At&t ni kampuni ya simu kama vodacom, ni ya kimarekani. Ila wao wana system tofauti na sisi, wanaingia mikataba na watengenezaji wa simu kama samsung, htc, sony na nyinginezo. Wananunua brand na baada ya hapo unanunua simu toka kwao, zikiwa locked kwenye network zao, mfano, waweza nunua samsung galaxy iii kwa mkataba wa miaka miwili kwa kulipia dola 100 kila mwezi, hiyo simu itakuwa locked, maana yake utatumia network za at&t tu, huwezi tia sim card ya verizon au zingine, mkataba ukuiisha unauhuru wa kununua sim nyingine.
Wanaoishi huko watatufahamisha zaidi.