Tofauti kati ya Sales na marketing

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Habari za wakati huu;

Wakati nikiwa shuleni niliambia kwamba Every Company employee is Sales Agent and a marketing Agent.Kila mwajiriwa wa kampuni ni afisa masoko na afisa mauzo.Kila afisa masoko ni afisa mauzo na kila afisa mauzo ni afisa masoko.Hii ni falsafa muhimu sana katika uendeshaji wa biashara ndogo.Leo nataka niibue mjadala mdogo nkuhusu tofauti ya Masoko na Mauzo.Masoko na Mauzo ni sawa na IN and OUT unapoingia sehemu.Kwa kawaida ili biashara iitwe biashara lazima ifanye Mauzo.Na ile biashara ifanye Mauzp ni lazima ifanye Masoko.Kwa Mfano mimi ninachokifanya hapa ni Masoko yaani ninapoandika hili andiko hapo na kulipost na kukufanya wewe kusoma kuhusu huduma na bidhaa zangu ninichotafuta hapo ni Masoko.

Kutafuta Masoko/Marketing kama inavoitwa kimombo ni sanaa.Ni sanaa ambayo inahitaji weledi,ubunifu na utulivu wa kipekee ili ianze kufanikiwa.Kwa kawaida Nguvu ya kufanya masoko ikiwa kubwa haimaanishi mauzo yatakuwa makubwa lakini nguvu ya kufanya masoko ikiwa ndogo basi mauzo yatakuwa madogo.Kwa kawaida kampuni nyingi hupenidi kutafuta namna ya kuunganisha kazi za Mauzo na Masoko.Hii ni ama kukwepa gharama,kupunguza idadi ya watu wa kampuni au kwa kutokuelewa.Mara nyingi hii hupelekea mtu anayefanya kazi za Masoko na mauzo kujikuta akiwa na conflicting Priorities.Kwa mfano mtu wa masoko ata hangaika mpaka apate Prospect(Mteja tarajali)Akishafikia hatua hiyo ni mtu wa sale anapaswa kuingia katika hatua ya Pili ya kuclose deal,kutuma invoice kuhakikisha malipo yanapokelewa na kuhakikisha huduma au bidhaa inamfikia mteja.Hata hivyo kampuni nyingi hupenda kuunganisha hizi roles mbili kwa sababu ya muingiliano mkubwa uliopo.Matokeo yake kuna wakati yanakuwa mazur na kuna wakati ynaweza yasiwe mazuri.

Kazi ya mtu wa masoko ni kuhakikisha kuwa kampuni ninapata visibility ya kutosha,bidhaa na huduma zake zinafahamika sehemu nyingi na zaidi ya hapo anatakiwa kuhakikisha kwamba kuna kuwa na kanzi data ya wateja ambayo ina taarifa zote muhimu za wateja.Mtu wa masoko anapaswa kufahamu watu ambao wako targeted na bidhaa au huduma mbalimbali na ni muhimu zaidi kuhakikisha kwamba anafahama demographical profile za wateja na anaelewa key features za huduma na bidhaa mbalimbali.Ni muhimu sana kwa mtu wa masoko kuwa na ushawishi na mvuto wa bidhaa husika na zaidi awe na uwezo wa kumuonesha mteja umuhimu wa bidhaa au huduma mbalimbali na awe pia na uwezo wa kuyaelewa mahitaji ya mteja na kumuonesha jinsi bidhaa/huduma inavyoweza kukidhi mahitaji yake.

Kazi ya mtu wa mauzo ni kuhakikisha mteja ananunua na kulipa bidhaa/huduma Ni lazima awe anaelewa sana kuhusu bei za bidhaa na huduma husika,ajue margins,ajue uwezo wa mteja kifedha na awe tayari kunegotiate bei na mteja na kuhakikisha kwamba mteja anapata fair deal na kampuni inapata fairer deal.Mtu wa mauzo anapaswa kuwa na imani na ubora wa bidhaa yake na anapaswa awe mwepesi wa kufanya maamuzi na kumpa mteja mrejesho.Anapaswa kuwa na kiwango kikubwa cha uaminifu kwa mteja na kwa kampuni.Mtu wa Mauzo ni mmoja kati ya watu ambao wnaweza kuchangia kukua au nkuanguka kwa mteja.

Kwa mfano mtu wa masoko anaweza kufanya kazi kubwa ya kupromote bidhaa au huduma fulani na kisha mteja aada ya kuvutiwa akawasiliana na mtu wa mauzo ambaye ana uelewa mdogo wa bidhaa.Katika mawasiliano yake na mteja anajikuta badala ya kumshawishi zaidi mtija anamvuruga kwa kutokuelewa kwamba huyu mteja tayari alikuwa na ufahamu kuhusu bidhaa/ huduma na tayari ana uhitaji nayo na kitendo cha yeye kuwasiliana na wewe ni kwamba anataka kufanya uamuzi wa kununua.

