getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,824
Wadau, hebu fikiri wakati wewe ukikua uliamka asubuhi na kuchukua Fagio na dumu la maji, kisha ukawahi namba asubuhi Kwenye mstari shuleni japo kuna baridi lakini ilibidi ukimbie kuwahi, baada ya hapo ulienda kufagia na kumwagia maua katika kitalu chako.ukimaliza unafagia darasa.! Ikiwa ni zamu yako, kisha mnaenda mstarini kukaguliwa, baada ya Ukaguzi wimbo Wa Taifa na wimbo Wa shule kisha sala, ya pamoja.! Baadae bendi inapiga wimbo mnaenda darasani, akiingia mwl mnasimama na kumuamkia shikamoo, mwl, huku mkono kichwani saa nne,! Ni kwa muuza bagia,ukikosa utagawana na mwenzio hata muwe kumi...saa sita utakimbia kula Nyumbani au utabaki shule mpaka saa tisa wakati Wa kazi za nje,kisha matangazo na kurudi Nyumbani ukifika Nyumbani, unamsaidia mama kuchota maji, au baba kukamua ng'ombe au..shughuli zozote, hii ikiwa ni baada ya kula chakula ulichowekewa ambacho bila shaka kitakuwa kiliisha poa..jioni Luna kazi za shule akisha Fanya ataangalia Tv na baba ( kama ipo) ikiwa ni baada ya kuondoa vyombo vilivyotumika.. Kisha ataenda kuandaa kitanda .. Huenda watafanya sala ya pamoja kabla ya kwenda kulala..
Malezi haya ni tofauti sana na malezi ya Leo ambayo mtoto anaamshwa na dada,! Kisha dada anamuandalia vifaa vyake vya shule, bila kusahau mkebe Wa take away ambao ndani yake kuna mayai na vipande vya mkate, labda na kichupa cha juice,
Baadae dada ansindikiza getini ambapo school bus imekuja kumchukua, akifika shule sio lazima sana waimbe wimbo Wa Taifa wala Ukaguzi,! Wanaingia darasani ambapo watu Wa usafi wameshafanya usafi, break tym anaenda kantin, mchana kuna lunch balance diet, akirudi Nyumbani atalala kidogo kisha akiamka atapata maziwa fresh, atacheza game kidogo kwenye computer! Halafu home work then ataangalia movie na daddy kabla ya kwenda kulala Kwenye kitanda ambacho huenda dada amekwisha kuandaa. Siku imeisha..
Wadau
Kati ya haya malezi ya aina mbili ni wapi anapopatikana Mume bora au mke bora, mama bora au baba bora. Ama mzalendo halisi Wa Taifa lake??