Tofauti ya Democrats na Republican ni ipi?

Kijakazi

Platinum Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
10,909
Reaction score
18,910
Nimekuwa nikifwatilia sana Siasa za Marekani kwa muda sasa lakini kuna kitu sijaelewa mpaka sasa hivi, ni ipi tofauti kati ya Vyama vyao viwili yaani Republikan na Democrats?

Kwa maana kila nikiangalia kwa mfano sioni tofauti kati ya Raisi Obama ambaye ni Democrat na raisi aliyepita Bush ambaye alikuwa Republican ingawaje wakati wa Kampeni kila mtu alikuwa ananadi sera ambazo ungeweza kusema kwamba hivi ni vyama viwili tofauti vyenye Sera mbili tofauti lkn linapokuja kwenye Sera hasa mmoja wapo anapokuwa madarakani sioni tofauti kabisa kati yao!

Kwa mfano Obama alikuwa anamlaumu Bush (Republican) kwamba ni mtu wa Vita lkn Obama alivyoingia (Democrat) Marekani imeshiriki vita mara nyingi klk wakati wowote ule sia ajabu ktk Historia ya Marekani, Haya mambo ya ushoga, kubadilisha jinsia, kutoa mimba n.k wote wawili hakuna anayepinga, Ukija kwenye mambo ya ndani Bush alianzisha wire tapping yaani Serikali kusikiliza maongezi ya simu na internet ya raia wake Obama alipinga wakati wa Kampeni sasa hvi amefanya zaidi ya Bush, aliahidi kufunga Guantanamo mpaka leo hakuna kilichofanyika, alisema Republicans wanatorture mateka wa kivita Obama alivyoingia kafanya mara dufu yake n.k

Sasa najiuliza tofauti yao ni ipi hasa? Na kama wote wanalingana hivyo kuna haja gani basi ya wao Wamarekani hata kupiga kura si wawe na Chama kimoja tu na kusevu fedha za Uchaguzi?
 
Tofauti ipo, hawa ni REPUBLIKANS na hawa ni DEMOKRATS. Tofauti ya pili ni kuwa Hawawezi kuitawala USA wote wawili kwa wakati mmoja!
 
Una maanisha ni kama banana na orange............?......
 
Na ujue kazi ya upinzani america si kuikosoa serikali bali 'to complicate and block' kupimana ubabe ili watu wakuona hufai kuongoza kwamba ni mnyonge kisha wawape utawala wapinzani wako.
 
Ndio Preta
Afu leo nimepita pita humu sijabahatika kukutia machoni, kumbe upo!

Nipo bana........nilikuwa naendesha Range na V8 kule kwenye thread.......nimesahau ipo jukwaa gani..........
 
Last edited by a moderator:

Najua lift huwezi nipa, basi hata honi, inantosha
 
Swali nzuri sana hili, natumai atakuja mtaalam wa mambo ya Marekani ashushe mambo. Hata mie natamani sana kujua tofauti maana Obama naona amekua mwehu zaidi ya waliokuwepo.
 
Nipo bana........nilikuwa naendesha Range na V8 kule kwenye thread.......nimesahau ipo jukwaa gani..........

ha ha haaa! kila anayepost kule, kama analovileeee duuu, mpaka nimekimbia
 
Republican chama cha matajiri na Democrat chama cha watu wa Masikini.
 
limetumbuka
Republicans ni conservatives (wanasupport mambo ya tamaduni zao na hawataki kuingiliwa na mila za nje. Hivyo basi wanapiga vita immigration (watu wasokuwa wazawa kuruhusiwa marekani) na mambo kama ushoga nk.)
Democrats ni liberals (the opposite)
 
yah...i thought so too...
 
Last edited by a moderator:
Nimekuwa nikifwatilia sana Siasa za Marekani kwa muda sasa lakini kuna kitu sijaelewa mpaka sasa hivi, ni ipi tofauti kati ya Vyama vyao viwili yaani Republikan na Democrats?

Kwa maana kila nikiangalia kwa mfano sioni tofauti kati ya Raisi Obama ambaye ni Democrat na raisi aliyepita Bush ambaye alikuwa Republican ingawaje wakati wa Kampeni kila mtu alikuwa ananadi sera ambazo ungeweza kusema kwamba hivi ni vyama viwili tofauti vyenye Sera mbili tofauti lkn linapokuja kwenye Sera hasa mmoja wapo anapokuwa madarakani sioni tofauti kabisa kati yao!

Kwa mfano Obama alikuwa anamlaumu Bush (Republican) kwamba ni mtu wa Vita lkn Obama alivyoingia (Democrat) Marekani imeshiriki vita mara nyingi klk wakati wowote ule sia ajabu ktk Historia ya Marekani, Haya mambo ya ushoga, kubadilisha jinsia, kutoa mimba n.k wote wawili hakuna anayepinga, Ukija kwenye mambo ya ndani Bush alianzisha wire tapping yaani Serikali kusikiliza maongezi ya simu na internet ya raia wake Obama alipinga wakati wa Kampeni sasa hvi amefanya zaidi ya Bush, aliahidi kufunga Guantanamo mpaka leo hakuna kilichofanyika, alisema Republicans wanatorture mateka wa kivita Obama alivyoingia kafanya mara dufu yake n.k

Sasa najiuliza tofauti yao ni ipi hasa? Na kama wote wanalingana hivyo kuna haja gani basi ya wao Wamarekani hata kupiga kura si wawe na Chama kimoja tu na kusevu fedha za Uchaguzi?

Mkuu hapo kwenye red hizo facts umezipata wapi? Chini ya Obama Marekani imeshiriki katika vita mara ngapi mpaka useme imeshiriki mara nyingi katika historia yake? George W Bush ni mhafidhina (conservative), kamwe hawezi kuunga mkono ushoga, kubadilisha jinsia wala kutoa mimba. Kuhusu hayo mambo mengine uliyoyataja hapo ni sera (policies) za serikali, hazihusiani na itikadi za vyama.

Kwenda vitani ulikuwa uamuzi wa vyama vyote sio Republicans peke yao ila kuna baadhi ya watu kutoka Democrats (akiwemo Obama walipinga) lakini baada ya kuingia madarakani inawezekana amefanya uchambuzi na kugundua kuwa sio rahisi kumaliza vita kama alivyodhani na ndio maana Guantanamo bado haijafungwa.

Sasa nikupe tofauti chache kati ya Republicans na Democrats;

1. Republicans wana mrengo wa kihafidhina (conservatism) wakati Democrats wana mrengo wa kiliberali (Liberalism)
2. Republicans wanaamini katika uhuru mtu mmoja mmoja kujiamulia mambo yake wakati Democrats wanaamini katika jamii kuamua mambo kwa pamoja.
3. Republicans hawapendi serikali isimamie shughuli za kila siku za watu, Democtrats wao ni kinyume na hapo.
4. Republicans wanapenda matumizi makubwa ya kwenye ulinzi (jeshi) na usalama wakati Democrats ni kinyume.
5. Republicans (walio wengi) hawakubaliani na ushoga, ndoa za jinsia moja na kuhalalisha utoaji mimba Democrats (walio wengi) hawana tatizo.
6. Repulicans (walio wengi) wanapinga serikali kudhibiti umilikaji wa silaha wakati Democrats (wengi wao) wanataka serikali idhibiti umilikaji silaha.
7. Repulicans wanataka Marekani idhibiti mipaka yake kupunguza wahamiaji, Democrats wanataka nchi yao iendelee kuwa kimbilio la wahamiaji.

Hizo ni baadhi tu, ukitaka zaidi google "the differences between Republicans and Democrats" utapata link kibao zenye tofauti nyingi na maelezo mengi zaidi.
 
pia Republicans wengi walikuwa wanapinga utumwa wakati Democrats wengi waliuunga.
 