Huwa katika kuwashauri wajasiriamali napenda kuwaambia kwamba badala kuajiri mtu wa Sales and Marketing waajiri mtu wa Business Development and Strategy Mtu huyu unampa kazi zote za sales and Marketing lakini unakuwa unamuandaa kujenga kitengo cha sales kilicho nje ya Marketing Hii inakupunguzia mzigo wa kuajiri watu wengi lakini unakuwa na uwezo wa kumpa huyu mtu control ya majukumu yake.Vile vile unaweza kuajiri watu wanaitwa Account managers(Account management officer) ambao nao majukumu yao yanafanana na ya BDO ingawa huyu anakuwa ni mtu ama wa Pre sales au After sales kwa kutegemea aina ya bidhaa au huduma.

Baada ya kuchokoza mada na kuwakaribisha kwa mjadala naomba nitangaze huduma kidogo na iwapo utapenda kupata mafunzo kwa ajili yako au timu yako hasa iwapo wewe unauza bidhaa ambazo zinahitaji kufanyiwa aggressive sales and marketing unaweza kuwasiliana nasi kwa email:masokotz@yahoo.com

Kuhusu SISI


Masoko Consulting ni Strategic Consulting Firm (Washauri waelekezi wa Kimkakati) ambao tunatumia mbinu za kisasa na utaalam wa kisasa katika kuwasaidia wateja wetu kutambua fursa na kuzitumia kwa ajili ya kukuza biashara zao na kukuza faida.Lengo letu ni kuwasaidi wafanyabiasha wadogo na wakati kubadilisha na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa biashara zao ili ziendane na dunia ya kisasa kwa kuwawezesha kufikia zana za kisasa,utaalamu wa kisasa na teknolojia katika kuendesha biashara zao.

Sisi tunatoa huduma ya usajili wa Majina ya biashara,kampuni,leseni,TIN number NGOs,Taasisi za Kijamii,SACCOS,Taasisi za KIDINI,Taasisi za ELIMU,Viwanda,UWEKEZAJI na pia tunatoa ushauri juu ya namna bora ya kuendesha biashara yako.Unaweza kupata huduma hizo kwa gharama nafuu.Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na:
  1. Kwanza tutakushauri kuhusu muundo wa biashara yako faida na hasara pamoja fursa mbalimbali
  2. Pili tutakufanyia utafiti na ushauri wa Jina la Biashara yako kwa kuzingatia vigezo vya SOKO
  3. Tutakufanyia Taratibu zote za usajili kuanzia Uandaaji wa Nyaraka Mpaka Kukamilika kwa Usajili Kampuni,TRA,Mashine za EFD,Vibali vya TBS pamoja na leseni
  4. Tutakuandikia Company Profile ya Kisasa kwa Lugha ya Kiingereza na Kiswahili
  5. Kama unahitaji mkopo kutoka katika taasisi za fedha tutakusaidia kufanya mchakato kwa kuzingatia mahitaji yako na vigezo vya taasisi husika.
  6. Tutakutengenezea Website ya kisasa kwa ajili ya Biashara na huduma zako.
  7. Tutakutengenezea, Logo, Business Card,Letter Head pamoja na Nyaraka nyingine za Kibiashara
  8. Tutakupatia Mfumo wa Kutunza kumbukumbu kwa njia ya Mtandao au kwenye Computer yako kwa ajili ya kusimamia Biashara yako
  9. Tutakufanyia Initial Marketing kwa Wateja wako (Inategemea aina ya biashara )wa Mwanzo ili kuwa na customer base ya kuanzia
  10. Pia tutakusaidia Mchakato wa Kufungua Bank Account kwa kutumia jina la Biashara yako (Deposit Ya Kwako)
  11. Tutakuwa nawe katika mchakato mzima wa kuendesha biashara yako mpaka itakapokuwa stable na wewe kupata uzoefu wa kutosha katika biashara yako.
Mawasiliano yetu ni:masokotz@yahoo.com au simu:+255710323060
 
Tupe gharama mtakayonipiga kwa kazi zote hizo. Biashara yangu ni kutengeneza na kuuza sabuni za kufulia na kuogea.
Habari kiongozi na samahani kwa kuchelewa kukujibu baada ya kuweka bandiko nilienda kurecharge mwili na roho na leo niko tayari kukuhudumia;

Kama nilivyoeleza awali kwamba huduma zetu zinapatikana kama huduma moja moja na kama sehemu ya package.Huduma ya package inahusisha hivyo vyote pamoja na huduma za STRATEGIC ADVISORY SERVICE kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kupitia mfumo wa RETAINER ambapo tutafanya kazi pamoja kwa kipindi cha MIEZI 6 au miezi 12 kwa gharama za malipo ya kila mwezi au kwa kutegemea aina ya biashara yako malengo yako ya mauzo na kiutendaje(KRA) na pia kwa kutegemea iwapo unataka huduma onsite au offsite.

Huduma ya offsite maana yake tunafanya kazi kwa njia ya simu na email with occassional face 2 face interaction na huduma ya ONSITE nitakuja na team yangu au utaunda team ambayo nitafanya kazi na kukaa katika eneo lako la kazi kwa kipindi cha mkataba tukifanya shughuli zote kwa pamoja.

Iwapo unapenda kufahamu zaidi kuhusu huduma zetu hizi za kipekee tafadhali tuwasiliane kwa njia ya email au namba ya simu masokotz@yahoo.com au 0710323060.

Kumbuka baada ya mazungumzo na kuelewa mahitaji yako tutakushauri iwapo kuna ulazima wa wewe kuchukua full package au la kulingana na mahitaji yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom