Tofauti kati ya mtu na binadamu

life coach

Senior Member
Apr 11, 2017
121
401
Katika hali ya kawaida wengi wetu tumekuwa tukiyachanganya maneno hayo mawili kwa kudhani kuwa ni maneno ambayo huwa na maana sawa au kumaanisha kitu kimoja.
Kimsingi maneno hayo sio sawa hata kidogo.
Zifuatazo ni maana za maneno hayo:-

1.MTU: Mtu ni jamii ya mnyama aliyepo kwenye kundi la hayawani( mamalia),jini ya maarifa/busara(homo).katika lugha ya kitaalamu ni homo sapiens ( wise man).

2.BINADAMU: Binadamu ni mtu ambaye anakiwango flani cha maadili ambayo hutakiwa na jamii husika.

Hivyo tunapozungumzia mtu basi tunazungumzia unyama na tunapozungumzia binadamu,basi tunajikita zaidi kwenye maadili.

Katika lugha ya kingereza maneno haya yanajitofautisha vizuri zaidi( human and man/person).

Nakaribisha mitazamo yenu.
 
Binadam linatokana na neno la Kiarabu Ibnu Adam (kiume) kwa kiebrania ni Ben Adam na kama ni Mwanamke ni Bint Adam. Hivyo Binadamu linatokana na kuunganishwa kwa Bin Adam Ikimaanisha mtoto (mwana) wa Adam.

Mtu ni neno linalotokana na lugha ya kibantu Ntu, likimaanisha kiumbe mwenye kujitambua na mwenye uwezo wa kuongea(human being)

Binadamu na Mtu yote yana maana moja tu tofauti itakuja pale mtu atakapotaka kuleta maana zake binafsi.
 
Asante sana,

Ila hata uko kwa waebrania ulikosema bado wanatofautisha mtu na mwanadamu pia.

Unapozungumzia adam( ambao ndo msingi wa neno Binadamu kwa mujibu wa maelezo yako),kwa waebrania basi himaanisha mtu wa kwanza kwenda kuishi katika bustani ya edeni.sasa edeni inamaanisha kiwango cha juu cha ustaarabu wa mtu,mana baada ya Adamu kukosea ndo akafukuzwa edeni,kwa maana nyepesi ustaarabu ulimshinda.

Nje ya edeni kulikuwa na watu wengi tu ambao walikuwa wakiishi,ila hawakuwa na kiwango cha ustaarabu ambao ulitakiwa kuwa nao ili kuishi edeni.

So bado mtu na binadamu wanatofautishwa kwa kiwango cha ustaarabu au maadili kulingana na jamii husika.
 
So bado mtu na binadamu wanatofautishwa kwa kiwango cha ustaarabu au maadili kulingana na jamii husika.

Ndio maana hapo mwishoni nimesema Mtu na Binadamu yote ni maana moja tu, tofauti itakuja mtu atakapotaka kuleta maana zake binafsi.
Kama ulivyoleta wewe hapo

Have a nice day.
 
Kila binadamu ni mtu lakini si kila mtu ni binadamu.

Wakati kimoja kikiwa ni sifa kingine ni kiambishikiambishi.

Kumbuka pia kuna utu na mtu na kuna ubinadamu na binadamu.. Binamu ni kitu kingine...
 
Back
Top Bottom