Tofauti ya degree ni ipi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti ya degree ni ipi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babu Ubwete, Jan 13, 2010.

 1. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #1
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wana JF. Katika Shughuli za kila siku nilipata kuchat na mzungu mmoja afanyaye kazi Barrick Gold, Na tuligusia mishahara wanayolipwa wageni na wazalendo na yeye moja ya sababu alizoto ni kwamba Hata kama wote wana Degree za Business Admin mfano kwao kuna wa canada, New zealand, Americans, South AFricans etc hawa wote degree zao si sawa kwa kigezo cha Course content na gharama walizolipia kwenda university, Ali justify na kusema ni lazima wageni walipwe mshahara juu based on quality of edu waliyoipata hivyo ni haki kabisa kwa mzalendo ama mbogo kulipwa kidogo. Je wana Jf mna maoni gani juu ya hili ni sahihi kweli ukizingatia mtanzania ndio anakuwa na cheo cha chini mzungu anakuwa senior na previlledges kibao ticket za kurudi kwao n stuffs
   
 2. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  nafikiri tatizo ni policy, policy yetu katika madini haiko wazi kuhusu mambo mengi including payments mbalimbali na benefits hizo,na pia nani anastahili kipi kwa sababu zipi,bila kujali elimu yake,ameipata wapi au anatoka wapi. mbona kuna watanzania leo hii wapo Marekani na Ulaya wanafanya kazi na wanalipwa zaidi ya hao wazungu, why b`se wenzetu wana policy,wanaisimamia na wanailinda.
   
 3. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  biashara za mheshimia benjamini kapa hizo ndugu! usithubutu kukacha kupiga kura ifikapo oktober!
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hawa ni expatriets,
  kwa vyovyote wanalipwa pesa na malupulupu kibao
   
 5. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ungetupa picha nzuri kama ungetoa mfano kama kuna mmbongo na yeye amesoma nje katika chuo sawa na mmoja wa hao wataalam wa kutoka huko mshahara upoje? still atalipwa kama mzalendo japokuwa kasomea huko huko kwao tena kwa gharama binafsi

  Japokuwa hata kwa hiyo hali ya awali bado sio sawa kwani mtu analipwa kutokana na nafasi yake katika kazi na masaa anayofanyakazi.

  Vigezo vya kuanza kuangalia rangi na amesomea wapi ni usanii tu huu kwani kwanini umemwajili mtu na kumpa hiyo nafasi kama elimu yake ni chini?

  watu wa daraja moja lazima walipwe mshahara sawa.
   
 6. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #6
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Barrick huwa inatabia ya kupeleka wabongo wachache kwenye crucial dept kama mining geophysicians etc Australia kwenye vyuo fulani lakini wanaporudi huwa wanakutana na mshahara ule ule wa kitanzania. Mining industry huwa haaihitaji sana proffessional ndio maana wengi wao wa step on the ladder by work experience n inhouse training. Swali linabaki ni kweli aliyesoma University of Minnesota twin cities na wa UDSM hawalingani ? kwa field kama za computer mi naamini kwani ukiangalia course modules za UCLA na UDSM au hata vyuo vya canada ni tofauti
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jan 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tunapokuwa watumwa kwenye ardhi yetu ndio huwa nachoka hapo!
   
 8. Jenerali QoyoJB

  Jenerali QoyoJB JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi marais wote hawa na mawaziri jumlisha wataalamu wote serikalini hakuna anayejua kuwa sra zetu zina matatizo mbona kila kukicha tuna lalama na hakuna mabadiliko?
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Kama kampuni inamhitaji sana mtu fulani ni kweli kuwa wanaweza wakamlipa zaidi, hasa kwenye mambo ya bonuses na benefits na chuo ulichosoma kinaweza kupelekea kampuni kukutaka zaidi.
  Lakini kuna wazawa wengi wamesoma nje, je hao nao wanalipwa sawa na expatriates?

  La gharama walizolipa kwenda university naona ni pumba kabisa, Waingereza wanasoma karibia bure, haina maana kuwa elimu yao ni duni.

  Je expatriates nao wanalipwa tofauti kulingana na Chuo walichosoma? Tafuta hilo jibu ndo utajua kama hiyo theory yake ni ya kweli.
   
Loading...