Tofauti ya masikini na tajiri katika ndoa

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
7,033
15,616
Morning JF,

Ingawa wanawake wengi wamekuwa wakiota kuolewa na matajiri au watu wenye uwezo ilhali yy mwanamke std7 na kwao maskini tegemea yafuatayo.
1)Mwanaume kukudharau na kuku
nyanyasa akijua hutaweza kurud
Kwenu ulikotoka.
2)utateswa na mawifi na wakwe wakijua umefata pesa kwa mwanae ht km unampenda kweli.
3)wazazi au ndugu zako wakija kukusalimia watadharauliwa pia na utapigwa mbele yao ht kama huna kosa.
4)utaendesha gar nzur utakula vizur utafany shopping lakin hutanenepa utazid kukonda wanawake wenzio wataona unafaidi lakin ukwel unao moyoni.
5)utavumilia ufe na tai shingoni ukiogopa kuondoka utachekwa na wabaya wako.

UKIOLEWA NA MASKINI

1)atakusaidia kuosha vyombo kupika na kufagia nk.
2)Mtakaa pmj kujadil jinsi kujiendeleza kimaisha.
3)mtakuwa marafiki mtashirikishana kila jambo.
4)hutakula vizur sn lakin utanenepa sbb ya nyama ya ulimi(kauli njema)
5)atapigana na yyte kwa ajili yako
Hatakubali uonewe kabisa.

KAZI KWENU WADADA
 
Huwa hakuna generalisation kwenye ishu za mapenzi, mahusiano na ndoa.
Ni kama mziki wa reggae kila mtu na style yake ya kucheza.
 
Hakuna mtu asiyependa pesa hivyo mwanamke mzuri na mrembo hawezi kukataa ofa za watu wenye fedha wanaomgombania kwa kuhofia eti atanyanyaswa. Isitoshe mwanamke mrembo siku zote anajiamini, anajua hata ukimuacha wewe atapata mwingine. Kwa mwanamke kujiamini hutokana na uzuri wake na kwa mwanaume pesa yake (ceteris paribus).
 
Mmh haya mambo hayana SI unit kabisa. Unaweza ukaolewa na maskini, mwanzoni atakupenda, atakujali, atakudekeza hadi uhisi dunia nzima wewe ndo unayependwa kumbe mmmh, kuna watu wana adabu kwa sababu hawana hela. Siku akizifuma sasa Hehehehe, "atahamia kwa wenye hadhi yake". Subiri akifulia ndo atakukumbuka na atarudi na kijuso chake.

Zamani nilidhani mtu ukitoka naye chini ndo atakuheshimu wee, but Sidhani kama hiyo ipo tena, kwa wachache sana. Hakuna uhusiano wa kuwa maskini na kuwa na upendo wa dhati, mwengine atajilazimisha tu kukupenda coz you are what he can afford for now (he has to settle for what is available), na kuna mwingine hela hana na adabu hana, atakudunda na atachepuka tu, huyu ndo komesha.
 
Mkuu sio kweli kama ukiolewa na maskini utakua na raha,nadhani ni hulka ya mtu kua na tabia chafu na hata hao wenye pesa kuna wengine utasema laitani mwenyezi mungu angeumba wanaume wote kama huyu,chamsingi nikuomba mungu tuu akupe mwenye kheir nawewe,mie mume wangu amenioa hana kitu nimemsomesha biashara nimechukua mkopo bank
nilikua nafasiri na mimba mpaka miezi 8 kwakua nilikua naenda kuchukua mzigo china,usa,singapore,na sio kama kwetu
walikata kumsadia hela ya mtaji yeye ndio alikataa kusaidiwa na mzee wangu leo hii Alhamdulillah lakini alikuja nambia
nimeiba pesa ya Brother wake alinigeukia kama hanijui, sasa mtu kama huyo unasemaje? sasa chamsingi nikumuomba
mwenyezi mungu atupe subra na atupe wenye kheir na sie kwenye maisha...
 
Eti atakusaidia Kuosha vyombo plsss...mwanaume yupi Africa anafanya hio kazi
 
Hakuna mtu asiyependa pesa hivyo mwanamke mzuri na mrembo hawezi kukataa ofa za watu wenye fedha wanaomgombania kwa kuhofia eti atanyanyaswa. Isitoshe mwanamke mrembo siku zote anajiamini, anajua hata ukimuacha wewe atapata mwingine. Kwa mwanamke kujiamini hutokana na uzuri wake na kwa mwanaume pesa yake (ceteris paribus).

hilo neno ceteris paribus bila shaka wewe ni mchumi hahahahhaha
 
Mmh haya mambo hayana SI unit kabisa. Unaweza ukaolewa na maskini, mwanzoni atakupenda, atakujali, atakudekeza hadi uhisi dunia nzima wewe ndo unayependwa kumbe mmmh, kuna watu wana adabu kwa sababu hawana hela. Siku akizifuma sasa Hehehehe, "atahamia kwa wenye hadhi yake". Subiri akifulia ndo atakukumbuka na atarudi na kijuso chake.

Zamani nilidhani mtu ukitoka naye chini ndo atakuheshimu wee, but Sidhani kama hiyo ipo tena, kwa wachache sana. Hakuna uhusiano wa kuwa maskini na kuwa na upendo wa dhati, mwengine atajilazimisha tu kukupenda coz you are what he can afford for now (he has to settle for what is available), na kuna mwingine hela hana na adabu hana, atakudunda na atachepuka tu, huyu ndo komesha.
Hii sentensi yako ya mwisho ni kama unanisema Mimi vile!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom