Habari za wakati huu wanajamii?
Natumaini mnaendelea vyema na shughuli zenu za hapa na pale.
Waungwana naomba kujuzwa tofauti ya maneno "nipo" na "niko"
mfano: kama ninaendesha gari natokea Posta Mpya kwenda Ubungo na nimefika eneo la Manzese; mtu akinipigia simu na kuniuliza sehemu ya uwepo wangu nitajibuje?
Je, haya maneno yote yanatumika katika kiswahili au moja sio sahihi?
Kama yote yanatumika, yanatumika kwa kutofautishwa vipi?
Ahsanteni
Haya maneno yanaweza kuwa sawa au si sawa kwa vile mtamkaji ana mazoea ya kutumia lipo..
Hasa yupo mmoja neno alijualo in nipo na sio niko..
Ninachotambua kuhusu niko ni hali inayoonesha hicho kitu,jambo au mtu ni katika ndani ya, katikati ya, au kuzingwa au kuzongwa na..
MF.niko mpira ni..niko kwenye foleni..
Niko nyumbani..
Hali neno nipo linaonesha kitu,jambo, au mtu yuko katika mahala huru kidogo..
MF.Mwalimu darasani akiita majina ktk orodha yake..
John Mussa...? Ataitikia nipooo..
Na hata akiwa hayupo watamjibia hayupooo..
MF.2.
Jamaa kapiga simu na akauliza..
"Mbona huonekani siku hizi" utamjibu nipo..yaani huru kidogo..
N.b Ki lugha matumizi yote ni sahihi kwa mawazo au mazoea ya mtumiaji na kwa watu wake, kwani wakati mwingine ubora wa neno au maneno ktk matumizi hufuatana na mazoea na vile mtakavyoweza kuelewana.
Wadau wa lugha Mpoo..
Mie niko hapa zogoni..