Nimekuwa nikifwatilia sana Siasa za Marekani kwa muda sasa lakini kuna kitu sijaelewa mpaka sasa hivi, ni ipi tofauti kati ya Vyama vyao viwili yaani Republikan na Democrats?

Kwa maana kila nikiangalia kwa mfano sioni tofauti kati ya Raisi Obama ambaye ni Democrat na raisi aliyepita Bush ambaye alikuwa Republican ingawaje wakati wa Kampeni kila mtu alikuwa ananadi sera ambazo ungeweza kusema kwamba hivi ni vyama viwili tofauti vyenye Sera mbili tofauti lkn linapokuja kwenye Sera hasa mmoja wapo anapokuwa madarakani sioni tofauti kabisa kati yao!

Kwa mfano Obama alikuwa anamlaumu Bush (Republican) kwamba ni mtu wa Vita lkn Obama alivyoingia (Democrat) Marekani imeshiriki vita mara nyingi klk wakati wowote ule sia ajabu ktk Historia ya Marekani, Haya mambo ya ushoga, kubadilisha jinsia, kutoa mimba n.k wote wawili hakuna anayepinga, Ukija kwenye mambo ya ndani Bush alianzisha wire tapping yaani Serikali kusikiliza maongezi ya simu na internet ya raia wake Obama alipinga wakati wa Kampeni sasa hvi amefanya zaidi ya Bush, aliahidi kufunga Guantanamo mpaka leo hakuna kilichofanyika, alisema Republicans wanatorture mateka wa kivita Obama alivyoingia kafanya mara dufu yake n.k

Sasa najiuliza tofauti yao ni ipi hasa? Na kama wote wanalingana hivyo kuna haja gani basi ya wao Wamarekani hata kupiga kura si wawe na Chama kimoja tu na kusevu fedha za Uchaguzi?

Kabla sijakujibu ukumbuke USA ilianzishwa kwa mfano wa bible inavyosema .Republican wanatetea ukristo na homosexual is a sin na abortion is wrong .Democratic wanasema homosexual ni kitu kizuri na NDOA sio lazima iwe ya MWANAMKE na mwanamume .Republican hawapendi serikali iingilie mambo yako na serikali ndio tatizo na serikali ndio wezi wenye we na wanaharibu kila kitu.Democratic serikali ndio tegemezi .Denmocratic wengi wao wanapinga Amri za Mungu .republican wanaimani Israeli ni taifa teule ndio maana republican wanamtetea muisraeli.Democratic wao hata masalaba hawapendi walipiga marufuku kusali kwenye public school .Lakini kuna democratic wa aina mbili( bill clinton,JFK na kuna wakina Obama ,Elizabeth warren) na republican nao wamegawanyika kuna Ted Cruz na watu wake na kuna Romney ,bush .Africa hatutoendelea kwa Sababu serikali imetutawala mnooo .
 
Republican chama cha matajiri na Democrat chama cha watu wa Masikini.

HUO NI UONGO mnoo.state zoote ambazo ni expensive to live ni democratic states ( NY,CT,Massachusetts,Virginia,California ,Maine,Washington dc ) hizo zoote ni democratic state unajua kwa nini high Taxes democratic atakuibia pesa akikuona mjinga na maskini haya sasa Republican states Texas ,Phoenix ,Mississippi ,Tn huko ndio unasikia watanzania wengi wanakaa why its cheap republicans no state taxes in some states .Hapa ct gari umenunua cash bado nililipie kodi
 
limetumbuka
Republicans ni conservatives (wanasupport mambo ya tamaduni zao na hawataki kuingiliwa na mila za nje. Hivyo basi wanapiga vita immigration (watu wasokuwa wazawa kuruhusiwa marekani) na mambo kama ushoga nk.)
Democrats ni liberals (the opposite)
Tunarudi pale pale wanapinga immigration kwa Sababu ya spending ( food stamps ,quality ya education inapungua ,Halafu wanachukulia mshahara mdogo immigrant na kumfanya mmarekani mwenyewe kukosa hiyo kazi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom