timetoloveyourself
JF-Expert Member
- Mar 24, 2015
- 206
- 206
Habari za weekend wana jamii,
Salamu nyingi kutoka huku shamba.
Hebu tutizame mambo kadhaa yanayomtofautisha mwanamume na mvulana kwa faida ya jamii yetu.
Ushauri kwa wanaume.
Dear men,
1. Kuwa na wanawake wengi hakukufanyi uwe mwanaume halisi, bali inakufanya uwe mvulana na kuna tofauti kubwa kati ya mwanaume na mvulana.
2. Mwanaume halisi anae mwanamke wake mmoja tu katika maisha yake. Hata ikitokea anao wengine ni wake wa ndoa na heshima yake kwa mwanamke wake haitaisha.
3. Kuwa vizuri kitandani hakukufanyi uwe mwanaume halisi. Mwanaume halisi ni yule ambae kamwe hakimbii majukumu yake.
4. Haikuhitaji kuvaa mlegezo na kutembea mabarabarani ukidhani utawavutia wanawake. Ukweli ni kwamba wavulana wadogo ndio huvaa mlegezo na wasichana wadogo wasiojitambua ndio hupenda wavaa milegezo.
5. Usiwatumie wanawake na kuwaacha. Kumbuka sheria ya "karma" what goes around must come back around.
6. Kama hutaki kumfanya awe mkeo, usimpe mimba au usimtongoze kabisa.
7. Usitii kichwa chako kidogo cha huko chini kila muda. Muda mwingi kichwa kidogo hutupeleka katika njia isiyo. Acha kichwa kikubwa kitawale kichwa kidogo.
8. Sio kila kitu unachokiona ndani ya sketi kinafaa kukikomalia ukile, sketi nyingine zimejaa nyoka ambao wanaweza wakakuuma. Jaribu ku control sex desire.
9. Usimtamani mwanamke kwa ajili ya umbo lake, maziwa yake na makalio. Hivyo vitu ni packaging tu na siku zote package huweza kuharibika.
10. Mheshimu mwanamke na kamwe usimpige hata kama ni mke wako.
11. Mwanaume wa kweli kamwe hasengenyi. Kama wewe ni msengenyaji jiweke katika kundi la wavulana.
12. Tumia muda wako mwingi kuhangaika kutafuta pesa. Mwanaume wa kweli na aliyekua kiakili hutumia muda wake mwingi kuplan na kufikiria jinsi ya kufanikiwa kiuchumi. Wanaume wapumbavu hutumia muda wao mwingi kuwaza jinsi ya kulala na wanawake mbalimbali.
13. Siku zote utafurahiwa kama utakuwa una mafanikio kiuchumi. Hakuna hata mtu mmoja atakayesheherekea kwa kuwa unao mademu wengi. Ipi faida umalize nguvu zako kujijenga kiuchumi au umalize protini yako kwa wanawake tofauti tofauti?
Kuwa mwanaume mwenye busara. Ambae ungependa Mwanao wa kiume aje kuwa kama wewe.
Wasalaam mie mkulima wa matikiti.