Tofauti ya mapokezi Hussein Mwinyi (CCM) na Tundu Lissu (CHADEMA)

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Kuna tofauti hapa kati ya mapokezi ya mgombei nafasi ya urais Zanzibar tiketi ya CCM Hussein Mwinyi na mtia nia nafasi ya urais Tanzania Tundu Lissu CHADEMA. Kwa Hussein Mwinyi redio na vituo karibu zote za televisheni vyombo vingine kama mitandao ya kijamii na magazeti pamoja na wakuu wa idara za umma walihamasisha na kuwataka watu kujitokeza kumlaki mgombea huyo wa CCM. Alipokelewa kwa shamrashamra na siku ikapita.

Tukija kwa Tundu Lissu tayari polisi wameonya watu wanaohamasisha mapokezi yake waache Mara moja na kuja na sababu ya kwamba taifa liko kwenye maombolezo kufuatia kifo cha Rais mstaafu awamu ya 3. Hata jeshi limeeleza kuwa kikatiba mtu hazuiliwi kumpokea ndugu yake.

Tundu Lissu anarudi nchini baada ya kukaa nje ya nchi kwa takribani miaka 3 akipokea matibabu baada ya shambulio lililotaka kutoa uhai wake kupigwa risasi 16. Pengine ndugu, wafuasi, marafiki, viongozi wa chama chake na vyama rafiki wangetaka kumpokea na kumpa pole. Vipi polisi waone kuwa haya mapokezi hayastahili na kunuia kuweka zuio? Mbona Kama jeshi la polisi linaonekana kukerwa na matukio yanayowahusu watu wema toka upinzani.

Marehemu Mkapa alikiri kwenye kitabu chake "My Life, My Purpose" kuwa alipotoshwa tukio la 21/1/2001. Sasa kwanini jeshi la polisi kila Mara linajitia kujitoa ufahamu kwenye jambo au tukio ambalo wanaweza kulisimamia kwa kutekeleza wajibu wao kulinda raia na Mali zao. Kwa wakiruhusu Lissu akapokelewa na wafuasi wake nini kitatokea?

Tangu tulipopata msiba huu wa rais mstaafu awamu ya 3, sijasikia kauli tofauti na ya kuenzi mazuri aliyoyafanya mpendwa wetu Mkapa. Hata hayati Mwl. Nyerere baba wa taifa alipoona watu wanambeba Augustine Mrema, aliwaomba jeshi a polisi kuwaacha wananchi wambebe hata kama machela.

Wito wangu: Jeshi la polisi waache wanasiasa washindane kwa hoja na hata kuna mtu anamzidi mwenzake kwa umashuhuri aachwe, wananchi ndio wataamua. Mbona kila siku tunasikia na kuona Mara wananchi wamekusanyika na kuzuia msafara wa rais, kipi ni hatari ?

Polisi tulizeni boli,nchi hii hahitaji nguvu bali upendo, haki na busara!
 
Mkuu kongole zitue kwako, kwa kuwa umeweza kuainisha "double standards" zinazofanyika hadharani bila hata aibu yoyote ile. CCM ya leo inataka kuhodhi kila kitu, lkn kamwe haitaweza kuhodhi yaliyo mioyoni mwa watu na hisia zao chanya kwa wale wawapendao na kuwaunga mkono.

Mienendo ya Jeshi la Polisi Tanzaniai kwa sasa ni sawa kabisa na kioo chenye kuweka wazi "reflection" ya hofu ya CCM dhidi ya Tundu Lissu na upinzani wa kweli kwa ujumla. Bila mbeleko ya dola CCM hakuna kitu.
 
Back
Top Bottom