Kusini, hata kama hao waZulu wangetaka kuhamahama kama waMaasai wasingeweza kufanya hivyo kwa namna ardhi ilivyokuwa ikimilikiwa hapo zamani na inavyo milikiwa sasa. Huwezi ukazagaa tu mbugani na kuamua kujenga tembe lako popote Afrika Kusini. Kila mita moja ya mraba inamilikiwa na mtu, tofauti na Tanzania ambako waMaasai wanaweza kuhamahama wapendavyo kwenye maeneo yao. Sijui hali hii itaendelea mpaka lini.